Watanzania kabla ya kuanza mradi wa Bandari ya Bagamoyo tafuteni Articles za 'Lesson from Sri Lanka Hambantota Port'

Watanzania kabla ya kuanza mradi wa Bandari ya Bagamoyo tafuteni Articles za 'Lesson from Sri Lanka Hambantota Port'

Kuna wakati tulikuwa chini sana kiuchumi nadhani kipindi cha marehemu Mkapa akaja na sera ya uwekezaji, zilikuwa zinatoka hoja kama hizi na watetezi walilenga kuamsha uchumi na kuongeza ajira zaidi lakini mapato zaidi kwa serikali. Na matokeo ya sera ya uwejezaji ule kila mtu ameona uzuri na ubaya wake.
Sasa mradi wa bagamoyo unakataliwa kwanini ?
Vipengere vya mkataba au hauna faida zinazotarajiwa?

Ama kuna maslahi binafsi yanatugawa?
Nadhani faida kuu ya mradi wowote wa serikali sio tuu mapato ya moja kwa moja kama wengi wanavyodhani,
bali ni fursa ambazo nchi na Mwananchi kwa ujumla watanufaika nazo, lakini hilo haliondoi kuhakikiwa usalama wa nchi na rasilimali zake. Sasa kwa mfano huo wa uwekezaji,
Bagamoyo ni moja ya mradi Mkubwa wenye fursa nyingi tuu lakini utaongeza GDP ya serikali ajira pia kukua kwa sekta nyingi kutokana na mradi huo mkubwa, labda kama kuna maslahi binafsi ya watu basi,
Tuchukue maneno ya mwendazake kama wakeup call tuanzie kurekebisha hapo. Nawakilisha.
Hivi mradi wa NSSF daraja la kigamboni lile limeongeza kitu gani cha mwananchi kujivunia?
 
Kila siku naliombea taifa, Mungu asaidie majitu majinga jinga kama hili yapungue lkn cha ajabu yanazidi kuongezeka, we mpumbavu kasachi uzi wa bandari ijengwe au isijengwe? Mule kuna madini yamechambuliwa we kasome page zote 17 naamini akili yako itafunguka upya jinga wewe.
nawezakuwa mjinga kwa ufahamu wako,lakini wewe ni mpumbavu kwa cheti rasmi.

unadhani hata ukianzisha mada kwanini ushoga uruhusiwe, watakosekana watu wa kusimika hoja zenye mashiko!!!!

swala hapa linabaki,nini lengo la mradi huo,faida ni kwa tz au muwekezaji??niwakumbushe vindege msola kama wewe $10bln sio pesa ya kununulia chupi.
 
Huyu jamaa alitumbuliwa bure tu, kumbe kichwa chake kimetulia namna hii.....
Jamaa kaongea vitu sensible kabisa ila wachumia tumbo wanaona sawa tu! Sababu washaseti michongo hela ziwe zinaingia tu kwenye familia zao kama mgao!
 
Maslahi mapana yatakuwa kwa familia za viongozi ambao wanaenda kuubariki huo mradi! Wengine tegemeeni kuwa vibarua tu 😂😂😂

Hizo ni haki ya msingi ya kila Mtanzania kuujua vipengele vyote vya huu mkataba. Wenyewe wanaona ni haki yao kuufichaficha.

Hawaweki wazi Faida na Hasara, (pros and cons) tunawezaje kupunguza au kuzitoa kabisa hasara.

There is no free lunch in this world.
 
Watanzania kabla ya kuanza huo mradi wa Bandari ya Bagamoyo naomba tafuteni Articles za LESSON FROM SRI LANKA Hambantota port.

Kama hizo article umezipata please tunaomba uzishare ndani ya huu uzi.

Wabongo mnataka mjidai mnawazidi akili wa Sri Lanka ninyi.

Tunataka siku mkianza kulia tulie sote.

Tafuteni Articles tuanze kusoma
wabunge TALE TALE, KIBAJAJI, MSUKUMA , watafute wasome na waseme bungeni, sisi tumewatuma watuwakilishe huko.
 
Hizo ni haki ya msingi ya kila Mtanzania kuujua vipengele vyote vya huu mkataba. Wenyewe wanaona ni haki yao kuufichaficha.

Hawaweki wazi Faida na Hasara, (pros and cons) tunawezaje kupunguza au kuzitoa kabisa hasara.

There is no free lunch in this world.
Wataufosi tu wapige hela za mkupuo paap! Unakuta mtu kashaseti apige zake Trillion moja mkataba ukisainiwa kisha wagawane gawane hela hio!
 
Ata wale waliopo bungeni wanaushadsdia kwasababu walienda ziara siku 21 huko nje na wapo kwenye kamati ya miundombinu wakalishwa presentation ya nusu saa hivi then wakapitishiwa mlungula ndiyo waliporudi kila mtu anantaka uendelee ule mradi alafu wanasema Wachina wanataka kuisadia nchi yetu!

Sent using Jamii Forums mobile app

Mmmmmm wasomi feki wa Tz,ninachojiuliza hv hawa ndo wanajua sana siri za huyo bandari kuliko jpm? Walaji mko kazini.
 
La Muhimu nchi si ya viongizi ni yetu sote. Uzuri tunayo mifano Mingi ya uharamia wa China Kwa nchi zetu za Africa. Nashauri haya.
1.tusikilizeni Sisi watanzania tunataka nini
2.mkiweka Pamba masikioni, wekeni hiyo mikataba hadharani tuione.
3.kama mtatusikuliza anzisheni shares watanzania popote walipo Kwa kushirikiana na serikali na baadhi ya wadau binafsi tujenge mtadi. Mbona Ethiopia wameweza kujenga DAM.

Otherwise the project has some signs of being curse na utawagarimu ama viongizi ama chama chao .hizi nginjera za kina ndugai tunajua kilicho Nyuma yao
 
Mradi wa Hambatota ni mkopo tofauti namradi wa Bagamoyo Special Economic Zone ambao ni uwekezaji wa pamoja kati ya China, Oman na Tanzania ambapo sisi tunatoa ardhi. Kwa vyovyote vile hata mradi ukiwa na hasara sisi hatuhusiki kwenye hiyo hasara.

Mada kama hizi ndio zinasababisha wengine tuamini mnaopinga mradi huu hamna akili ya kuchanganua mambo makubwa kama haya ila mnalazimisha msikilizwe japo hamna nguvu ya hoja.
Mkuu umakini lazima uwepo tu. Nchi hii ishaingia mikataba mingi sana kama ya MANGUNGO na KINJIKITILE halafu mnataka watu wasijadili? Vip kuhusu gesi ya mtwara kuna la maana hapo? Bagamoyo jumong akicheza ikakula kwetu? umakini uwepo wa kutosha ili manufaa yawezo isiwe kama gesi ya mtwara ambayo wanamtwara waliambiwa watakuwa kama ulaya lakini mpaka leo hamna kitu.
 
Kuna thread humu imefafanua vizuri kwa kupangua propaganda za babu yenu mwendakuzimu we ufukunyue tu utaelewa.
Hata we kuzimu hiyo inakusubiri Kwa hamu. Inaonekana hata Imani huna so imagine kuzimu plus Moto
 
La Muhimu nchi si ya viongizi ni yetu sote. Uzuri tunayo mifano Mingi ya uharamia wa China Kwa nchi zetu za Africa. Nashauri haya.
1.tusikilizeni Sisi watanzania tunataka nini
2.mkiweka Pamba masikioni, wekeni hiyo mikataba hadharani tuione.
3.kama mtatusikuliza anzisheni shares watanzania popote walipo Kwa kushirikiana na serikali na baadhi ya wadau binafsi tujenge mtadi. Mbona Ethiopia wameweza kujenga DAM.

Otherwise the project has some signs of being curse na utawagarimu ama viongizi ama chama chao .hizi nginjera za kina ndugai tunajua kilicho Nyuma yao
Point namba tatu ni ya msingi sana. We have got to think independently na kufanya vitu kwa namna yetu.
 
Watanzania kabla ya kuanza huo mradi wa Bandari ya Bagamoyo naomba tafuteni Articles za LESSON FROM SRI LANKA Hambantota port.

Kama hizo article umezipata please tunaomba uzishare ndani ya huu uzi.

Wabongo mnataka mjidai mnawazidi akili wa Sri Lanka ninyi.

Tunataka siku mkianza kulia tulie sote.

Tafuteni Articles tuanze kusoma
Mama Samia na serikali yake watatukosea sana watanzania kama wakijifanya hawasikii. Wachina ni wabaya sana kiuchumi zaidi ya wazungu wa Ulaya.
 
Hata we kuzimu hiyo inakusubiri Kwa hamu. Inaonekana hata Imani huna so imagine kuzimu plus Moto
Huyo mwache maana akili kaziweka mfukoni kazi yake kuongelea wafu. Hajua amnatakiwa kutengeneza mapito yake, Yeye kila siku anaongelea mwendakuzimu, hajua hata anachoongelea,Kazi yakekujihesabia haki yeye mwema wenzie wabaya.
 
Wataufosi tu wapige hela za mkupuo paap! Unakuta mtu kashaseti apige zake Trillion moja mkataba ukisainiwa kisha wagawane gawane hela hio!

Nguvu ya umma bado ni kubwa, watu wanaweza kuweka pressure uwekwe wazi mkataba.

Tusirudie mambi ya mradi wa gesi (90% inaenda kwa wawekezeji), IPTL na Tanesco scandal, mikataba hovyo ya madini na Acacia, Meremeta, radar mbovu.

Imetugharimu na inaendelea kutugharimu matrillioni ya shilingi.
 
N
nawezakuwa mjinga kwa ufahamu wako,lakini wewe ni mpumbavu kwa cheti rasmi.

unadhani hata ukianzisha mada kwanini ushoga uruhusiwe, watakosekana watu wa kusimika hoja zenye mashiko!!!!

swala hapa linabaki,nini lengo la mradi huo,faida ni kwa tz au muwekezaji??niwakumbushe vindege msola kama wewe $10bln sio pesa ya kununulia chupi.
ndio maana nikasema we ni lipumbavu huna akili, unataka biashara ya kufaidika upande mmoja utaipata dunia ya nani? Ktk hiyo bandari wanufaika watakuwa wore tz, omani na China, jinga kweli unapinga kitu usichokielewa.
 
Back
Top Bottom