Watanzania Kama KARNE hii tupo hivi nasadiki kusema Mwalimu Nyerere(Baba wa Taifa) alipambana Sana

Watanzania Kama KARNE hii tupo hivi nasadiki kusema Mwalimu Nyerere(Baba wa Taifa) alipambana Sana

Wewe umefanya nini cha maana chenye impact kwa jamii yako? ACHA UJINGA!
Msamehe bure hawa ndio wale wale ambao ana maralia anaambiwa ndugu zako wanakuroga ana amini anaenda kwa wagaga wanamtandika na majani ya muarobaini anazimia wanampeleka hospitali anawekewa drip anapona anatoka anasema mganga kamsaidia sana ndugu wangemuua.

Kwa kifupi kachagua kuwa hivyo
 
Mimi nimefanya kwenye familia yangu na kuwanunulia nyie mliolishwa propaganda kwamba huyo mnaemtukuza ndio Chanzo Cha ujinga wa Watanzania.

Mwisho Mimi Sina madaraka wenye nayo ndio wanawajibu wa kufanya.
Mkuu kwahiyo Kwa kufanya hayo uliyo yaandika ndiyo unajiona unaakili kumzidi Baba wa Taifa?

Kiasi kwamba kumsema kwamba hakuwa lolote wala chochote kwenye hili Taifa?
 
Aise ni huzuni Mkuu me nazani shida ni Watanzania sio chama. cuz CCM ni chama tu ambacho ndani yake Kuna Watanzania.

Hivyo basi hata kama CHADEMA au CHAUMA ikishika uongozi shida itakuwa palepale cuz shida sio chama shida ni Watanzania Mkuu.
True kabisa. Si umeona akina Polepole, Kitila mkumbo, mbowe, Kafulila, Kabudi ,na wengineo baada ya kupewa shavu wamefanya nini?

Hata kama kusema mambo wamekuta tofauti mbona wasije na kuandika waraka wa namna ilivyokuwa ngumu kusaidia serikali kutatua maisha magumu kwa wanainchi.

Wamekaa kimya wanakula pesa za kodi. Wakitoka wanaanza kelele.
 
Ndio maana Nyerere alikuwa anawatukana sometimes na kuwaambia baadhi ya Wanasiasa wana tabia za Kimalaya malaya, yaani kama malaya anavyonunulika kwa beer tu🤣🤣🤣🤣
😄 Noma Sana Mkuu ndiyo maana mimi huwa nasema humu Kila siku. Tanzania shida sio chama shida ni Watanzania hata kama Leo CHADEMA au CHAUMA wakishika uongozi shida zitakuwa palepale cuz shida sio chama shida ni Watanzania Mkuu.
 
Ukitazama ujinga tulionao Watanzania wengi katika karne hii utagundua kuwa Mwalimu Nyerere alipambana sana.

Hakika Baba wataifa alipata tabu sana kusugua kutu na Msasa kwenye vichwa vya Watanzania.

Imagine ujinga wakipindi chake ulikuwaje kama hivi sasa ni 2025 Watanzania karibia wote tunaujinga mkubwa namna hii, Yani kuanzia ngazi za(familia) na kila kona ni ujinga ujinga, umbea umbea tu Lord have Mercy.
Tatizo siyo ujinga ni wahuni wachache walio vuna rasilimali za nchi kuogopa watafikishwa mbele y haki

Hata hivyo tunaishi kwenye jamii ya kanyanga twende jamii ambayo wengi wao hawawezi kuchakata fikra chanya na hasi yaani jamii ambayo unaweza kuisafisha ubongo ikafikiri unavyotaka wewe

Jamii inayo sababishiwa umasikini lakin wakati wa uchaguzi wanapewa vijizawadi, (hongwa), wakiambiwa huko kuna mikopo mbio huku wamejifunza vibwebwe mikopo kausha damu
 
Walikuwa wajinga sana enzi hizo. Na Nyerere aliutumia ujinga huo kuwaaminisha kuwa yeye ana akili kubwa kwa kuwahutubia mambo aliyokuwa akiyaona kwenye TV ama kuyasoma kwenye vitabu.
Hizi ndo story tulizo nazo Watanzania ni huzuni kwakweli.

Hakika Nyerere alipata tabu sana kama mpaka wewe wa Karne hii unaongea vitu Kama hivi.
 
mkuu nchi hii ukihoji unapigwa nakuumizwa.kwahio watu wamenyamaza unawaona wajinga.

hio simba na yanga ingekuwa nayo ukiongea unapigwa watu wange ufyata
Issue sio kuongea Mkuu, tunashida nyingi sana Watanzania achana hata na siasa.

Mambo mengi yanatushinda angalia hata kwenye ngazi za Familia vitu vidogo vya kusolve watu hawezi zaidi zaidi wanaongeza matatizo.
 
Bora simba na yanga ,mtu anaandika uzi wa kumsifia mwanamke wa fulani ...Nyuzi za kishamba mpaka unajiuliza hawa vijana watakua lin.
Ni huzuni Mkuu ingia mitandao yote Mada ni za ngono ngono tu hakuna challenge za maana shida sana.
 
Hebu tuambie aliutengenezaje ujinga kwa mfano?
Matumizi ya Kiswahili mashuleni. Lugha ambayo Aina ushindani kwenye soko la Ajira .


Kusaini Sheria inayomtaka mbunge kujua kusoma na kuandika Tu Kama sifa ya kuwa mbunge
 
Back
Top Bottom