Watanzania Kama KARNE hii tupo hivi nasadiki kusema Mwalimu Nyerere(Baba wa Taifa) alipambana Sana

Watanzania Kama KARNE hii tupo hivi nasadiki kusema Mwalimu Nyerere(Baba wa Taifa) alipambana Sana

Nyerere kama binadamu wengine alikua na mazuri na Mabaya kama binadamu uzuri aliuishi ujamaa akua Fisadi angeamua Migodi yote Tanzania angeweza kuifanya mali yake hakuna mtu angekataa au kuingia mikataba ya Kinyonyaji ovyo akachukua 10% kama Mwinyi alivyouza Roliondo na Mwinyi pia ana mazuri yake aliwatoa watu kwenye kuongea majani ya mapapai kuja kwenye sababuni
Katika historia Mwalimu Nyerere ni moja ya viongozi bora kabisa Afrika na Duniani Kwa ujumla wanao Pinga hawana hoja ni wambea wambea tu wapuuzwe.
 
Katika historia Mwalimu Nyerere ni moja ya viongozi bora kabisa Afrika na Duniani Kwa ujumla wanao Pinga hawana hoja ni wambea wambea tu wapuuzwe.
Nyerere ni mtu na Nusu sema kwenye katiba alituachia bomu ambalo kulitegua Imekua changamoto
 
Ndugu mleta mada nadhani ungetofautisha uzalendo na ujinga. Wananchi wa zama za J. K. Nyerere kweli wengi walikuwa wajinga kielimu ila walikuwa wazalendo na wafianchi kwelikweli kuanzia ngazi ya kaya mpaka taifa na kiwango cha ubinafsi kwa viongozi wa umma kilikuwa chini mnoo. Kiongozi wa umma kweli alimaanisha na aliheshimika hivyo na alikuwa kioo cha jamii kwelikweli. Kiongozi wa umma ambaye alikengeuka alibainika mapema na kuzibitiwa mapema sana na Izo ITI wake ulikuwa fundisho kwa wengine. Hata kuhisiwa tuu kiongozi umefanya jambo la hovyo ilikuwa balaa. Linganisha haya na leo halafu urudi kwenye mada yako.
Kutokuwa mzalendo niujinga pia Mkuu.

Wewe kama sio mzalendo wa nchi yako tunakuitaje Mkuu ?

Zamani tulikuwa tunapata tabu kuwaelimisha wajinga lakini Leo hii tunapata tabu kuwaelimisha wasomi.
 
Siyo makusudi bali ni kwa bahati mbaya au niseme kwa kutowajibika. Tatizo la watanzania ni elimu. Pengine utauliza mbona tuna vyuo na sekondari nyingi tu na idadi ya wahitimu ni kubwa? Jibu ni elimu yetu haifanyi watu waelimike bali kukariri kwa ujanja ujanja ili wapate vyeti. Ndiyo maana siku hizi unaona watu wanashindana kuonyesha kuwa ni wasomi kwa kutumia titles kama injinia, wakili msomi, Dr, CPA nk kabla ya kuandika majina yao. Hii ni inferiotity complex inayotokana na ''wasomi'' wengi kujiona hawana uwezo wa kushindana na wasomi wengine duniani hivyo wanajaribu kujiliwaza. Kukosa elimu sahihi kunafanya watu wasione correlation kati ya maisha yao na uongozi wa kisiasa na kukata tamaa mapema.
Good.
 
Wewe utakuwa unatabia ya ubinafsi cuz hayo yote uliyo yasema umeyatazama katika jicho la miaka ya hapa karibuni sio kipindi kile Cha Mwalimu.

Aliweka hizo Sheria Kwa kipindi kile wasomi walikuwa wachache.

Hao wakina BIBI TITI lugha ya kingereza walikuwa hawaelewi.

Pia watu wengi walikuwa hata kiswahili hawawezi wengi wanaongea lugha za makabila yao.

Je Mwalimu angeweka lugha ya kingereza na wengi ya wapigania uhuru lugha ya kingereza ilikuwa changamoto kwao unazani ingekuwaje?
Ingekuwa poa Sana sababu angekuwa amewekeza kwenye future now days tungekuwa mbali Sana kwenye soko la Ajira ngambo . SASA ona how primitive we are kwamba ata waziri Tu kimombo NI shida
 
Kwa Africa sidhani kama kuna Taifa Lina Manyumbu zaidi ya Tanzania
Kuwaita watanzania wajinga ni kuwapa hadhi.

Mjinga ni mtu asiyejua kitu fulani. ila akifahamishwa kuhusu kitu hicho, anaelewa na ujinga wake unamtoka.

Wabongo sio wajinga tu, bali ni wapumbavu wa milele.
 
Kuwaita watanzania wajinga ni kuwapa hadhi.

Mjinga ni mtu asiyejua kitu fulani. ila akifahamishwa kuhusu kitu hicho, anaelewa na ujinga wake unamtoka.

Wabongo sio wajinga tu, bali ni wapumbavu wa milele.
Maiti kabisaaa
 
Ukitaka kujua watanzania ni machenjeu Kuna watu wanaona pole pole hafai na anamuonea ssh!!!hakika taifa Lina laana
... kwaweli Kuna watu wajinga sana Tanzania! ... kama mpaka kuna watu wanamuona Polepole 'genius' basi tukubali tu WaTZ ni vilaza!
kU
 
Ukitazama ujinga tulionao Watanzania wengi katika karne hii utagundua kuwa Mwalimu Nyerere alipambana sana.

Hakika Baba wataifa alipata tabu sana kusugua kutu na Msasa kwenye vichwa vya Watanzania.

Imagine ujinga wakipindi chake ulikuwaje kama hivi sasa ni 2025 Watanzania karibia wote tunaujinga mkubwa namna hii, Yani kuanzia ngazi za(familia) na kila kona ni ujinga ujinga, umbea umbea tu Lord have Mercy.
Tatizo unataka watu wengine wafanye mambo unayoyataka. Amua kuwa sehemu ya mabadiliko unayoyataka ili uache kulalamika na kujitukana.
 
Ujinga mwingi ulitengenezwa na hao hao kina Nyerere
kweli kabisa kwani yeye ndiye wa kwanza kukataa vyama vingi na kuleta udikteta wa chama kimoja, failed theories of villagisation, nationalisation and party supremacy. Na hata kipindi cha watu kuanza kuamka alikuwa akisema TV na friji ni luxuries ambazo watanzania hawahitaji (lakini yeye alikuwa na satellite dishes mbili kwake ikulu)
 
Aisee Mkuu ahsantee Sana Kwa kumuelimisha huyu kijana mpotevu.

Huwa napata hasira Sana kuona vijana wajinga wajinga kama huyu bwana mdogo wakimshushia heshima Baba wa Taifa kwa story zao za kupikwa.

Story nyingi mbayambaya kumuhusu Nyerere wengi wamesimuliwa na wazee wao wajinga wajinga nawao wanakuja kutuletea sisi.

Kiufupi vijana wengi wakitanzania hawajui story kuhusu Nchi yao bali wanajua umbea umbea kuhusu hii nchi. Yani umbea kutoka Kwa wazee wajinga walio waaminisha ujinga na chuki juu ya Baba wa Taifa hili.
Nawewe hata kuna mambo mengi huyajui kupitia hii comment
Nyerere lazima alaumiwe kwa sababy mpaka leo tunatumia katiba yake na mfumo mzima wa uongozi ni yeye ndo aliyeuasisi kwa lazima alaumiwe
 
Ingekuwa poa Sana sababu angekuwa amewekeza kwenye future now days tungekuwa mbali Sana kwenye soko la Ajira ngambo . SASA ona how primitive we are kwamba ata waziri Tu kimombo NI shida
Ni kweli kingereza nishida nchini lakini isiwe reason ya kumdisrespect Baba wa Taifa hili.

Alifanya yanayo mpasa kufanya kama kiongozi Kwa nyakati zile/zake.

Na sisi tuendelee kujenga panapo hitajika lakini kwakuwa Watanzania wengi ni wajinga tunabaki kumpa lawama merehemu Kwa kuwa na sisi ni marehemu tunaoishi bado.
 
Tatizo unataka watu wengine wafanye mambo unayoyataka. Amua kuwa sehemu ya mabadiliko unayoyataka ili uache kulalamika na kujitukana.
Tatizo umesoma thread hii kisiasa zaidi(upendeleo) ndiyo maana umekuja na hoja hii.

Nitakupa mfano ninapo sema ujinga ni Kwa upana sana MFANO hivi sasa Watanzania wengi wamekuwa wachafu sana hawasafishi mazingira wanatupa taka hovyo hovyo, wanasubiri mpaka Mh Rais au kiongozi mkali ndio wafanye hata kusafisha majumba yao wenyewe.

Watanzania sio wazalendo, hawajitumi uvivu, umbea umbea n.k huo ni ujinga.
 
Back
Top Bottom