Watanzania mnaojiua kila siku nani aliyewaambieni kuwa sisi wengine hatukupitia changamoto kubwa za kimaisha kuwazidi?

Huyo Daktari wa Afya ya Akili unayeenda kumuona bila ya Mwenyezi Mungu Kumbariki Kitaaluma angeweza Kukutibu?
 
Uko sahihi
 
Pole Sana Mdogo wangu kwa kua na Mawazo hayo.
 
Nakupongeza kwa huu Uzi adhimu Chief

Mungu ni muweza wa yote. Yeye ndie alfa na umega. MUNGU akubariki na rehma zake ziwe juu yako.
Amen / Amina Mkuu. Kuna Watu wanadhani wakichukiwa au wasiposaidiwa na wachache basi na wengine wa kuwasaidia na kuwapenda hawapo tena duniani. Mwenyezi Mungu kaumba Wanadamu wa aina mbili wale wa Kukumaliza na wale wa Kukuokoa na Kukuinua sasa inategemea tu Wewe uko wapi na unajichanganya nao vipi.
 
Usilaumu kuna watu wamelelewa na roho nzuri wakitegema watu wawapende kama wanavyowapenda wao. Wanaodumu katika hii dunia ni watu ambao wapo cynical(nipe nikupe) unaweka upendo na hisia pembeni. Unamtreat mtu kutokana na mchango wake katika maisha yako na sio upendo. Lakini ukiweka hisia na upendo binadamu watakukatisha tamaa. Wanaojimaliza na kujiua wengi wanakuwa wanajitoa kuliko uwezo wao. Wakiamini kujitoa kwao ndio kutafanya wathaminike zaidi.
 
Matatizo ni sehemu ya mwanadamu
Kwa hiyo hadi wanaosumbuliwa na magonjwa wana-afya ya akili sikutegemea una mawazo mfu hivi
Soma vizuri tena , matatizo yakirundikana bila kuwa na suluhu ndio huzalisha msongo mkubwa wa mawazo na kudhorotesha afya ya akili.
 
Soma vizuri tena , matatizo yakirundikana bila kuwa na suluhu ndio huzalisha msongo mkubwa wa mawazo na kudhorotesha afya ya akili.
Sio kila changamoto au maumivu sababu ni matatizo ya akili kama unavyotaka kuaminisha watu

Hakuna mtu anayependa kurundika matatizo inatokea tu anajaribu kuyaondoa ila anashindwa
mfano mtu aliyefeli figo huwezi mlaumu kwa hilo tatizo lipo nje ya uwezo wake
 
matatizo mengine Ni ya kiroho lakini sisi tunayalazimisha yawe ni ya Katika macho ya nyama. Hivi unajua kusema uwongo kupindukia unajisababishia tatizo rohoni mwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…