Kuna wakati tulikuwa chini sana kiuchumi nadhani kipindi cha marehemu Mkapa akaja na sera ya uwekezaji, zilikuwa zinatoka hoja kama hizi na watetezi walilenga kuamsha uchumi na kuongeza ajira zaidi lakini mapato zaidi kwa serikali. Na matokeo ya sera ya uwejezaji ule kila mtu ameona uzuri na ubaya wake.
Sasa mradi wa bagamoyo unakataliwa kwanini ?
Vipengere vya mkataba au hauna faida zinazotarajiwa?
Ama kuna maslahi binafsi yanatugawa?
Nadhani faida kuu ya mradi wowote wa serikali sio tuu mapato ya moja kwa moja kama wengi wanavyodhani,
bali ni fursa ambazo nchi na Mwananchi kwa ujumla watanufaika nazo, lakini hilo haliondoi kuhakikiwa usalama wa nchi na rasilimali zake. Sasa kwa mfano huo wa uwekezaji,
Bagamoyo ni moja ya mradi Mkubwa wenye fursa nyingi tuu lakini utaongeza GDP ya serikali ajira pia kukua kwa sekta nyingi kutokana na mradi huo mkubwa, labda kama kuna maslahi binafsi ya watu basi,
Tuchukue maneno ya mwendazake kama wakeup call tuanzie kurekebisha hapo. Nawakilisha.