Watangazaji waliokuwa wanamuhoji Ruto, Tanzania hatutowapata wa kiwango kile daima

Huwa nasikiliza watangazaji wa, wasafi, efm, TBC, pale kuna vilaza watupu, wasafi pale kuna kitenge, zembwela, Ando, huwa hakuna cha maana, cha kiuchunguzi, ni porojo kama za, Kjiwe cha bodaboda!
Juzi nikamsikia, zembwela akisema, "anakula vzr Sana sasa hv kufidia maisha magumu aliyoishi akiwa mtoto"sasa nikajiiuliza kuna haja gani, ya,kusema hv kwenye national TV, haisadii chochote, ni swala binafsi Sana, halina maana yoyote kwa jamii,
Inge kuwa anasema, kutoka na na maisha magumu aliyoishi akiwa mtoto, aliamua tangu zamani, atakuwa anatoa 50% ya mshahara wake kusaidia vituo vya yatima, au anasomesha watoto kadhaa, Inge kuwa na, maana Sana, ni, taharifa kama hii ni for public consumption,
Kuna upuuzi mwingine pale efm, kipindi, cha jioni ya Leo, kuna masimulizi, ya kutunga na ujinga mwingi, nikisikia biki kipindi, huwa, nasikia kutapika,
Kuna wachambuzi wao wa mpira dada mmoja anasauti mbaya kama katuni
 
Unatarajia mtu kama baba Levo atahoji nini cha maana.

Angalia mtu kama Joe Ageyo na elimu yake kubwa ndio maana aliweza kuuliza critical questions hadi Ruto akazikwepa
 
Kabisa mkuu, huwezi linganisha na huyu
 
Yule ni zero Brain, inasikitisha mno aisee
 
Kipindi cha nyuma tulikuwa na Watangazaji wa Maaana na Waandishi pia, na ndioa maana wakawa aanapata Platform hadi kwenye vyombo vya nje kama BBC na VOA au Sauti ya Ujerumani, ila kuanzia awamu ya 5 ndio kila kitu kilichange hadi leo hii. Kwa saaa tuna Comediam, mtu kama Kitenge kutoka Mtangazaji hadi kuwa Comedian.

Angalia mtu kama Salim Kikeke kwa sasa yule ni Chawa. vyombo vya nje ndio maana kwa sasa vimejaa watangazaji kutoka Kenya tu.

Hapo kati kati ndio mambo yamekuja kuvurugika kabisa.
 
Kenya, wametuacha mbali Sana, kwa elimu, exposure, ninafanya kazi, na m Kenya kwenye shirika moja LA UN, siku ya, kwanza, nilipokutana naye,alikuwa, anafsnya matengenezo ya, milfumo ya, kusafisha making ya kunywa, pump nk, nikasema, huyu ni plumber, wiki moja, nikakuta anafunga motor za, umeme, na control circuit zake,na, anafanya kuchomelea vyuma, ikabidi nimuulize,ye ye ni kasomea nini,anasema ye ye ni technician wa umeme, Ila amejifunza pia, plumbing, carpentry, na mambo ya wastewater system,
Fundi mmoja lakini anajua vitu kibao, wa, huku kwetu kijana ana kashahada kake,mbwembwe nyingi,
Kwa mahojiano hayo ya Kenya, kina kitenge, ando, na zembwela, watapita kama hawakuona vile hawatayazungumzia maana, kile ni kiwango ambacho hawana, na hawawezi, kukipata in this life time, watazungumzia upuuzi, mwingine tu
 
Nchi hii imewahi kuwa na watangazaji hapo zanani enzi za RTD. Sasa hivi tuna wachumiatumbo na machawa. Hivi kweli akina baba levo na Juma Lokole nao ni watangazaji? Inachekesha sana🀣🀣🀣🀣
 
Nchi yoyote ambaye Uhuru wa vyombo vya habari ni wa kutosha na hauingiliwi lazima utapata watangazaji dizaini Ile Kwa kuwa wao wako huru na hawawezi kufukuzwa kazi kama majizo alivyomfukuza Gerald hamdo.
 
 

Nchi hii, kila eneo, tumepwaya.

Uchawa, unafiki na woga, huwa vina kawaida ya kupumbaza na hata kuounguza uwezo wa akili. Tasnia yabari ni miongoni mwa walioathirika sana kwenye hili.
 
Huwa sisikilizi radio siku hizi - Nimejaribu kufungua last week..kila nikipata station ni Simba,Azam & Yanga..na wote ni kawa wanafanana tu..huwezi jua utofauti - mada ni zilezile - za kitototo tu..
Nikiwa mdogo ilikuwa lazima saa 7 niskilize DW...saa 12 na nusu lazima nitafute BBC..idhaa ya kiswahili - unasikiliza habari mpaka ubajiskia raha..then kidogo kama dk 5 wanaongelea michezo kwa ufasaha kabisa.
Hivi media zetu ni kinyume - 80% michezo, 5% habari, 15% muziki...
Tatizo lipo kwa WAMILIKI pia - VISION yao ni nini?? Kama ni kupiga pesa kwa kutumia ujinga wa wananchi wanafanikiwa..na kama lengo lingekuwa kusaidia kutoa ujinga..tungeona utendaji tofauti.
 
Hivi kuna Kiongozi wa juu kutoka ccm anayeweza kuja kwenye press kavukavu?

Pengine tusiwalaumu waandishi wetu. Tulaumu na Viongozi wenyewe hawapendi/hawawezi au ni weupe zaidi
Umenikumbusha mwaka. 2010 nafikiri .. JK alipoukac ha Mdahalo wa Dk Slaa akaandaliwa wake... 😁😁😁 uaani waliotukusanya pamoja wakatuita Watanganyika sijui alitupa Nini aisee!
 
Mkuu hawa watangazaji wa kitanzania unawalaumu bure tu, hili ni tatatizo la nchi nzima kwa watu wake. Kila mmoja wetu hapa akipewa nafasi ya kuongea ndio tutajuana vzr uelewa wetu ulivyo wa hovyo. Sisi sio watu wakujifuza sana na kutafta maarifa. Kifupi ni wa vivu
 
Mbona Pascal Mayalla alimuuliza swali JPM, badala ya kujibiwa alipata vitisho. Baada ya hapo wewe kama mtangazaji unapata wapi nguvu ya kuhoji. Mfumo wa Taifa hili ni Zidumu fikra za Mwenyekiti, uchawa ulianza zamani. System ni kusifia sifia hat kama mtu anaharibu ndio maana terminology kama anaupiga mwingi unazikuta zimetaradadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…