Watanzania huu ni upole au ujinga? Kiongozi anachukuliwa meza kuu, mbele yenu mnapiga makofi!

Umejisemea kilicho akilini mwako!!
Kweli! Nimeshindwa kuelewa lengo na thrd yako ilikuwa ni nini! Yaani unaamini mukishakuwa wengi basi, ni kutumia nguvu kuwashinda askari kila kona! Halafu hujui kama ni upole au ujinga wa Watanzania! Hukutumia kichwa kwa manufaa yako. Hakuna jamii ya aina unayoitaka.
 
Umewahi kupigana na askari akiwa on duty?

Umewahi kua eneo ambalo askari wamekuja kwa ajili ya kupiga na kukamata?

Umewahi kua eneo ambalo yanapigwa mabomu ya machozi?

Umewahi kuingilia ugomvi wa askari?

Kuongea ni rahisi kweli kweli
Maswali Kama haya ni mazuri sana kujiuliza kabla ya kuchukua hatua, ila maswali haya haya ndio yataendelea kuwafanya hawa wanaofanya wanalotaka wao kwa maelekezo ya wanaowajua wao bila kujali haki na usawa waendelee kuonea watu maana wanatambua hayo maswali yamejaa vichwani mwetu na yameshatujengea hofu na kuamua kumuachia Mungu!

Wakristu wanajua Daudi ili kumshinda Goliat hakumuachia Mungu, alichukua jiwe akalifunga kwenye kombeo na Goliath alipojitokeza tu kuja kummaliza Daud, alikutana na jiwe la kwenye paji la uso lililorushwa ki ustadi kabisa na Daud. Daud angesema amuachie Mungu, nani angekufa?
 
Mkuu, tukikupa askari mmoja upigane naye sasa hivi unaweza ukampiga, tena sana tu.

Tatizo linakuja kwenye consequences za kumpiga.

Yeye sheria itamlinda kwa nguvu zote unlike wewe raia.
 
Kulikuwa hakuna haja ya jeshi la polisi kujiingiza katika huo mtego,

na kutumia nguvu kubwa kana kwamba hawa waliokutana kwa nia njema ni magaidi.

Ifike mahali jeshi la polisi lijitafakari kwa wanayowafanyia wapinzani.

Pole pole yupo huko anafanya mikutano ya nje na hakuna hatua jeshi la polisi linachukua.
 
Jeshi la polisi lisikie tu kwenye taarifa ya habari ila ukiwa mkaidi wazazi wako watalia na kusagameno.
 
Mkuu, tukikupa askari mmoja upigane naye sasa hivi unaweza ukampiga, tena sana tu.

Tatizo linakuja kwenye consequences za kumpiga.

Yeye sheria itamlinda kwa nguvu zote unlike wewe raia.
Kila mtu analifahamu hilo, lakini tutaendelea hivi hadi lini? Tuwaache waendelee kutuone tu kwasababu sheria zitawapendelea wao? Ni nani atabadilisha hali hii? Inatakiwa kitokee nini ili hali hii isiwepo? Haya ndo mambo jamii inatakiwa ijiulize na kutafutia majawabu
 
Kulikuwa hakuna haja ya jeshi la polisi kujiingiza katika huo mtego,

na kutumia nguvu kubwa kana kwamba hawa waliokutana kwa nia njema ni magaidi.

Ifike mahali jeshi la polisi lijitafakari kwa wanayowafanyia wapinzani.

Pole pole yupo huko anafanya mikutano ya nje na hakuna hatua jeshi la polisi linachukua.
Haya ndo yanayoleta hasira
 
Umewahi kupigana na askari akiwa on duty?

Umewahi kua eneo ambalo askari wamekuja kwa ajili ya kupiga na kukamata?

Umewahi kua eneo ambalo yanapigwa mabomu ya machozi?

Umewahi kuingilia ugomvi wa askari?

Kuongea ni rahisi kweli kweli
Nadhani raia hawa jakuelewa........wanachukulia rahis sana........siku wakiwa mtu kati ndio watajua kumbe hata mgambo akiwa na sare naye ni mwanajeshi
 
Watu zaidi ya 100 wapo ndani kiongozi wao anachukuliwa kutoka meza kuu wao wanapiga makofi kama vile anapelekwa kupewa cheo kumbe rumande

Eti Mungu anawaona, iko siku yataisha tu, yana mwisho hayo, hawataingia Mbinguni. Hii ndiyo misemo ya watanzania siku hizi mara wanaponyanyaswa na mfumo Imla wa awamu ya 5. Tujiulize huu ni upole au ujinga? Hii ni busara au ujinga? Huu ni uvumilivu au ujinga? Je, babu zetu wangetumia misemo mkoloni angeondoka?

Hata mbuyu ulianza kama mchicha! Wamewazuia maandamano mmekubali, wamewazuia mikutano ya hadhara mkakubali, sasa watawazuia hata mikutano ya ndani pia mtakubali
Mkuu 'lukoma', umeuliza maswali mengi, tena kwa mfululizo kuonyesha kiasi cha hisia ulichokuwa nacho wakati ukiwasilisha mada yako.

Inaeleweka.

Nimejaribu kusoma baadhi ya michango iliyowekwa kwenye mada hii, lakini kama kawaida ya JF yetu, sikuona mchango uliojaribu kujibu maswali yako. Kila jambo hapa jamvini siku hizi hata liwe mhimu kiasi gani, ni lazima litajadiliwa kishabikishabiki tu. Ni hivi ndivyo ulivyojibiwa hadi sasa.

Maoni yangu:

Hapana, waTanzania sio wajinga, siyo wapumbavu, n.k., n.k.

Chukulia mfano huo hapo, uliouweka wewe. Kiongozi akiendesha mkutano, mara ghafla mkutano unavamiwa bila staha.

Ndiyo, ingeeleweka, kama hao watu 100 wangezuia kiongozi wao kudhalilishwa na kulianzisha, kwa sababu ni hulka ya binaadam yeyote kutafuta njia za kujihami anaposhambuliwa, au akimbie toka sehemu inayohatarisha.

Katika hali iliyopo nchini sasa hivi, maoni yangu ni kwamba ni kazi bure kwa hao ndugu, kama wangesimama na kuzuia kwa nguvu kiongozi wao asichukuliwe. Uamini wangu ni kuwa hicho ndicho wanachokitafuta kitokee hao waliotumwa kukamata kiongozi.

Unakumbuka ile kesi iliyompeleka Mbowe jela na kusababisha kifo cha Akwilina? Unaweza kuona mfanano wowote hapa?

Nisije nikaandika gazeti na kukuchosha kusoma...; ni hivi, kuna njia nyingi za kukataa manyanyaso yote haya bila ya kuwaumiza zaidi viongozi na wananchi kwa ujumla. Kitu kinachokosekana ni viongozi wanaoelewa njia hizi mbadala na kuzisisitiza kwa wananchi ili zitumike wakati tukielekea kwenye hiyo ngazi kubwa unayoikikmbilia wewe.

Hayo unayotaka waTanzania wayafanye sasa hivi, haina maana kwamba ikifika mahali wakishindwa kuvumilia hayatakuwepo. Kwa sasa hivi, weka juhudi kuwaelimisha wazitumie njia nyingine, kama hiyo ya kuwadharau hao waliovamia mkutano wao na kumchukua kiongozi wao.
 
Watu zaidi ya 100 wapo ndani kiongozi wao anachukuliwa kutoka meza kuu wao wanapiga makofi kama vile anapelekwa kupewa cheo kumbe rumande

Eti Mungu anawaona, iko siku yataisha tu, yana mwisho hayo, hawataingia Mbinguni. Hii ndiyo misemo ya watanzania siku hizi mara wanaponyanyaswa na mfumo Imla wa awamu ya 5. Tujiulize huu ni upole au ujinga? Hii ni busara au ujinga? Huu ni uvumilivu au ujinga? Je, babu zetu wangetumia misemo mkoloni angeondoka?

Hata mbuyu ulianza kama mchicha! Wamewazuia maandamano mmekubali, wamewazuia mikutano ya hadhara mkakubali, sasa watawazuia hata mikutano ya ndani pia mtakubali
KWA FAIDA YA WAPENDA AMANI NA UTULIVU MPUMBAVU KAMA WEWE HATUWEZI KUKUACHA BILA KUKUPATIA KILE UNCHOSTAHILI KUTOKANA NA UPUMBAVU WAKO KWA HIYO UNADHANI WALE MIA NI WAPUMBAVU KAMA WEWE WALIONA KUNA UKWELI NDIYO MAANA WALITULIA INGEKUWA NI MWIZI WANGAPIGA MPAKA KUUWA LAKINI SERIKALI WANAIHESHIMU NDIYO MAANA WAKATII SHERIA BILA SHURUTI ILA KAMA WEWE NI JEURI NA UNAONA UNA NGUVU SANA KAMCHOMOE MTUHUMIWA YEYOTE POLISI AU MAGEREZA NDIYO TUTAAMINI HUO UPUMBAVU ULIOANDIKA HAPA, HATA HIVYO ZAID YA KUBWABWAJA NA KUANDIKA HAYA ULIYOANDIKA WEWE BINAFSI UMECHUKUA HATUA GANI ILI NA SISI TUKUFUATE KAMANDA WETU?
 
Lakini kuna kauli mnasemaga watumishi nchi hii ni wajinga/mazoba/mafala wanaonyonywa na utawala huu hafu wapo kimya tu!Kumbe na nyie ni mazoba pia hampambanii haki zenu?
 
Umewahi kupigana na askari akiwa on duty?

Umewahi kua eneo ambalo askari wamekuja kwa ajili ya kupiga na kukamata?

Umewahi kua eneo ambalo yanapigwa mabomu ya machozi?

Umewahi kuingilia ugomvi wa askari?
Kwahiyo ukiogopa polis hautakufa??
Kuongea ni rahisi kweli kweli
 
Watu zaidi ya 100 wapo ndani kiongozi wao anachukuliwa kutoka meza kuu wao wanapiga makofi kama vile anapelekwa kupewa cheo kumbe rumande

Eti Mungu anawaona, iko siku yataisha tu, yana mwisho hayo, hawataingia Mbinguni. Hii ndiyo misemo ya watanzania siku hizi mara wanaponyanyaswa na mfumo Imla wa awamu ya 5. Tujiulize huu ni upole au ujinga? Hii ni busara au ujinga? Huu ni uvumilivu au ujinga? Je, babu zetu wangetumia misemo mkoloni angeondoka?

Hata mbuyu ulianza kama mchicha! Wamewazuia maandamano mmekubali, wamewazuia mikutano ya hadhara mkakubali, sasa watawazuia hata mikutano ya ndani pia mtakubali

Ingependeza sana huu Ujasiri wako ungeanza Kutuonyesha Sisi wengine Mfano kwa Wewe kwenda mbele ili Ukifa tuzidi Kujimaarisha dhidi yao.
 
Back
Top Bottom