Anachokifanya January kujenga mazingira mazuri na ya kitaalamu ili aweze kuiendesha wizara yake. Mkuu, kuhusu matumizi ya maneno ya Kiingereza ndivyo ambavyo mtu yeyote anayetumia lugha yoyote anaweza kufanya ili kutokuweza kupoteza maana aliyoikusudia.
Nenda hata katika hicho Kiingereza ambacho unakisema, kimeazima maneno mengi kutoka katika lugha nyingine hasa Kilatini ili kutopoteza maana lengwa. Maneno kama; ceteris paribus, mutatis mutandis, fait accompli, functus officio, ad hoc, n.k.
Hata Nyerere akiwa kama msomi, katika hotuba zake nyingi ndivyo ambavyo alikuwa akifanya. Pole mkuu, kama nimekuharbia siku kwa kuchanganya maneno, sina njia yoyote ile ya kukusaidia.