Watanzania hatuna shukrani Mungu atusamehe kwa huu ujinga tunaofanya

Nape alikuwa mbunge kipindi cha JPM, kwa nini hakusema pale bungeni kwa sababu wabunge wetu tumewapa kinga. alishindwa ni wakati wananchi wa MTAMA tulimpeleka kutetea haki zetu.
Moja Tuache unafiki wa kuuliza hili swali la kwann hakusema kipindi hicho.

Pili hilo swali kuulizwa sasa haimaanishi kuwa jambo hilo halina umuhimu tena sababu limepita.

Tatu hii haitakiwi kuwa kipindi cha awamu ya 5 tu, hata huko nyuma mikopo ikiangaliwa ni vizuri ili nchi ifahamu wapi pa kurekebisha.

Nne na mwisho hoja si matumizi mabaya ya mkopo hoja ni uwazi wa matumizi ya mkopo. Ubaya na uzuri utakuja baada ya uwazi.
 
Ugoro!!! Umekula maharage ya wapi weweee
Nimekula maharage pale kwa mfipa, kuna watu hamtaki kukubari lakini legacy haiwezi kuvunjwa kirahisi 10(NYERERE+MWINYI+MKAPA+KIKWETE)n= 5JPM
 
Umesahau waliopotezwa, kupigwa risasi na watumishi kutopandishwa/kuongezwa mishahara na madaraja.
Huwezi kukomboa nchi huku unapandisha mishahara, lazima wananchi tufunge mikanda then tujenge uchumi. hivi yule ndugu yako angepata mkopo wa elimu ya juu, yule mdogo wako angesoma secondary bure? hiyo SGR na Ndege ungezipata wap?
 
Ukifanya ukaguzi ukakuta kuna wizi JPM yuko wapi? si bora angesema akiwa hai kwa sababu kwa sasa wa kujibu hayupo labda mama Samia, vice preisendent na prime minister
 
Akili za watanzania wengi zimebakwa mpaka zimezoea kubakwa na kuona ni haki yao.

 
Ukifanya ukaguzi ukakuta kuna wizi JPM yuko wapi? si bora angesema akiwa hai kwa sababu kwa sasa wa kujibu hayupo labda mama Samia, vice preisendent na prime minister
Hata angekuwa hai raisi hashtakiwi. Kuna mtendaji aliyehusika kufanya hilo kosa nje ya utaratibu. Mfano yaliyomkuta yule wa hai na utetezi wake wa kuagizwa.
 
Naunga mkono hoja kwa 100%. Barabara za lami zilitandazwa nchi nzima. Kabla ya Magufuli, kiijijini kwangu safari ya km 60 ilikuwa ikichukuwa nusu siku. Sasa ni saa moja tu. Umeme umezagaa na watu wanalipia kwa simu tu bila hata kuhitaji kwenda mjini. Vijana wanaangalia senema na mpira wa ligi kuu za Uingereza, Hispania , n.k. Maji ya bomba yamepatikana, kitu ambacho awali kilikuwa ni ndoto. Kliniki kuna dawa na wagonjwa wanalazwa. Ni pale tu mgonjwa akizidiwa ndiyo inabidi apelekwe hospitali kubwa zaidi mjini. Maisha ya kijijini yamekuwa bora maradufu na mtu hawazii kwenda mjini kwa kuwa kila kitu kinapatikana hapohapo kijijini. Labda kwenda kuangaza macho tu mara moja.

Ndiyo, kuna wanaolalamika lakini hawa ni wale walionyang'anywa tonge mdomoni; kwa mfano 'wafanyakazi' hewa; waliogushi vyeti; wapiga dili; n.k. Hawa na walalamike tu na ikibidi wajinyonge kabisa.

 
10 Nyerere + 10 Mwinyi + 10 Mkapa + 10 Kikwete + Samia = 5 Magufuli [emoji3]

This man was a Legend! Uthubutu mkubwa umefanyika katika awamu ya tano.Huyu mwamba ameweka standard ya uongozi/Urais unapaswa uweje.
Daah Nchi nyingi zilijifunza kutoka kwake, Mungu amrehemu ila wenye akili ndo tulimwelewa huyu mwamba
 
Ta
Tatizo watu hawatembei, hawajui nchi ilivyofunguka kipindi cha JPM.
 
Hayo yote kuna wahuni hawayaoni, wanatekeleza matakwa ya mwajiri wao ya kumtukana marehemu.
 
watanzania hata uwakumbushe aliyoyafanya jpm bado wanaona ndoto sio kweli wacha mungu atuletee ukame ndio utajua kama ulikuwa hujui
Hili nalo neno mkuu! Kikwete ukame ulizidi ni sawa na huyu mama
 
Awamu ya nne wapigaji walitumia akili sio kama awamu ya tano, MAJIZI MACHACHE ILA YALIIBA KWELI KWELI.
 
Awamu ya nne wapigaji walitumia akili sio kama awamu ya tano, MAJIZI MACHACHE ILA YALIIBA KWELI KWELI.
Waliiba kwa akili mbona waligawana hela za kifisadi kwenye magunia mchana kweupe! Ile ilikuwa akili au matope? Kisha kukana hela sio za serikali!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…