Watanzania 38 waukana uraia wa Tanzania

Hahaa.

Umenikumbusha leo nilikuwa namsikiliza mtangazaji wa BBC World anautaja mji wa Houston Texas.

Wenyewe wamarekani wanautaja kama "Hyuston" yeye akawa anautaja "Hauston".

Nikasema Marekani ina wenyewe.
Lakini ile Houston street ya Manhattan New Yorkers huwa wanaitamka "Hauston" na siyo "Hyuston". Wanasema ni sababu hizo sehemu mbili zilikuwa named after two different people with different pronunciations in their surnames.
 
Uingereza washkaji kibao wana british passport na na passport ya Tanzania na wanazitumia zote.

Wahapahapa hawawezi kulijuwa hili, hizi ni siri za jandoni.
Kisheria ikoje mfano British immigration officer wakufume??
 
Tena sio madogo mkuu hii nchi iyangalie NiDa ukitumia pesa chap, passport ukitaka ukitumia pesa chap, vyeti vya kuzaliwa Chap yaani pesa tu ww tumia fedha.
So inamaana ugumu wanaouweka kwenye kupata hizi documents ni kutengeneza mazingira ya kujipatia rushwa , na sio usiri wala usalama?????
 
Nimekuelewa kisai, nifafanulie hapa kwa kuwa sasa wewe ni raia wa Marekani na una passport ya USA je ukienda Tz huwa una apply for visa or unatumia passport yako ya zamani ya Tz??

Je kutakuwa nakosa gani kisheria, since Tz hatuna Dual citizenship na sheria zinasema ukipata uraia wa nchi nyingine automatically wewe sio mTz tena ?
 
Sijawahi kurudi TZ tangu nichukue uraia wa US, lakini mwaka huu napanga kuja.

Kama nikija, nitakuja na passport ya US na kuingia Tanzania kwa visa.

Kama nilivyoandika, passport yangu ya Tanzania ime expire na sijai renew, sina mpango wa kui renew. Nimekaa nayo kama kumbukumbu ya safari zangu tu.

Sitaki kui renew kwa sababu nafahamu Tanzania kimsingi hairuhusu uraia pacha na kuwa na passport zaidi ya moja.
 
Siku hizi Hauwezi kuomba kujiunga na jeshi kama sio raia wa US au huna Green card.
Na umri ni kuanzia 16 hadi 35 mwisho kutegemea na Branch unayotaka kuomba ,
Mfano branch ya Marine wanachukuwa umri mdogo zaidi chini ya 28 hivi, lakini navy hadi 35
 
Lakini ile Houston street ya Manhattan New Yorkers huwa wanaitamka "Hauston" na siyo "Hyuston". Wanasema ni sababu hizo sehemu mbili zilikuwa named after two different people with different pronunciations in their surnames.
Yeah,

Unaunyaka ule mtaa?

New Yorkers wenyewe wale ukiutamka ule mtaa "Hyuston" huwa wanamind sana.
 
Hata mimi na Familia yangu (Tuko Watano) tutaukana hapo mbeleni.
Finland, Sweden au Uswisi zinatuhusu in few years to come.
Kila la kheri mkuu, hata watoto wako watakosa urithi wa ardhi yako hapa tz?
 

Uraia pacha ni muhimu sana ukitaka kila kitu kiwe kisheria. Kwa maslahi ya wengi na nchi husika.
 
Faida za kuwa na passport nyingi illegally ni kwaajili ya advantage ya Visa on arrival/visa free??
 
Faida za kuwa na passport nyingi illegally ni kwaajili ya advantage ya Visa on arrival/visa free??
Visa fee almost always si issue.

Yani mimi nikizidisha sanduku moja tu kwenye ndege fee ya extra luggage kwenye ndege tayari ni visa fee. So that is not a big deal. Yani ukienda airport na taxi nauli ya taxi tayari ni nusu ya visa fee.

Mara nyingi watu wanataka kuwa na nafasi ya kuwekeza Tanzania kama raia, si kama wageni.

Tanzania uwekezaji kama mgeni ni hela ndefu sana, au hata ukitaka kwenda kutalii mbugani kama mgeni unapigwa hela ndefu sana ukilinganisha na raia.

Ila mimi niliamua katika maisha yangu sitavunja sheria za uhamiaji za nchi yoyote hata mara moja kwa kujua, labda nivunje bila kujua tu.

Yani ni bora nitafute loophole kwenye sheria na kuitumia kuliko kuvunja sheria.
 
Faida za kuwa na passport nyingi illegally ni kwaajili ya advantage ya Visa on arrival/visa free??

Mkuu kuna passport zenye nguvu duniani ambazo unapata visa on arrival na hiyo ukiwa nayo ni poa
Hiyo nyingine ya kurudia nyumbani
Watu wengi wana multiple passports kwa sababu kuna nchi gundu sana
 
Aisee wangeruhusu uraia pacha ,kisha wange tunga sheria kama wanahisi kutakuwa na mkanganyiko au athari wanazozihofia
 
Nimekuelewa vyema mkuu, kuna makosa ya kisheria mengine ambayo ukiyafanya yanaweza kukuletea shida hata baada ya maiaka kadhaa kupita
 
Mkuu kuna passport zenye nguvu duniani ambazo unapata visa on arrival na hiyo ukiwa nayo ni poa
Hiyo nyingine ya kurudia nyumbani
Watu wengi wana multiple passports kwa sababu kuna nchi gundu sana
Na ukitaka kurudi ulipotoka unatumia pasi nyingine ? Record zinakaa vipi sawa hapa?
 
Aisee wangeruhusu uraia pacha ,kisha wange tunga sheria kama wanahisi kutakuwa na mkanganyiko au athari wanazozihofia
Mimi nilipata mchongo wa kuajiriwa Benki Kuu ya Marekani. The Federal Reserve.

Jamaa waliangalia resume yangu (Tanzania tunaita C.V), wakaipenda.Tena nilikuwa hata sitafuti kazi nilikuwa nafanya kazi sehemu nyingine.

Wakasema wananitaka nifanye nao kazi, wamependa uzoefu wangu na elimu yangu.

Ila, wameona kitu kimoja tu, kwamba nimetokea Tanzania. Lakini nimefanya kazi miaka mingi Marekani

Je, nishachukua uraia wa Marekani?

Nikawaambia bado. Hapo nilikuwa na Green Card tu.

Wakasema samahani sana, tumepemda uzoefu wako sana, elimu yako nzuri, lakini hii kazi ni sensitive sana, ina sharti la kwamba mtu atakayeifanya ni lazima awe raia wa Marekani. Haijalishi kama ana uraia wa nchi nyingine, lakini awe raia wa Marekani.

Yani Tanzania ilikuwa na nafasi ya kuwa na mtu wao Benki Kuu Marekani apate uzoefu, hata aweze kusaidia mambo Tanzania.

Hapo nilikuwa nishasubiri sana dual citizenship kwa uzalendo.

Nikasema sasa basi sisubiri tena.

Ilikuwa nina uwezo wa kupata uraia wa Marekani miaka kadhaa nyuma lakini nilikuwa nangojea dual citizenship Tanzania.

Nikaenda ku apply uraia wa Marekani, nikauchukua.

Kuanzia hapo nikafungua milango ya zile kazi zote sensitive ambazo watu walikuwa wana mind uraia.

Mpaka leo sijajutia uamuzi wangu huo.

Kama Watanzania wameshindwa kujua umuhimu wa watu walio nje, wao ndio wanakosa kitu hapo.
 
Na ukitaka kurudi ulipotoka unatumia pasi nyingine ? Record zinakaa vipi sawa hapa?

Mkuu kila kitu kinawezekana chini ya jua
Wengine wanakula ya kubrashi
Na wengine wameambiwa wasile sana

Watu wanapita kila kukicha na kuingia/kutoka
Hata Mexico wanavuka kutwa
Dunia hii huwa sioni kinachoshindikana
 
Kila la kheri mkuu, hata watoto wako watakosa urithi wa ardhi yako hapa tz?
Watarithi za huko huko.
Japo hatutaacha Asili yetu.

Kuishi nje ya nchi hakutanizuia kurudi Tz mara moja moja kuwasabahi ndugu zangu.
 
Sijui shida ni ubinafsi kwa Tz au bado tunaongozwa na watu wenye mawazo ya zama za kitambo ??/

Ni kweli aisee kazi za federal usipo kuwa raia hauwezi pata hata kama una green card
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…