Uliwahi kuona wapi Nyerere amewekeza kwenye Elimu zaidi ya zile zile za wakoloni?
Nadhani ni vema kabla ya kujenga hoja ukajiridhisha kuwa kama una utashi na taarifa za kutosha kwaajri ya kutetea hoja yako.
Okay kwa kifupi wakati Nyerere anapewa Tanganyika kulikuwa na gepu kubwa sana la wasomi wa kutake over serikali na kushika majukumu baada ya malkia kumpa inchi. Kwa wakati ule walifosi sana watu kusoma na hata wengine kupelekwa nje ili kupata watendaji wa serikali.
So mfumo wa elimu ya wakati huo ulitengenezwa kwaajiri ya kukidhi mahitaji ya watendaji kwa wakati huo. Lakini pia mitaala ilitengenezwa kwaajiri ya raia waliopo vijijini. Kulikuwa na elimu za kilimo na ufugaji,elimu ya uraia ,ujamaa (sio ujima) na kujitegemea, na elimu za mahesabu. Mimi mzee wangu alikuwa na mavitabu kibao ya wakati huo.
So nadhani unachofanya wewe ni kutazama kufeli au mkwamo wa elimu ya sasa kwa muktadha wa elimu ya miaka hiyo,unakosea vibaya. Imeshapita miaka mingapi tokea uhuru? Nyerere alitoka lini madarakani, amefariki lini,je vikao vingapi vya bunge vimepita tokea bunge la kwanza, kwahiyo nyerere ndie anaepanga na kutaka elimu iweje au watu waliowaachia nafasi?
Aliona ni Bora kutumia pesa za Nchi kwenda kuanzisha vita ya Idd Amin kumsaidia Jamaa yake Obote.
Hakwenda kuanzisha vita tulivamiwa na Iddi amini maeneo ya kagera (nenda kasome hostory vizuri) na video zipo iddi amini akisema kwamba Tanganyika ilichukua eneo la Uganda ni lazima walichukue kutoka Tanganyika.
Wewe unajua kwamba iddi amini alienda hadi kwa malkia Elizabeth huyu aliyefariki juzi hapa kumuomba vifaa vya kivita ili aivamie Tanganyika kunyang'anya kagera, malkia akamkatalia akaenda kwa Gaddafi ndio akampatia silaha, askari na vifaru na mapantoni ndipo iddi amini akavamia kagera, ukitaka afanyaje akae kimya? 🤔
Hivi ninyi vijana wa siku hizi mbona mnatia mashaka uwezo wenu wa kufikiria, internet ipo ,majibu yapo why mnakuwa waropokaji na watunzi wa majibu vichwani bila hata shuhuda? Video zipo iddi amini anaongea na waandishi wa habari kabisa anawaambia atavamia Tanganyika? Wewe unasema Nyerere alikwenda kuanzisha vita haya tuambie alikuwa na sababu zipi kuanIsha vita? Mnatoa wapi upuuzi huu kwenye vichwa vyenu?
Aliona Bora msalie wajinga ila atymie pesa za Umma ma Rasilimali watu nk kusambaza wanajeshi nk kupigana kwenye Nchi zingine.
Unaona sasa ulivyokuwa hauna taarifa?😂 Vita vya Tanganyika na Uganda kwa taarifa yako bajeti ilikuwa ni chini sana kwasababu hatukuwa na jeshi kubwa kihivyo na silaha zilizotumika ni zile zile za urithi kutoka kwa mjerumani na mwingereza baada ya ukoloni.
Kwa taarifa yako, sehemu kubwa ya wapiganaji walikuwa ni raia wa Tanganyika waliojitolea kusaidia jeshi baada ya kupewa mafunzo ya muda mfupi, cuba,china,kenya,msumbiji, na urusi walitoa pia sapoti kubwa. Silaha nyingi tulikwenda kuzichukua kwenye kambi za askari wa Iddi amini na kuwanyang'anya kwasababu hawakuwa vizuri kivita walikuwa walevi hawana mbinu na hawana maandalizi.
Tanganyika tulisaidiwa training na Israel kabla ya vita na wakati wa vita Israel na baadae cuba so tulikuwa vema sana kwenye guerilla style. Ukisema tulitumia pesa nitakuuliza shilingi ngapi useme.
Of course vita ilidumaza uchumi wetu ila sio kwa kiwango ambacho wewe unataka kujiaminisha maana ilikuwa ni vita ya mwaka m'moja na muda wote huo Tanzania ilikuwa inatembeza mkong'oto bila kurudi nyuma. So jipange tena na hizo hadithi za kuambiwa na wazee wanywa kahawa 😂😂
Kimsingi hana lolote la maana Aliwahi fanya kwenye mambo ya Maendeleo zaidi ya kukandamiza Wapinzani wake na kuwapoteza.
Hapa sasa umekuwa muwazi kuwa hauna shukurani na si ajabu hata wazazi wako huwa unawatamkia haya haya kuwa hajakusaidia lolote tokea wa kuzae wakusababishia umasikini ulitakiwa uzaliwe ulaya ndio ungeridhika.
Ukisema Nyerere hajafanya lolote basi haina haja ya kujadili lolote kwasababu nitakuwa naongea na mtu ambaye sio tu haijui historia ya taifa anapoishi ila hata yeye hajui yupo taifa gani ns limetokea wapi. Pole sana.