Watanzania Kama KARNE hii tupo hivi nasadiki kusema Mwalimu Nyerere(Baba wa Taifa) alipambana Sana

Watanzania Kama KARNE hii tupo hivi nasadiki kusema Mwalimu Nyerere(Baba wa Taifa) alipambana Sana

Mkuu kwahiyo Kwa kufanya hayo uliyo yaandika ndiyo unajiona unaakili kumzidi Baba wa Taifa?

Kiasi kwamba kumsema kwamba hakuwa lolote wala chochote kwenye hili Taifa?
Sio swala la kujiona na kumzidi ni suala la kulinganisha alitakiwa kufanya nini na alifanya kipi.
 
Ukitazama ujinga tulionao Watanzania wengi katika karne hii utagundua kuwa Mwalimu Nyerere alipambana sana.

Hakika Baba wataifa alipata tabu sana kusugua kutu na Msasa kwenye vichwa vya Watanzania.

Imagine ujinga wakipindi chake ulikuwaje kama hivi sasa ni 2025 Watanzania karibia wote tunaujinga mkubwa namna hii, Yani kuanzia ngazi za(familia) na kila kona ni ujinga ujinga, umbea umbea tu Lord have Mercy.
Ndugu mleta mada nadhani ungetofautisha uzalendo na ujinga. Wananchi wa zama za J. K. Nyerere kweli wengi walikuwa wajinga kielimu ila walikuwa wazalendo na wafianchi kwelikweli kuanzia ngazi ya kaya mpaka taifa na kiwango cha ubinafsi kwa viongozi wa umma kilikuwa chini mnoo. Kiongozi wa umma kweli alimaanisha na aliheshimika hivyo na alikuwa kioo cha jamii kwelikweli. Kiongozi wa umma ambaye alikengeuka alibainika mapema na kuzibitiwa mapema sana na Izo ITI wake ulikuwa fundisho kwa wengine. Hata kuhisiwa tuu kiongozi umefanya jambo la hovyo ilikuwa balaa. Linganisha haya na leo halafu urudi kwenye mada yako.
 
Mwalimu mwenyewe kwa busara ya hali ya juu kabisa aliuweka ujinga miongoni mwa wale maadaui wakuu watatu!
Ila kiujumla ujinga huu unaojidhihirisha kwa sasa umetengenezwa makusudi na ccm.
Siyo makusudi bali ni kwa bahati mbaya au niseme kwa kutowajibika. Tatizo la watanzania ni elimu. Pengine utauliza mbona tuna vyuo na sekondari nyingi tu na idadi ya wahitimu ni kubwa? Jibu ni elimu yetu haifanyi watu waelimike bali kukariri kwa ujanja ujanja ili wapate vyeti. Ndiyo maana siku hizi unaona watu wanashindana kuonyesha kuwa ni wasomi kwa kutumia titles kama injinia, wakili msomi, Dr, CPA nk kabla ya kuandika majina yao. Hii ni inferiotity complex inayotokana na ''wasomi'' wengi kujiona hawana uwezo wa kushindana na wasomi wengine duniani hivyo wanajaribu kujiliwaza. Kukosa elimu sahihi kunafanya watu wasione correlation kati ya maisha yao na uongozi wa kisiasa na kukata tamaa mapema.
 
Ukitazama ujinga tulionao Watanzania wengi katika karne hii utagundua kuwa Mwalimu Nyerere alipambana sana.

Hakika Baba wataifa alipata tabu sana kusugua kutu na Msasa kwenye vichwa vya Watanzania.

Imagine ujinga wakipindi chake ulikuwaje kama hivi sasa ni 2025 Watanzania karibia wote tunaujinga mkubwa namna hii, Yani kuanzia ngazi za(familia) na kila kona ni ujinga ujinga, umbea umbea tu Lord have Mercy.
Sio ujinga tu ,IQ ya mtanzania ni ndogo mno .Yaani watanzania wengi ni kama maiti zinazotembea
 
Mimi nimefanya kwenye familia yangu na kuwanunulia nyie mliolishwa propaganda kwamba huyo mnaemtukuza ndio Chanzo Cha ujinga wa Watanzania.

Mwisho Mimi Sina madaraka wenye nayo ndio wanawajibu wa kufanya.
Tafauta kazi halali ujenge nchi.

Uchawa io kazi.
 
Matumizi ya Kiswahili mashuleni. Lugha ambayo Aina ushindani kwenye soko la Ajira .


Kusaini Sheria inayomtaka mbunge kujua kusoma na kuandika Tu Kama sifa ya kuwa mbunge
Baada ya yeye kuondoka madarakani aliwazuia kubadilisha hizo sheria? Tuna miaka mingapi tangu aondoke? 🤣🤣🤣
 
NCHI YA MAKONDOO NA MANYUMBU, NDIO MANA NASEMA CCM WATATAWALA SANA LABDA WAAMUE WENYEWE, MAANA HATA HUKO JESHINI KOTE MANYUMBU TU
Issue sio chama Mkuu shida ni Watanzania. Amini nakwambia Mkuu hata kama CHADEMA au CHAUMA wakishika uongozi shida zitakuwa palepale cuz shida sio chama shida ni Watanzania Mkuu.
 
Nadhani ni vema kabla ya kujenga hoja ukajiridhisha kuwa kama una utashi na taarifa za kutosha kwaajri ya kutetea hoja yako.

Okay kwa kifupi wakati Nyerere anapewa Tanganyika kulikuwa na gepu kubwa sana la wasomi wa kutake over serikali na kushika majukumu baada ya malkia kumpa inchi. Kwa wakati ule walifosi sana watu kusoma na hata wengine kupelekwa nje ili kupata watendaji wa serikali.

So mfumo wa elimu ya wakati huo ulitengenezwa kwaajiri ya kukidhi mahitaji ya watendaji kwa wakati huo. Lakini pia mitaala ilitengenezwa kwaajiri ya raia waliopo vijijini. Kulikuwa na elimu za kilimo na ufugaji,elimu ya uraia ,ujamaa (sio ujima) na kujitegemea, na elimu za mahesabu. Mimi mzee wangu alikuwa na mavitabu kibao ya wakati huo.

So nadhani unachofanya wewe ni kutazama kufeli au mkwamo wa elimu ya sasa kwa muktadha wa elimu ya miaka hiyo,unakosea vibaya. Imeshapita miaka mingapi tokea uhuru? Nyerere alitoka lini madarakani, amefariki lini,je vikao vingapi vya bunge vimepita tokea bunge la kwanza, kwahiyo nyerere ndie anaepanga na kutaka elimu iweje au watu waliowaachia nafasi?

Hakwenda kuanzisha vita tulivamiwa na Iddi amini maeneo ya kagera (nenda kasome hostory vizuri) na video zipo iddi amini akisema kwamba Tanganyika ilichukua eneo la Uganda ni lazima walichukue kutoka Tanganyika.
Wewe unajua kwamba iddi amini alienda hadi kwa malkia Elizabeth huyu aliyefariki juzi hapa kumuomba vifaa vya kivita ili aivamie Tanganyika kunyang'anya kagera, malkia akamkatalia akaenda kwa Gaddafi ndio akampatia silaha, askari na vifaru na mapantoni ndipo iddi amini akavamia kagera, ukitaka afanyaje akae kimya? 🤔

Hivi ninyi vijana wa siku hizi mbona mnatia mashaka uwezo wenu wa kufikiria, internet ipo ,majibu yapo why mnakuwa waropokaji na watunzi wa majibu vichwani bila hata shuhuda? Video zipo iddi amini anaongea na waandishi wa habari kabisa anawaambia atavamia Tanganyika? Wewe unasema Nyerere alikwenda kuanzisha vita haya tuambie alikuwa na sababu zipi kuanIsha vita? Mnatoa wapi upuuzi huu kwenye vichwa vyenu?

Unaona sasa ulivyokuwa hauna taarifa?😂 Vita vya Tanganyika na Uganda kwa taarifa yako bajeti ilikuwa ni chini sana kwasababu hatukuwa na jeshi kubwa kihivyo na silaha zilizotumika ni zile zile za urithi kutoka kwa mjerumani na mwingereza baada ya ukoloni.

Kwa taarifa yako, sehemu kubwa ya wapiganaji walikuwa ni raia wa Tanganyika waliojitolea kusaidia jeshi baada ya kupewa mafunzo ya muda mfupi, cuba,china,kenya,msumbiji, na urusi walitoa pia sapoti kubwa. Silaha nyingi tulikwenda kuzichukua kwenye kambi za askari wa Iddi amini na kuwanyang'anya kwasababu hawakuwa vizuri kivita walikuwa walevi hawana mbinu na hawana maandalizi.

Tanganyika tulisaidiwa training na Israel kabla ya vita na wakati wa vita Israel na baadae cuba so tulikuwa vema sana kwenye guerilla style. Ukisema tulitumia pesa nitakuuliza shilingi ngapi useme.

Of course vita ilidumaza uchumi wetu ila sio kwa kiwango ambacho wewe unataka kujiaminisha maana ilikuwa ni vita ya mwaka m'moja na muda wote huo Tanzania ilikuwa inatembeza mkong'oto bila kurudi nyuma. So jipange tena na hizo hadithi za kuambiwa na wazee wanywa kahawa 😂😂

Hapa sasa umekuwa muwazi kuwa hauna shukurani na si ajabu hata wazazi wako huwa unawatamkia haya haya kuwa hajakusaidia lolote tokea wa kuzae wakusababishia umasikini ulitakiwa uzaliwe ulaya ndio ungeridhika.

Ukisema Nyerere hajafanya lolote basi haina haja ya kujadili lolote kwasababu nitakuwa naongea na mtu ambaye sio tu haijui historia ya taifa anapoishi ila hata yeye hajui yupo taifa gani ns limetokea wapi. Pole sana.
Aisee Mkuu ahsantee Sana Kwa kumuelimisha huyu kijana mpotevu.

Huwa napata hasira Sana kuona vijana wajinga wajinga kama huyu bwana mdogo wakimshushia heshima Baba wa Taifa kwa story zao za kupikwa.

Story nyingi mbayambaya kumuhusu Nyerere wengi wamesimuliwa na wazee wao wajinga wajinga nawao wanakuja kutuletea sisi.

Kiufupi vijana wengi wakitanzania hawajui story kuhusu Nchi yao bali wanajua umbea umbea kuhusu hii nchi. Yani umbea kutoka Kwa wazee wajinga walio waaminisha ujinga na chuki juu ya Baba wa Taifa hili.
 
Msamehe bure hawa ndio wale wale ambao ana maralia anaambiwa ndugu zako wanakuroga ana amini anaenda kwa wagaga wanamtandika na majani ya muarobaini anazimia wanampeleka hospitali anawekewa drip anapona anatoka anasema mganga kamsaidia sana ndugu wangemuua.

Kwa kifupi kachagua kuwa hivyo
Hakika Mkuu msamaha unahitajika watu wengi(Watanzania ) hawaelewi history ya nchi yao bali wana taarifa za kiumbea umbea kuhusu nchi hii.
 
True kabisa. Si umeona akina Polepole, Kitila mkumbo, mbowe, Kafulila, Kabudi ,na wengineo baada ya kupewa shavu wamefanya nini?

Hata kama kusema mambo wamekuta tofauti mbona wasije na kuandika waraka wa namna ilivyokuwa ngumu kusaidia serikali kutatua maisha magumu kwa wanainchi.

Wamekaa kimya wanakula pesa za kodi. Wakitoka wanaanza kelele.
Hakika Mkuu mtu akipata ulaji anaufwata akikosa anaanza kukunja ndita.

Ingawa naamini tunajifunza kupitia makosa (lakini Watanzania tunajifunza kutokana na kukosa ulaji).
 
Nyerere kama binadamu wengine alikua na mazuri na Mabaya kama binadamu uzuri aliuishi ujamaa akua Fisadi angeamua Migodi yote Tanzania angeweza kuifanya mali yake hakuna mtu angekataa au kuingia mikataba ya Kinyonyaji ovyo akachukua 10% kama Mwinyi alivyouza Roliondo na Mwinyi pia ana mazuri yake aliwatoa watu kwenye kuongea majani ya mapapai kuja kwenye sababuni
 
Tatizo siyo ujinga ni wahuni wachache walio vuna rasilimali za nchi kuogopa watafikishwa mbele y haki

Hata hivyo tunaishi kwenye jamii ya kanyanga twende jamii ambayo wengi wao hawawezi kuchakata fikra chanya na hasi yaani jamii ambayo unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe

Jamii inayo sababishiwa umasikini lakin wakati wa uchaguzi wanapewa vijizawadi, (hongwa), wakiambiwa huko kuna mikopo mbio huku wamejifunza vibwebwe mikopo kausha damu
Jamii jamii jamii ya Watanzania ni huzuni kwakweli.
 
Ni sawa na watu wanaowalaumu wakoloni wakati tupo huru kwa zaidi ya miaka 60. Nyumbu kabisa ninyi
Kasheshe Mkuu kizazi Cha lawama lawama na hakuna jitihada zinazo chukuliwa.
 
Huwezi kulinganisha principles na dedication ya watu wa kipindi hicho na watu wa sasa na hii sio Bongo tu bali dunia as a whole.... Kipindi hicho watu walikuwa sio wavivu na walichanganya na za kwao leo hii na information ya kutosha watu wamekuwa primitive na wabinafsi wanaoishi kwa leo...

1754850689106.png
 
mfano kitu gani mkuu?
1. Kutokutimiza majukumu (kulea, kufanya kazi, kujituma-uvivu, kushindwa kujisimamia n.k)

2. Miji michafu watu wanatupa taka ovyo wanataka mpaka wawekewe Sheria Kali ndiyo wafanye usafi mpaka kwenye majumba yao wenyewe.

3. Uzalendo hakuna kwenye Kila sekta.

4. Watanzania tuna matatizo/shida nyingi Sana sitaweza kuziandika zote Mkuu.
 
Matumizi ya Kiswahili mashuleni. Lugha ambayo Aina ushindani kwenye soko la Ajira .


Kusaini Sheria inayomtaka mbunge kujua kusoma na kuandika Tu Kama sifa ya kuwa mbunge
Wewe utakuwa unatabia ya ubinafsi cuz hayo yote uliyo yasema umeyatazama katika jicho la miaka ya hapa karibuni sio kipindi kile Cha Mwalimu.

Aliweka hizo Sheria Kwa kipindi kile wasomi walikuwa wachache.

Hao wakina BIBI TITI lugha ya kingereza walikuwa hawaelewi.

Pia watu wengi walikuwa hata kiswahili hawawezi wengi wanaongea lugha za makabila yao.

Je Mwalimu angeweka lugha ya kingereza na wengi ya wapigania uhuru lugha ya kingereza ilikuwa changamoto kwao unazani ingekuwaje?
 
Back
Top Bottom