Watanzania acheni roho mbaya kuhusu Zuchu na mziki wake, embu mwambieni ukweli

Watanzania acheni roho mbaya kuhusu Zuchu na mziki wake, embu mwambieni ukweli

Hahaaa kuna kipindi alikua na yale matamasha yake alizingua kichizi watu wametoa hela ndefu kuingia harafu mtu anaingia anaimba km kabanwa mlango tangu kipindi kile hajafanya tamasha lake.Live show kwa wabongo bado sana hata huyo mondy mwenyewe hovyo tu.Ipigwe honey live bila playback unaweza kusema huyo sio zuchu ni chuzu maana hata
Hahaha hatari mkuu ile wasafi festival yao walikuwa wanapiga makelele tu
 
Zuchu anajua sana kubadilikana na kujua soko linataka nini. Ndio maana nyimbo za Zuchu zinaimbwa kuanzia na watu wazima hadi watoto

Ukimsikiliza Zuchu aliyeimba "nisamehe" na aliyeimba "raha" tofauti kabisa

Ukimsikiliza Zuchu aliyeimba "nyumba ndogo" na aliyeimba "wana" au "sukari" ni tofauti

Huyu demu anajua sana, msikilize Zuchu kwenye "jaro" au "love"

Ni dhambi kumfananisha Zuchu na Nandy
Umemaliza kila kitu
 
Acheni roho mbaya bali semeni ukweli. Kwa Sasa Tanzania na East Africa hatuna msanii wa Maana kama Zuchu, bidada anajua kwa kweli sijui hawa wakina Nandy, Nadia Mukami na wasanii wengine wa kike ambao mnawapa maua ya uongo na ukweli wamepigwa gap sana na Zuchu tena kubwa kuanzia uandishi, sauti na hata ubunifu kawaacha palefu sana wenzie.

Kuna kipindi niliwaza sana nikasema ni msanii gani anaweza akachukua mikoba ya Vanessa Mdee na Shaa(kusema ukweli hawa wadada wawili walijitahidi sana enzi zao) hasa Vee Money na walipokuja kuachana na muziki nikahisi labda Maua Sama anaweza kutufuta machozi kwa sababu na huyu bidada enzi zake alikuwa wa moto sana sijui aliteleza wapi kama hujawai ambiwa wewe ndo ulikuwa msanii wa kutubeba sisi WATANZANIA baada ya wakina Shaa na Vee Money kuachana na mziki ila ulijiangusha mwenyewe sijui ni issue ya management au vp ila ulikuwa na kila kitu rafiki yangu.

Najua Nandy mnashangaa kwanini sijamtaja, binafsi Nandy naonaga ni msanii ambaye anaweza kutamba ndani labda na nchi za jirani tu kama Kenya, Congo na Majirani zetu wengine ila hatuwezi kumtegemea Nandy atupeperushie bendera yetu Afrika na duniani kiujumla.

Why Zuchu ukiachana na issue za management yake kwanza bidada ana kipaji kikubwa sana uwezo wake wa kubadilika badilika kama kinyonga ndio unaomtofautisha na wasanii hao wengine akiamua aimbe nyimbo za kuamsha vibes, zenye melody kali, zenye ujumbe mkali imagine ngoma za Napambana na Naringa mnaziona za kawaida ila ni ngoma za hatari zile nyie.

Zishindanishe watu hapa ila nasema Zuchu ndiye msanii bora Tanzania na East Africa.

WATANZANIA mnasubiri Zuchu afe ndo mseme ukweli! Mpeni maua yake sasa hivi.


NYIE WANAWAKE MNA KAZI. NI NANI HUYO ZUCHU?
 
Back
Top Bottom