Watanzania acheni roho mbaya kuhusu Zuchu na mziki wake, embu mwambieni ukweli

Zuchu ni mwanamuziki mzuri ila Nandy mi naona kama analazimisha tu kuwa mwanamuziki, she's like Ali Kiba na Jux watu ambao hawafai hata kidogo kuwa wanamuziki, wanabebwa tu tena Jux ndiyo kabisaaaa.
 
Mpaka sasa kati ya Abby na Zuchu nani anajulikana zaidi kwenye soko la nje?
Zuchu ana popularity kubwa zaidi haswa kimuziki ila globally, naona Abby ana platform kubwa zaidi maana anajihusisha na kazi za mashirika ya umoja wa mataifa pia. Ukiangalia hata kupata interview na show kubwa marekani kama kelly clarckson au kuwa posted na Beyonce kwenye insta page yake. Vyote vilimpa mileage ambayo Zuchu hajawahi kupata
 
Kupostiwa hata Miso Misondo kapostiwa na Chris Brown

Nyimbo za Zuchu zinachezwa na watu wengi nje ya nchi ukiangalia kwenye TikTok unajionea

Ni tuzo gani kubwa Abby aliwahi kwenda kuiwakilisha Tanzania nje ya bongo?
 
Sawa tuachane na shows zake za nje, tukija hata hizo za ndani nafikiri wewe kama shabiki uliitazama Wasafi Festival mwaka jana mwanzo mwisho, labda unaweza ukaniambia kama namsingizia ile sauti wewe unaona iko sawa na ndio tunayoisikia kwenye nyimbo zake
 
Zuchu apewe maua yake.
 
Bora wewe umeeleza ukweli mkuu Zuchu kwa asilimia kubwa anabebwa na WCB Media na umaarufu wa mama yake, ila angeanza mwenyewe from the scratch asingekuwa hapo hata nyimbo zake ni watu ndio wanazifanya zinakuwa hit songs, so hata za Nandy nazo mashabiki wangeamua zingekuwa hit songs vile vile sema ndio vile tena ushabiki wa kimazoea
 
Hata Nandy ana hits mfano dah, falling, mchumba, siwezi etc

Ila nadhani kinachompa Zuchu advantage ukiachana na label ni aina ya uimbaji anaofanya. Ni rahisi mtoto wa pwani aliezoea taarab kuzipenda nyimbo za Zuchu kuliko Nandy kwa hiyo Zuchu, anafikia fans wa aina tofauti zaidi ya Nandy

Ila hadi sasa bado Nandy ni A'List artist East Africa nzima na ukiongelea top 3 ya waimbaji wa kike, humtoi
 
Kupostiwa hata Miso Misondo kapostiwa na Chris Brown

Nyimbo za Zuchu zinachezwa na watu wengi nje ya nchi ukiangalia kwenye TikTok unajionea

Ni tuzo gani kubwa Abby aliwahi kwenda kuiwakilisha Tanzania nje ya bongo?
Zuchu ni mkubwa kwa Abby kimafanikio na popularity ila hajamzidi Abby platform globally kwa sababu nje ya Muziki, Zuchu hana kingine wakati ukifuatilia Abby,ana foundation nzito ya mashirika ya umoja wa mataifa kama UNICEF..Hii ndio point yangu kama ulikuwa bado hujanisoma mkuu

So, yeah Abby hajawahi pata global nomination, Zuchu ameshapata MTV EMA

Siwalinganishi maana hata Abby bado anajitafuta, unaweza muweka kwenye top 5 ya mwaka huu ila sio top 3. So, tusubiri tuone
 
Oyaa ushawahi kumsikia Zuchu akiimba live, ni kweli studio wanachuja sana sauti ila kwa Zuchu nahisi maproducer huwa wana kazi ya ziada maana siyo kwa sauti ile, uwezo wa msanii hautakiwi kuonekana studio tu bali hata jukwaani kwenye show
Hahaaa kuna kipindi alikua na yale matamasha yake alizingua kichizi watu wametoa hela ndefu kuingia harafu mtu anaingia anaimba km kabanwa mlango tangu kipindi kile hajafanya tamasha lake.Live show kwa wabongo bado sana hata huyo mondy mwenyewe hovyo tu.Ipigwe honey live bila playback unaweza kusema huyo sio zuchu ni chuzu maana hata
 
Tupe top 5 yako yenye Abby tuone
Sorry nilimaanisha kwenye upande wa female artists...

Maana ukiingiza wasanii wa kiume, ukishamuweka mariio, platnumz, jay melody, Harmo, hata wa kike wawili hawakai

Wa kike kwa mwaka huu kama sitosahau mtu, Zuchu, Nandy, Phina, Abby, Yammi..
 
Hazina msaada wowote kwenye muziki wake
Chochote chenye kumpa mtu vissibility ama publicity ni muhimu katika showbiz.... Na kwa Aby ambaye brand yake haijaegemea kwenye controversies, kuwa na back up ya charity work ni muhimu sana

Kuna wengine kama Nandy wameongeza uigizaji, kwa hiyo inasaidia kuwafanya wawe relevant
 
Tanzania tuna wanamuziki wa kike wafuatao,
1.Lady Jay dee
2.Vanessa Mdee
3.Ruby
4.Jolie, na
5. Saraphina.

The rest ni wasanii yaani waswahili wajanja wajanja, Masuperstar wa mitandaoni na skendo, Wazuri/Warembo, Wauza uchi na Viburi tu wanaoforce mambo kutokana na Mwanya walioupata.
 
Mkuu unamuongelea Zuchu yupi? huyu aliyeimba mafuta ya taa yamemwagika, mara chapati sijui imefanyaje, sijui anamkatikia nani viuno yaan vitu havieleweki😇😇😇
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…