Watanzania kabla ya kuanza mradi wa Bandari ya Bagamoyo tafuteni Articles za 'Lesson from Sri Lanka Hambantota Port'

Watanzania kabla ya kuanza mradi wa Bandari ya Bagamoyo tafuteni Articles za 'Lesson from Sri Lanka Hambantota Port'

Nami naanza kuona umuhimu wa sara ili Mungu aingilie kati. Huyu mama ni tatizo. Elimu ya hapa na pale hiyo!
Kwenye hizo Sara zenu msisahau kumwambia huyo Mungu sometimes awe pro-active na sio re-active unless otherwise mtakuwa watu wa kuombeana uchawi kwa mgongo wa Mungu...
 
HIzo ni sababu za watu wazembe maana ni hao wachina ambao walipewa SGR ya kuelekea Isaka.

Kazi kweli kweli. Na bado mtalaamu ananishangaa.

To be honest nina mawazo kuwa tuna shangaana. Ndiyo maana nikadhani tulihitaji kufahamiana zaidi:

Haiwezekani labda tukawa kama manyani tu wasioyaona ma**ndu yao?
 
Wewe unatengeneza laana juu ya kichwa chako kama unacho bado. Nenda shule kwanza ndipo ujue zana za utetezi kwa njia ya uchambuzi!. Lessons from Sri Lanka on China's 'debt-trap diplomacy' - ISS Africa
Kwanini mnatuletea taarifa za waliofeli? Yaani miradi mamia tuliofanya na wachina hapa bongo hawajatupora ila waje kutupora kwenye bandari?? Kwanini mnakuwa pessimistic hivi? SGR, Bwawa la Nyerere, N.k tumekopa ila sijasikia mkiogopa tutaporwa miradi kwanini mnasema tutaporwa bandari ilihali hatukopi?

Hii nchi inaendeshwa kwa propaganda kuliko facts
 
Mradi wa Hambatota ni mkopo tofauti namradi wa Bagamoyo Special Economic Zone ambao ni uwekezaji wa pamoja kati ya China, Oman na Tanzania ambapo sisi tunatoa ardhi. Kwa vyovyote vile hata mradi ukiwa na hasara sisi hatuhusiki kwenye hiyo hasara. Mada kama hizi ndio zinasababisha wengine tuamini mnaopinga mradi huu hamna akili ya kuchanganua mambo makubwa kama haya ila mnalazimisha msikilizwe japo hamna nguvu ya hoja.
Hapana.

Hata wewe bado huna uelewa kabisa na hiyo bandari ya Sri Lanka, ila unakuja hapa kudanganya watu.

Watu kuhoji mradi wa Bagamoyo kwa masharti yanayosemwa yamo kwenye mkataba siyo kosa, kwa sababu wanataka Tanzania ifaidike na mradi huo kwa kiasi kikubwa.
Tanzania iufanye huo mradi ni mradi wake, na inakaribisha hao washirika ishirikiane nao; hii ndio 'bottomline.'

Unasema hapa kwenye andiko lako kuwamba hata mradi ukishindwa Tanzania haina hasara? Hivi unaelewa unachoandika? Mwanzo umeeleza Tanzania ni mshirika katika mradi huo, halafu hapo hapo unasema mradi ukishindwa mshirika mmoja wapo hapati hasara?

Umeandika kipi cha maana katika mistari yako mitatu hapo juu hadi uhitimishe "...wanaopinga mradi hamna akili ya kuchanganua mambo...."?

Huoni kwamba wewe ndiye usiyekuwa na akili?
 
Halafu wachina walivyo, watatia fitna na kuua milango mingine yote ili ategemewe yeye tu katika hilo lango moja.

Hapo ndipo watu wataanza kufukua hizi topic na kuishia kuweweseka na kuanza kutafuta wachawi.
Na hili ndo lililopo! wazungu wanasema 'the bottom line'
 
Mkuu, labda kama utakuwa hukunielewa kabisa. Tambua kuwa:

1. Ninatambua kuwa kulikuwa miradi wa bandari ya Bagamoyo ulioasisiwa na JK awamu #4.
2. Ninatambua pia kuwa mradi huo ulipigwa munda "unceremoniously" na JPM awamu #5.
3. Mimi na wewe hatujui contents za mradi ule.
4. Ninakusoma wewe vyema kwa nini mradi ulipigwa chini.
5. Sizikatai sababu ulizozitoa, ila tu ninakwenda mbele kukuunga mkono kwa mshangao kuwa, kwamba inawezekana je?

View attachment 1832409

Kwamba kwa mujibu wako JPM aliamua kuwakomoa wachina kwa kuuzima mradi wote kwa sababu tu hawakuwa wamevutiwa na mradi wa SGR?

Hebu zirejelee kuona kama sababu hizo siyo za kitoto kabisa?!
SGR ulikuwa uwe mradi ujengwe na mchina,na jk ndo alienda china kuweka agreement kama sikosei kwa kutumwa na Jpm,
Wachina wakaanzisha harakati za ujenzi,,kisha jpm akaona waturuki ndo wajenge,,akawatoa wachina..
Baadae kama sikosei wachina walifuatwa tena ili watoe funding,,wakagoma
 
Kwanini mnatuletea taarifa za waliofeli? Yaani miradi mamia tuliofanya na wachina hapa bongo hawajatupora ila waje kutupora kwenye bandari?? Kwanini mnakuwa pessimistic hivi? SGR, Bwawa la Nyerere, N.k tumekopa ila sijasikia mkiogopa tutaporwa miradi kwanini mnasema tutaporwa bandari ilihali hatukopi?

Hii nchi inaendeshwa kwa propaganda kuliko facts
Mkuu, kuna mkanganyiko wa hali ya juu sana kuhusu jambo hili hapa JF.

Usipokuwa mwangalifu, utajikuta na wewe umemezwa kwenye mikanganyiko hiyo ya watu wasiojua lolote.

Mfano mzuri ni huo ulioujibu hapo. Kuna watu hawajui tofauti ya miradi ya mikopo, na miradi ya ushirikiano kama huu wa Bandari.

Mimi naiunga mkono Bandari ya Bagamoyo, lakini siyo kwa gharama yoyote kwa Taifa hili.

Nataka, kama washiriki katika mradi huo, Tanzania isipoteze umhimu wa ushiriki wake.

Kama Tanzania ni mshiriki, basi sioni sababu ya kuwa na mkataba ambao utakuwa unamlalia mshiriki mmoja wapo. Nataka uwe ni mkataba unaoonyesha haki kwa kila mmoja wa washiriki.

Magufuli alikuwa ni kiongozi asiyeona haya hata kusema uongo ulio wazi kabisa, lakini pamoja na kulitambua hilo, ni vyema kuangalia tena matakwa yaliyomo katika makubaliano yaliyomo ndani ya mkataba huo.

Maana ya kuandika haya ni hili la kujibu uliyoandika hapo juu: waliouasisi mradi huu wa bandari ya Bagamoyo hadi kufikia hatua ya kuweka jiwe la msingi; hawa nao ni watu ambao hatuwezi kusema siyo watu wa kuhojiwa.
Na wanaoonekana kusukuma kwa nguvu mradi huo kwa sasa ni kundi hilo hilo ninaloweza kuliita bila kusita kwamba ni kundi la maslahi la mradi huo.

Hawa watu wanaharaka sana na mradi huo. Naomba, kama alivyoeleza Rais, majadiliano yafanyike na marekebisho yafanyike kwenye sehemu ambazo zinaumiza maslahi ya taifa letu.

Kama hawa washiriki katika majadiliano watakuwa na nguvu hiyo, na Rais wetu akalisimamia hivyo, mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni mradi wetu kwa manufaa ya Taifa letu, kwa nini tuupinge?

Lakini, kama ni kunufaisha hawa (sitaki kukuhusisha nawe kwenye kundi hilo, lakini mwajina wako naona yupo huko huko, nilisoma makala yake jana), basi hata ukijengwa katika hali hiyo, tutajuwa ni akina nani waliliingiza taifa letu gizani.
 
Hili la Hambantota Port (Bandari ya Sri Lanka) nilishawahi kulielezea hapa!

In short, unlike proposed Bagamoyo Port Project, Bandari ya Hambantota ilijengwa kwa mkopo kutoka chini (as of now, taarifa zinazofahamika kuhusu Bandari ya Bagamoyo, ujenzi wake utakuwa financed under BOT Scheme).

Ukweli ni kwamba, Hambantota Port imejengwa sehemu nzuri sana, kwa sababu ipo jirani sana moja ya shipping lanes kubwa sana duniani. Katika hali ya kushangaza, Bandari ya Hambantota ikawa inakosa meli za kutosha za kuifanya bandari kuwa commercially viable pamoja na kuwa imejengwa kjirani kabisa na njia kuu ya meli zinazotoka Ulaya na America (Atlantic) kwenda Asia.

Kwavile bandari ilikuwa inakosa meli za kutosha, ikaanza kuelekea kuwa White Elephant Project! Mkopo waliochukua ukawa unazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka, na kuelekea kutolipika!!

Utawala uliokuwa umejenga bandari ile ukawa umemaliza muda wake, na ulipoingia utawala mwingine ukakuta zigo la deni la ujenzi wa bandari linazidi kuongeza!!

Kutokana na hilo, utawala mpya ukaamua kubinafsisha ili isiendelee kutia loss!!! Hakuna taarifa za moja kwa moja za kampuni ngapi hasa zilijitokeza kutaka kuuziwa hisa za bandari hiyo lakini itoshe tu kwamba, China Merchants Port Holding wakauziwa 70% ya hisa za bandari husika!!!

Hapa ieleweke kwamba, kilichofanyika Hambantonta hakina tofauti na tulichofanya Tanzania pale Container Terminal tuliyowakodishia TICTS!! Tofauti za msingi kati yetu na Sri Lanka ni:-

1. Wao wamekodisha Hambantonta baada ya kuona bandari hiyo inaelekea kuwa White Elephant Project, kiasi cha kufanya mkopo waliochukua ushindwe kulipika, sisi hatukuwa na deni lolote!

2. Tofauti ya pili ni muda... wakati sisi tumewakodishia TICTS kwa miaka 25, Sri Lanka wamekodisha kwa miaka 99 (sijui walikuwa wanafikiria nini)!

REMEMBER: Bandari ya Hambantota ilibinafsishwa 4 years baada ya kutangazwa kwa the so-called Belt and Road Initiative (BRI)... a Chinese Initiative inayolenga kuiunganisha China na mataifa mbalimbali duniani kupitia infrastructure! Moja ya infrastructure zinazopewa kipaumbele kwenye BRI ni bandari.

Kwa bahati mbaya sana, Marekani na Washirika wake (ingawaje wameshaanza kusalitiana) wanaiogopa BRI kama ukoma!! Sasa kwavile Hambantota Port ilibinafsishwa katikati ya kilele cha BRI, habari ambayo ilisambazwa duniani haikuwa tena "Sri Lanka wanabinafsisha bandari" bali ikawa "Wachina wameipoka Bandari ya Sri Lanka" ili kujilipa deni lao!!

Yaani vyombo vya magharibi vikataka kutoa picha kwamba, kilichofanyika ni kama kile kinachofanywa na taasisi kama Bayport pale wanapokudai!!

The New York Times kwa mfano, waliandika:-
Yes, though feasibility studies said the port wouldn’t work. Yes, though other frequent lenders like India had refused. Yes, though Sri Lanka’s debt was ballooning rapidly under Mr. Rajapaksa.

Over years of construction and renegotiation with China Harbor Engineering Company, one of Beijing’s largest state-owned enterprises, the Hambantota Port Development Project distinguished itself mostly by failing, as predicted. With tens of thousands of ships passing by along one of the world’s busiest shipping lanes, the port drew only 34 ships in 2012.

And then the port became China’s.

Kinyume na The New York Times ambayo habari yao imekaa kishabiki na kichochezi zaidi, wanaojali taaluma, The Financial Times la Uingereza wanaandika:-
The $1.3bn port was opened seven years ago using debt from Chinese state-controlled entities. But it has since struggled under heavy losses, making it impossible for Colombo to repay its debts.

In 2016, Sri Lankan ministers struck a deal to sell an 80 per cent stake in the port to the state-controlled China Merchants Port Holdings.

Baada ya ubinafsishaji huo, current performance ya Hambantota Port huioni kupitia magazeti kama The New York Times lakini angalau, India Today wanatujuza:-
In the pandemic year of 2020, the RO-RO transshipment hub has seen rapid growth in vehicle volumes while bulk cargo volumes have also grown by 44 per cent. Total RO-RO units handled during 2020 fell to 388,031 from 411,027 as coronavirus hit global shipping and Sri Lanka banned vehicle imports but transshipment have started to grow rapidly in recent months.

By December 2020, volumes had pickup up to 58,996 units which is a rise of 25.9 per cent compared to the corresponding period in 2019, driven almost entirely by international volumes as imports dwindled to 215 units in 2020 from 4,214 a year earlier. In January 2021 the port had handled 55,068 units, up 29 per cent from a year earlier. Vehicles coming from India, Korea, Japan, and China are discharged at Hambantota for transshipment to the Middle East, South Africa, and South America.
Sasa tukiacha mapungufu ya mkataba husika ambayo watu wa nje hawawezi kuyajua zaidi ya Wachina na Sri Lanka wenyewe, lengo la kubinafsisha hiyo bandario ilikuwa ni kuifanya iwe commercially viable kama inavyoonekana kutoka kwenye habari ya India Today hapo juu!

Na ikumbukwe kwamba, media hizo hizo za US zilikuwa zinaandika kwa mwelekeo huo huo pale Serikali ya Ugiriki ilipokaribia kufilisika, na hatimae kuamua kuuza hisa za Bandari ya Piraeus kwa Mchina!!

Leo tunapoongea, Bandari ya Piraeus ndio leading Mediterranean Port, huku ikikaribia kuwa among Top 5 Performing Ports in Europe, wakati miaka kadhaa tu iliyopita, haikuwa hata among Top 15!!!
 
Srilanka haikushikiwa bandari na china,Exim bank walikua wanaidai sri lanka dola bilion 1.4.
Sri lanka wakaona hawawezi kulipa kwa speed,bandari ilikua haingizi pesa haraka,wakatafuta kampuni iitwayo china metchant wakaikodisha bandari kwa miaka 99 na wakalipwa pesa cash bilion 1 na ushee usd,
So badala ya kuilipa Exim bank,hizo pesa wakaingiza kunako foregn reserve currency ili kubalance hesabu,,
Hivyo sri lanka bado hawakulipa deni,,bandari wamelease kwa kampuni nyingine ya kichina na wakalipwa cash
 
Watanzania kabla ya kuanza huo mradi wa Bandari ya Bagamoyo naomba tafuteni Articles za LESSON FROM SRI LANKA Hambantota port.

Kama hizo article umezipata please tunaomba uzishare ndani ya huu uzi.

Wabongo mnataka mjidai mnawazidi akili wa SRI LANKA ninyi.

Tunataka siku mkianza kulia tulie sote.

Tafuteni Articles tuanze kusoma
Kwamba eti Wachina watanyang’anya mali za taifa endapo mradi huo utapata hasara kama ilivyokuwa kwa mradi wa Bandari wa Sri Lanka. Ukweli ni kwamba mradi wa Bagamoyo sio sawa na mradi wa Sri Lanka au mradi wa ujenzi wa Reli ya Kenya. Tofauti na miradi hiyo miwili ya Kenya na Sri Lanka, mradi wa Bagamoyo unatekelezwa kwa njia ya uwekezaji (FDI) kwa asilimia 100, wakati ile miradi ya Kenya na Sri Lanka inatekelezwa kwa mikopo ambayo nchi inawajibu wa kuweka dhamana (sovereign guarantee)

Kwa hiyo mtuache na mradi wetu.
 
Kuna watu wanawaza rushwa tu. Akili wamepewa na Mungu hawataki kuzitumia kufanya kazi na kupata pesa, they don't think beyond today.
Bandari ya Dar ipo haitumiwi to full capacity watu wanataka wajenge nyingine.
Tumetupa hela kule chattle kwa kujenga uwanja wa ndege ambao Ni Kama Gbadolite, people don't want to learn..
One thing is clear, if you don't learn from examples, you will be another example.
Wakenya wameuza Mombasa kwa Bei ya kutupa, Sri Lanka wanajuta. Tutake mifano ipi Tena ????
 
Hakuna haja ya kuhofia eti mradi ukikamilika basi JPM atafunikwa ,hatuko hapa kulinda lagacy za watu⛹️👌,tuko kufanya maendeleo ya nchi yetu,jpm alifanya yake,mazuri na mengine yasiyo mazuri,tuache na wengine wafanye yao,hamna haja ya kuhofia eti watapata sifa kumzidi jpm,,hapa hatutafuti sifa za watu, na safari hii miradi ya maendeleo itafanywa bila kujali majungu ya watu wenye nyoyo za korosho
 
Kuna watu ambao mpaka muda huu wanapambana kumiliki vyoo wanajifanya kushindana na macho madogo.

Hakuna watu corrupt kama macho madogo.

Imetuchukua muda kupambana nao kwenye tenda za ujenzi wa barabara sidhani kama tuna personell competent kuchuana na hawa jamaa.
Issue sio akili, sio kweli wavimba macho wanaakili kiviiile kiasi cha kutuzidi...sio hao wavimba macho tu hata wazungu sio kweli kama wana akili kutuzidi waAfrica au wabongo..

Shida kubwa ya Africa ni tamaa na rushwa, viongozi wetu wanakula mlungula then wanasign tu bora liende kwa maslahi ya matumbo yao........
 
Knowledge is power. If you dont want knowlege means your life is a mistake. Sishindani na watu wasioona mbele. Ninayo namna nyingine ya kufanya kwa kuwa mawazo ya kifisadi na kipumbavu juu ya taifa yatatuathiri hata tusiohusika. Sitakaa kubishana na mawazo ya kijinga.

Jibu la maswali yako, fanya tu kutafuta maarifa utajua nini watu wanasema.
Kwanini mnatuletea taarifa za waliofeli? Yaani miradi mamia tuliofanya na wachina hapa bongo hawajatupora ila waje kutupora kwenye bandari?? Kwanini mnakuwa pessimistic hivi? SGR, Bwawa la Nyerere, N.k tumekopa ila sijasikia mkiogopa tutaporwa miradi kwanini mnasema tutaporwa bandari ilihali hatukopi?

Hii nchi inaendeshwa kwa propaganda kuliko facts
 
Kwamba eti Wachina watanyang’anya mali za taifa endapo mradi huo utapata hasara kama ilivyokuwa kwa mradi wa Bandari wa Sri Lanka. Ukweli ni kwamba mradi wa Bagamoyo sio sawa na mradi wa Sri Lanka au mradi wa ujenzi wa Reli ya Kenya. Tofauti na miradi hiyo miwili ya Kenya na Sri Lanka, mradi wa Bagamoyo unatekelezwa kwa njia ya uwekezaji (FDI) kwa asilimia 100, wakati ile miradi ya Kenya na Sri Lanka inatekelezwa kwa mikopo ambayo nchi inawajibu wa kuweka dhamana (sovereign guarantee)

Kwa hiyo mtuache na mradi wetu.
Huo uwekezaji ni kwa maslahi ya nani ikiwa mchina ataendesha hiyo bandari kupitisha mizigo yake bila mamlaka za nchi kuona kinachoendelea, unajua athari za kiusalama na kimaslahi kwa nchi kuachia lango lake la bandari liendeshwe na nchi nyingine bila yenyewe kujua chochote kinachoendelea......hovyo kabisa!
 
Acheni ushamba nyie mapromwendazake hujui chochote.

Marehemu aliwaharibu akili nyie
 
SGR ulikuwa uwe mradi ujengwe na mchina,na jk ndo alienda china kuweka agreement kama sikosei kwa kutumwa na Jpm,
Wachina wakaanzisha harakati za ujenzi,,kisha jpm akaona waturuki ndo wajenge,,akawatoa wachina..
Baadae kama sikosei wachina walifuatwa tena ili watoe funding,,wakagoma
Mkuu, Elungata,

Yanayotokea sasa ni ushahidi tosha kuhusu viongozi hao wawili: Kikwete na Magufuli, kulikuwa na jambo kati yao, na matokeo yake ndiyo haya.

Kikwete ndie mwanzilishi wa miradi yote miwili, SGR na hiyo bandari ya Bagamoyo (hii iliizima ile ya Mwambani Tanga, na sababu zake hazijulikani hadi leo).

Katika mradi wa SGR, Kikwete kuondoka madarakani, ilikuwa kazi ianze ya ujenzi wa reli hiyo. Tulianza kusikia habari za Magufuli kulala na mafaili mvunguni mwake akiyasoma usiku kucha, na kuibuka na sababu kwamba mikataba yake ilikuwa haifai, kwa hiyo ndipo waturuki wakachukuwa sehemu ya ujenzi wa mradi huo.
Hili liko wazi wala halina mkanganyiko wowote. Tusichojuwa ni wachina walikuwa wamepanga kutudunda vipi juu ya mradi huo.

Kwa hiyo hatujui kama madai ya Magufuli yalikuwa kweli au hapana; lakini pia hatujui kama Kikwete alikuwa ametuandalia kuliwa, hilo nalo hatulijui.

Hali iko hivyo hivyo, juu ya huu mradi wa bandari ya Bagamoyo. Madai ya Magufuli angalau yapo yametamkwa, hata kama hatujui ukweli wake hasa upoje.

Kwa upande wa Kikwete, inaonekana dhahiri sasa, kuondoka kwa Magufuli kumewapa nguvu washiriki wote katika mradi huo kuendeleza walipokuwa wameyaachia yaendelezwe kwenye awamu ya Magufuli, lakini yakazimwa.
Sasa hivi wanatumia nguvu nyingi sana kuusukuma huu mradi ili wanufaike na walichokuwa wamekitegeshea. Hili nalo lipo wazi.

Ninachomwomba Mama Samia, asipuuze alichokiona Magufuli, kama kipo (pamoja na uongo wake). Na asifumbie macho na akili hili kundi la wapigaji lililopo chini ya Kikwete. Namwomba sana atazame maslahi ya nchi yetu bila ya kujali makundi haya mawili ya viongozi hao.

Mkataba wa bandari ya Bagamoyo ni lazima uwe ni kwa maslahi ya nchi yetu, na si kwa maslahi ya kundi la watu.
 
The issue is ,

Is Samia that competent to discover all that??

Sidhani.
 
Back
Top Bottom