Watanzania lazima Tufahamu Rais wa nchi siyo Sawa na Rais Wa Bendi ya Mziki kiulinzi na Kiusalama

Watanzania lazima Tufahamu Rais wa nchi siyo Sawa na Rais Wa Bendi ya Mziki kiulinzi na Kiusalama

Hakuna tukio la kijinga Ila nyie ndio mmefanya watu wawashangae na kuwaona wababaishaji kwa kushupalia kitu Cha kawaida katika masuala ya ulinzi na usalama wa Rais wa nchi,Hii yote ni kutokana na kuwa mlishaishiwa Sera za kuwaweka masikioni na mioyoni mwao watanzania ndio maana mnajaribu kujirusha kila eneo

Wenye sera msingeendekeza siasa za utukufu wa bei rahisi kwenye nyumba za watu za ibada.
 
Wenye sera msingeendekeza siasa za utukufu wa bei rahisi kwenye nyumba za watu za ibada.
Tunakubalika ndio sababu ya kupewa heshima kila sehemu, Tofauti na nyie mlioshindwa kujenga hata ofisi ya makao makuu licha ya mamilioni mliyokuwa mnapokea Kama Ruzuku lakini mmeishia kuzitafuna na kunywea pombe
 
Heshima ya kushurutisha haijawahi kuwa heshima bali dhihaka.
 
Kaidai ww maana ulishuhudia Sabodo akitoa hiyo hela.
Kwani wewe ulikuwa wapi wakati huo Sabodo akitoa? Basi umechelewa Sana kufika hapo ufipa na kumbe huelewi kwanini makamanda walishamkimbia Mbowe hapo, walishashituka mchezo wake wakuzitafuna Ruzuku na michango yote ya wanachama na wafadhili bila huruma huku vijana mkipigwa jua tu
 
Watanzania wameridhishwa na kuridhishwa na CCM ndio maana unaona nchi ikiwa imetulia vyema

Hata akina Mugabe walipokuwa wanatawala kwa shuruti huku wananchi wakiwa waoga, wapambe wake kama wewe walisema nchi imetulia. Yaani kwao uoga huku wakinajisi chaguzi waliita ni nchi kutulia. Siku watu waliingia mtaani hawakuamini.
 
Usifananishe nchi yetu chini ya serikali ya CCM na mambo yasiyoendana, wewe huoni kila mtu anakuja kujifunza hapa Tanzania, Anzeni kumpumzisha Mwenyekiti wenu ambaye muda wote yupo madarakani
 
Usifananishe nchi yetu chini ya serikali ya CCM na mambo yasiyoendana, wewe huoni kila mtu anakuja kujifunza hapa Tanzania, Anzeni kumpumzisha Mwenyekiti wenu ambaye muda wote yupo madarakani

Nani anakuja kujifunza Tanzania boss, labda waliopoteza ramani. Lakini hakuna mtu au nchi inayojitambua inaweza kuja kujifunza Tanzania. Sana sana watakuja kuangalia asili ya huu ujinga na uoga imetokana na nini.
 
CCM Ni Tanuri la kupika viongozi wa leo na kesho, Ndio maana unaona hata nchi jirani zinatuheshimu
 
CCM Ni Tanuri la kupika viongozi wa leo na kesho, Ndio maana unaona hata nchi jirani zinatuheshimu

Tanuri la kupika wanafiki, waongo, wazandiki nk. Narudia tena watu wanaoweza kuja kujifunza hapa labda watoke Burundi maana hao ndio waliochoka kuliko sisi.
 
Ndugu zangu Kuna watu wanaleta ujuaji Sana hapa nchini, Kuna watu wanafikiri kila kitu ni siasa, Kuna watu wanafikiri kila kitu ni sawa na wanavyowaza, kuna watu wanamchukulia Rais Kama raia wa kawaida, kuna watu kwa upeo wao mdogo wanamlinganisha Rais na sisi, Kuna watu wanazani uzito wa Rais Ni Sawa na uzito wa Mwenyekiti wa chama kilicho kama Saccos.

Lazima Tufahamu kuwa Rais wa nchi Ni mkuu wa nchi na kiongozi wa Serikali, Ni Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, Akishakupigiwa kura na kuapishwa hawi Kama yule uliyekuwa unamfahamu, hajiamulii mambo Kama alivyookuwa anajiamulia kiusalama, Haendi kila sehemu aliyokuwa anaenda awali, hapiti kila eneo alikokuwa anapita awali, Hali chakula kila mgahawa alikokuwa anakula awali, hasalimiani na kila mtu Wala hasogeleani na kila mtu hata Kama alipanga msitari kumpigia kura katika uchaguzi, Wala hapandi kila gari na kupita popote pale na njia yoyote ile.

Lazima Tufahamu kuwa kila kitu kinawekwa katika utaratibu maalumu, utaratibu wa kijasusi,utaratibu wa kiusalama na kiulinzi, lazima Tufahamu kuwa usalama na ulinzi wa Rais wa nchi Ndio Jambo la muhimu kuliko kitu kingine chochote kile hapa nchini, amani na utulivu wa nchi hauwezi ukatenganishwa na usalama wa Rais na familia yake.

Rais hawezi akayumba kiafya halafu utegemee nchi isiyumbe, lazima iyumbe, itetemeke, ipepesuke, mambo lazima yatetereke na kusua sua, lazima idara zisimame kazi zake, lazima watu watege masikio juu ya Hali ya Rais, lazima mawazo ya watu yawe mahali pamoja tu, lazima kila muda iulizwe Hali ya Rais ikoje, lazima ufanisi wa kazi upungue makazini kwote na kila idara, mpaka Rais atakapo toka hadharani kulipungia mkono na kulisalimu Taifa ama kulihutubia Taifa letu ndipo mioyo ya watu itapona na kupata amani na Kuendelea na kazi kwa moyo wote.

Hivyo tusiwafundishe Wala kuwaingilia katika kazi watu waliopewa dhamani juu ya ulinzi na usalama wa Rais wetu, Tusiwachanganye Wala tusiwaone Ni wajinga, Mwenyezi Mungu alitupatia maarifa wanadamu hivyo lazima maarifa yote yatumike katika kuhakikisha Rais anakuwa salama muda wote, hiyo ni kazi yao. Ni wajibu wao wakufa na kupona kuhakikisha Rais Ni salama. Tusilete uanaharakati kwa kila Jambo.

Macho yetu lazima tujuwe Ni vipofu linapokuja suala la ulinzi na usalama wa Rais, sisi tunaona kwa macho haya ya nyama pekee, macho ya kukosoa, ambayo yanafumba hata upepo ukipita, macho yetu siyo Kama ya wale tuliyowapa dhamani ya ulinzi wa Rais wetu mpendwa, wao wanaona mbali, wanao hata tusivyoweza kuona kwa macho ya kawaida, wanaona hata kabla ya kukaa, wanaona hata mioyo yetu, wanaona hata ishara zetu, wanaona hata mifuko yetu, wanaona hata katikati yetu. Wakati sisi hata tukizibwa na mtu mrefu mbele yetu hatuwezi kusimulia kilichokuwa mbele yetu hatua chache.

Tuache ujuaji na kukosoa kila kitu, tuache uanaharakati kwa kila kitu, tuache utalaamu kwa vitu ambavyo hata darasni hatujawahi kukaa kujifunza, tuache umbilikimo wa kifikira na kimawazo, tuache werevu wakati ni vipofu wa masuala ya usalama, Tuache idara zetu za usalama zifanye kazi zake, zitekeleze wajibu wake.

Idara yetu ya ulinzi na usalama wa Rais Rai yangu kwenu ni kuwa endeleeni na majukumu yenu Wala msiyumbishwe Wala kuondolewa katika mstari wenu ,Wala kufundishwa kazi, Wala kuelekezwa na mtu wa nje kipofu wa masuala ya ulinzi na usalama, tunachohitaji Ni kuona Rais wetu ni salama kwa gharama zozote zile, tunampenda Rais wetu na tumewakabidhini ulinzi na usalama wake muutekeleze ipasavyo na kwa weledi mkubwa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu mtoa njia maarifa.

Kazi iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Ukishangaa ya Musa.....
 
Tanuri la kupika wanafiki, waongo, wazandiki nk. Narudia tena watu wanaoweza kuja kujifunza hapa labda watoke Burundi maana hao ndio waliochoka kuliko sisi.
Nilikuuliza hivi Ile michango ya join the chain IPO wapi? Mmetafuna nazo? Mbona hamna huruma nyie? Watu wanaomba mrejesho, mbona kimya? Au ndio zimetafunwa kama zile za Ruzuku?
 
Back
Top Bottom