Watanzania lazima Tufahamu Rais wa nchi siyo Sawa na Rais Wa Bendi ya Mziki kiulinzi na Kiusalama

Hicho kiti mbona hakwenda nacho UK?
 
Kabisa hasa suala Hilo la ulinzi na usalama wa mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani tuviachie vyombo vyetu vinavyohusika na ulinzi wa Rais

Kwahiyo hapa Tanzania ambapo mnasema aliingia madarakani kwa kura halali ndio usalama wake mdogo, ila kule UK alikopakizwa bus usalama wake ndio mkubwa?
 
Kijana pamoja uchawa wako wote huo katika awamu hii, pengine mbali na kunufaika na hizo buku 7 unazozipata, zidi kujipendekeza hata uambulie nafasi ya katibu mtendaji kata,
 
Hicho kiti mbona hakwenda nacho UK?
Tindo ndugu yangu embu acha kuniabisha kwa maswali yasiyoendana na uwezo wako wa kufikiri, Mimi nafahamu uwezo wako Ni zaidi ya hapa na huwezi ukauliza swali la namna hii
 
Kijana pamoja uchawa wako wote huo katika awamu hii, pengine mbali na kunufaika na hizo buku 7 unazozipata, zidi kujipendekeza hata uambulie nafasi ya katibu mtendaji kata,
Siandiki hapa kwa malipo ya aina yoyote Ileeeee , naandika kwa utashi wangu binafsi na msukumo unaotokana na kuridhishwa na utendaji kazi wa kutukuka wa mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani , Nami nahangaika natafuta vocha Kama wewe nakuingia humu kuchangia mawazo na mtizamo wangu, Kama wewe unalipwa Ni wewe binafsi usifikiri wote tunaingia humu kwa malipo
 
Kwahiyo hapa Tanzania ambapo mnasema aliingia madarakani kwa kura halali ndio usalama wake mdogo, ila kule UK alikopakizwa bus usalama wake ndio mkubwa?
Kwani John F Kennedy hakuingia madarakani kwa kura halali? Abraham linkolin hakuingia kwa kura? Mambo ya usalama tuviachie vyombo vyetu vifanye kazi yake bila kuingiliwa na mtu yoyote yule
 
Rais asichukuliwe kama mungumtu. Anatakiwa awapende raia wake na kuongoza utatuzi wa matatizo yao. Akiwa rais ni binadamu wa kawaida kwenye hali ya kawaida. Atavaa mamlaka yake pale inapohitajka mfano kiutangaza vita, kutoa amri fulani, kuteua nk. Wananchi humpenda raisi anayewapenda na kuwatumikia na sie anayewatawala na kuwapa amri kisa ni raisi tu.
 
Rais siyo Mungu mtu lakini usalama na ulinzi wa Rais hauwezi ukawa sawa na Mimi au wewe, hiyo haiwezekani hata kidogo na haiji kuwezekana popote pale Dunianiii, Usalama na ulinzi wa Rais wetu mpendwa lazima ndio kiwe kipaombele Cha idara zetu za ulinzi na usalama popote pale anapokuwepo au atakapokuwepo Rais wetu,
 
Tindo ndugu yangu embu acha kuniabisha kwa maswali yasiyoendana na uwezo wako wa kufikiri, Mimi nafahamu uwezo wako Ni zaidi ya hapa na huwezi ukauliza swali la namna hii

Hamna kitu, kutaka umaarufu wa kijinga. Mnaingia madarakani kwa wizi wa kura, kisha mnapeleka utukufu usio na tija kwenye nyumba za ibada!
 
Kwani John F Kennedy hakuingia madarakani kwa kura halali? Abraham linkolin hakuingia kwa kura? Mambo ya usalama tuviachie vyombo vyetu vifanye kazi yake bila kuingiliwa na mtu yoyote yule

Kwahiyo akiingia kanisani na kiti chake ndio hayawezi kumkuta ya akina Kennedy? Acheni kutaka sifa za kijinga. Kwahiyo huko msikitini ataingia na jamvi lake? Utukufu wa kijinga kabisa.
 
Hamna kitu, kutaka umaarufu wa kijinga. Mnaingia madarakani kwa wizi wa kura, kisha mnapeleka utukufu usio na tija kwenye nyumba za ibada!
Serikali ya CCM ipo madarakani kihalali kabisaa Ndio maana hata Lisu aliposema muandamane kupinga matokeo wote wafuasi wake mlimgomea kuandamana maana mlijuwa matokeo Ni halali kabisaa na kwamba hakuwa na Sera Wala ajenda ambazo zingemfanya Apewe kura na watanzania.
 
Watu hawakuandamana kutokana na woga wa kuuwawa, sio kwa uhalali wa matokeo. Endeleeni kuomba uoga uendelee kuwa wa kiwango hiki hiki, siku woga ukiisha ndio itakuwa mwisho wa CCM kukaa madarakani kwa shuruti.
 
Kwahiyo akiingia kanisani na kiti chake ndio hayawezi kumkuta ya akina Kennedy? Acheni kutaka sifa za kijinga. Kwahiyo huko msikitini ataingia na jamvi lake? Utukufu wa kijinga kabisa.
Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ndio vinajuwa uratibu wa suala Hilo la ulinzi wa Rais wetu mpendwa, kwa hiyo usianze habari za kusema huku itakuwaje au kule atabeba Nini, ndio maana Nilishasema nyie chadema Ni watu wakudandia matukio yasiyo hata wapa kitu, mkitoka hapa mnapoteana Tena maana hamnaga ajenda za kudumu,
 
Watu hawakuandamana kutokana na woga wa kuuwawa, sio kwa uhalali wa matokeo. Endeleeni kuomba uoga uendelee kuwa wa kiwango hiki hiki, siku woga ukiisha ndio itakuwa mwisho wa CCM kukaa madarakani kwa shuruti.
Sasa na wewe usiye muoga mbona hukuandamana? Halafu acheni kuwatukana watanzania kwa kusema Ni waoga baada ya kuwa wamewapuuza kutokana na kukosa kwenu muelekeo na dira ya kueleweka
 
Mnafanya matukio ya kijinga kisha mnashangaa watu kuyakosoa?!
 
Sasa na wewe usiye muoga mbona hukuandamana? Halafu acheni kuwatukana watanzania kwa kusema Ni waoga baada ya kuwa wamewapuuza kutokana na kukosa kwenu muelekeo na dira ya kueleweka

Nasema hivi, hakuna watu waoga kama watanzania, lakini uoga huu utaisha tu maana tayari wameshajitambua. Sasa hivi watu wamelipuuza box la kura maana wamejua linachezewa. Iko siku mtakuta hawa waoga wako barabarani hamtaamini.
 
Hakuna tukio la kijinga Ila nyie ndio mmefanya watu wawashangae na kuwaona wababaishaji kwa kushupalia kitu Cha kawaida katika masuala ya ulinzi na usalama wa Rais wa nchi,Hii yote ni kutokana na kuwa mlishaishiwa Sera za kuwaweka masikioni na mioyoni mwao watanzania ndio maana mnajaribu kujirusha kila eneo
Mnafanya matukio ya kijinga kisha mnashangaa watu kuyakosoa?!
 
Anza wewe kwanza usiye muoga ili wengine wafuatw nyuma yako,
Nasema hivi, hakuna watu waoga kama watanzania, lakini uoga huu utaisha tu maana tayari wameshajitambua. Sasa hivi watu wamelipuuza box la kura maana wamejua linachezewa. Iko siku mtakuta hawa waoga wako barabarani hamtaamini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…