Watanzania huu ni upole au ujinga? Kiongozi anachukuliwa meza kuu, mbele yenu mnapiga makofi!

Watanzania huu ni upole au ujinga? Kiongozi anachukuliwa meza kuu, mbele yenu mnapiga makofi!

Unakuta Mtu na akili zake anashangilia CCM oyeee wakati kwa meiaka 5, mshahala wake haujaongezwa hata sent 1. Na wakati ghalama za Maisha zipo juu.
 
Nguvu nyingi sio solution for both sides.Lakini upande wa watawala wasipoliona hilo na kulitatua mapema,majuto ni mjukuu.
 
Wewe mbona hukufanya chochote!

Uvunje Sheria wewe, waijitokeze wengine waende jela ama kuumizwa Kwa ajiri yako, huo ndio upumbavu unaozitesa nchi nyingi za Africa

Au Umeona wapi hata huko nchi za watu wenye akiri, akikosea kiongozi mwanasiasa wanajitokeza wananchi wa kusema watalipia makosa yake, kama sio Kampeni za kijinga za Mabeberu ili tuuwane!!

Kila mtu afuate Sheria, likitokea la kuwakera wananchi wataandama wenyewe na sio kiongozi mjinga wa kisiasa amevunja Sheria Eti niandamane, Bora Tanzania sasa huo ujinga unapotea

Kila mtu Apambane na Hali yake
Umenikumbusha ujinga wa watu wa Afrika Kusini na Zimbabwe miaka 1960,1970 ,1980 eti wanapinga kukamatwa kwa Mandela na Mugabe yaani.
 
Watu zaidi ya 100 wapo ndani kiongozi wao anachukuliwa kutoka meza kuu wao wanapiga makofi kama vile anapelekwa kupewa cheo kumbe rumande
Kondoo wa Nyerere!!!!!!
 
Watu zaidi ya 100 wapo ndani kiongozi wao anachukuliwa kutoka meza kuu wao wanapiga makofi kama vile anapelekwa kupewa cheo kumbe rumande

Eti Mungu anawaona, iko siku yataisha tu, yana mwisho hayo, hawataingia Mbinguni. Hii ndiyo misemo ya watanzania siku hizi mara wanaponyanyaswa na mfumo Imla wa awamu ya 5. Tujiulize huu ni upole au ujinga? Hii ni busara au ujinga? Huu ni uvumilivu au ujinga? Je, babu zetu wangetumia misemo mkoloni angeondoka?

Hata mbuyu ulianza kama mchicha! Wamewazuia maandamano mmekubali, wamewazuia mikutano ya hadhara mkakubali, sasa watawazuia hata mikutano ya ndani pia mtakubali
Taifa la wajinga na mang'ombe ndio Hilo Lenu mnakaa na hao wanaowanyanyasa mtaani
 
Umewahi kupigana na askari akiwa on duty?

Umewahi kua eneo ambalo askari wamekuja kwa ajili ya kupiga na kukamata?

Umewahi kua eneo ambalo yanapigwa mabomu ya machozi?

Umewahi kuingilia ugomvi wa askari?

Kuongea ni rahisi kweli kweli
Hahaha Mtanzania kwenye ubora wake,unaanza kujinyea kabla tukio

Woga Ni adui mkubwa wa maendeleo yako,Tunisia,Egypt, Suadn,Algeria........nk,wameweza kwanini Watanzania Wasiweze
 
Wewe mbona hukufanya chochote!

Uvunje Sheria wewe, waijitokeze wengine waende jela ama kuumizwa Kwa ajiri yako, huo ndio upumbavu unaozitesa nchi nyingi za Africa

Au Umeona wapi hata huko nchi za watu wenye akiri, akikosea kiongozi mwanasiasa wanajitokeza wananchi wa kusema watalipia makosa yake, kama sio Kampeni za kijinga za Mabeberu ili tuuwane!!

Kila mtu afuate Sheria, likitokea la kuwakera wananchi wataandama wenyewe na sio kiongozi mjinga wa kisiasa amevunja Sheria Eti niandamane, Bora Tanzania sasa huo ujinga unapotea

Kila mtu Apambane na Hali yake


Alivunja (alikiuka) sheria gani?
 
KWA FAIDA YA WAPENDA AMANI NA UTULIVU MPUMBAVU KAMA WEWE HATUWEZI KUKUACHA BILA KUKUPATIA KILE UNCHOSTAHILI KUTOKANA NA UPUMBAVU WAKO KWA HIYO UNADHANI WALE MIA NI WAPUMBAVU KAMA WEWE WALIONA KUNA UKWELI NDIYO MAANA WALITULIA INGEKUWA NI MWIZI WANGAPIGA MPAKA KUUWA LAKINI SERIKALI WANAIHESHIMU NDIYO MAANA WAKATII SHERIA BILA SHURUTI ILA KAMA WEWE NI JEURI NA UNAONA UNA NGUVU SANA KAMCHOMOE MTUHUMIWA YEYOTE POLISI AU MAGEREZA NDIYO TUTAAMINI HUO UPUMBAVU ULIOANDIKA HAPA, HATA HIVYO ZAID YA KUBWABWAJA NA KUANDIKA HAYA ULIYOANDIKA WEWE BINAFSI UMECHUKUA HATUA GANI ILI NA SISI TUKUFUATE KAMANDA WETU?
Upumbavu haujibiwi kwa jazba tena mtu makini hapotezi muda wake kujibu upumbavu!
Kumbe maneno ni silaha kubwa sana! Ona sasa ulivyoumia kwa maneno machache tu kama umejeruhiwa na silaha ya moto kumbe maneno.
 
Ukitaka kujua kuwa jeshi la polisi lipo kila mahali jaribu kufanya vurugu tu
Hata wana waisrael walivumilia sana miaka ya kutosha ila ilifika siku farao alitoa ruhusa kwa midomo yake mwenyewe, unafikiri farao hakuwa na jeshi?
Ni mda tu ila juwa ipo siku kabla hujafa utaelewa kuwa maandiko hayakudanganya
 
Mkuu 'lukoma', umeuliza maswali mengi, tena kwa mfululizo kuonyesha kiasi cha hisia ulichokuwa nacho wakati ukiwasilisha mada yako.

Inaeleweka.

Nimejaribu kusoma baadhi ya michango iliyowekwa kwenye mada hii, lakini kama kawaida ya JF yetu, sikuona mchango uliojaribu kujibu maswali yako. Kila jambo hapa jamvini siku hizi hata liwe mhimu kiasi gani, ni lazima litajadiliwa kishabikishabiki tu. Ni hivi ndivyo ulivyojibiwa hadi sasa.

Maoni yangu:

Hapana, waTanzania sio wajinga, siyo wapumbavu, n.k., n.k.

Chukulia mfano huo hapo, uliouweka wewe. Kiongozi akiendesha mkutano, mara ghafla mkutano unavamiwa bila staha.

Ndiyo, ingeeleweka, kama hao watu 100 wangezuia kiongozi wao kudhalilishwa na kulianzisha, kwa sababu ni hulka ya binaadam yeyote kutafuta njia za kujihami anaposhambuliwa, au akimbie toka sehemu inayohatarisha.

Katika hali iliyopo nchini sasa hivi, maoni yangu ni kwamba ni kazi bure kwa hao ndugu, kama wangesimama na kuzuia kwa nguvu kiongozi wao asichukuliwe. Uamini wangu ni kuwa hicho ndicho wanachokitafuta kitokee hao waliotumwa kukamata kiongozi.

Unakumbuka ile kesi iliyompeleka Mbowe jela na kusababisha kifo cha Akwilina? Unaweza kuona mfanano wowote hapa?

Nisije nikaandika gazeti na kukuchosha kusoma...; ni hivi, kuna njia nyingi za kukataa manyanyaso yote haya bila ya kuwaumiza zaidi viongozi na wananchi kwa ujumla. Kitu kinachokosekana ni viongozi wanaoelewa njia hizi mbadala na kuzisisitiza kwa wananchi ili zitumike wakati tukielekea kwenye hiyo ngazi kubwa unayoikikmbilia wewe.

Hayo unayotaka waTanzania wayafanye sasa hivi, haina maana kwamba ikifika mahali wakishindwa kuvumilia hayatakuwepo. Kwa sasa hivi, weka juhudi kuwaelimisha wazitumie njia nyingine, kama hiyo ya kuwadharau hao waliovamia mkutano wao na kumchukua kiongozi wao.
Great! Watu wanapanic sana.
 
Ingependeza sana huu Ujasiri wako ungeanza Kutuonyesha Sisi wengine Mfano kwa Wewe kwenda mbele ili Ukifa tuzidi Kujimaarisha dhidi yao.
Ujasiri gani? Mkuu kwani unaongelea issue gani?
 
Hahaha Mtanzania kwenye ubora wake,unaanza kujinyea kabla tukio

Woga Ni adui mkubwa wa maendeleo yako,Tunisia,Egypt, Suadn,Algeria........nk,wameweza kwanini Watanzania Wasiweze
Mi nimewahi kua katika baadhi ya situations hapo. Wewe umewahi?
 
Nyinyi mababu ndiyo mnakaa mnatulaumu vijana kwanini tunaandamana wakati vyuoni tumeenda kusoma. Leo upo nyuma ya keyboard unaandika tu unachojisikia.

Haya sisi vijana tushajionjea. Zamu yenu sasa, toka kwenye keyboard nenda Msimbazi waambie umekuja kuwafundisha adabu.
 
Unataka KONDOO awe na usemi , sauti na akili ya kujiamulia. Utabaki ukiendelea kuota ndoto mchana na usiku.
 
Back
Top Bottom