Watanzania mtakapoona kila nyumba kuna msiba ndipo mtatubu kusifia kila neno

Watanzania mtakapoona kila nyumba kuna msiba ndipo mtatubu kusifia kila neno

Nchi itabaki na vijana kwa hali hii inauma ila hamna namna, msiba usikie kwa jirani sio kwako, sii poa

Tanganyika tusipo kuwa makini Corona itahamia kwetu milele, na kuna ugonjwa mpya wa kushindwa kupumua sijui ndo upi
 
Tulipokuwa tunawaambia haya maneno tangu mwanzoni mwa 2016 (actually kuna watu walianza kutuonya wiki ya kwanza tu ya utawala wake bwana jiwe) mlitutukana kila aina ya matusi. Mlidhani athari zake zitakuwa kwa kina Mbowe na wenzake pekee?
Na bado, unachokiona sasa ni cha mtoto. Subiri kubwa lake.
[/QUOTE]Utakuwa umetumwa wewe na mabeberu kuja kuyaongea hayo
 
Ww ndio ulikuwa msifiaji wa kila kitu, saa hii ulichokuwa unasifia kimeanza kutoa matunda kisha unakimbia mavuno!

Usishangae tumefikaje hapa wakati ww mwenyewe ulishiriki kuua nguvu ya kuhoji ndani ya hii nchi.
Naomba kuweka kumbukumbu vizur. Nilisema kwenye moja ya uzi wangu Covid 19 imetukuta wakati mbaya sana nakuwahusia Watanzania wasali naku support serikali kutofunga shughuli.

Hakuna mahali au bandiko napigia debe serikali isitoe taarifa za wagonjwa wa Covid 19. Mm najielewa nasiwezi kutoa ushauri au support jambo lahatari kama hili. Kuwanyima watu taarifa ya watu wanao uguwa na kufa kwa ugonjwa kamahuu nikuwauwa maelfu ya watu kwa kukusudia au kutokukusudia.
 
Tusidanganyane Covid 19 inamaliza watu silence na kwakuwa serikali yetu imeamua kufanya siri na kuficha kila kitu basi ndugu zangu vifo vitatuumbua nataka kuwaambia dunia itakuja kuangalia nini kimetokea Tanzania.

Watu watakufa na watashindwa kuzika mbaya zaid watakao jifanya wanaume kuzika nawao watazikwa.

Kwakuwa mambo yanaenda kwa siri huduma za afya zitakuwa mbaya why? Hakuna anaye taka kufa na kwakuwa serikal imeficha taarifa basi tumekwisha.

Nani jasiri atamwambia Rais ukweli kauli yake inaliangamiza taifa silence na mwisho hata yeye hatokuwa salama na serikali yake? Nina alie mshauri ? Na nikwamasilahi gani?

Tuliza boli kiongozi. Kama noma ishakuwa noma. Israel leo amesambaratisha sio mchezo. Ila tuzidi kuombeana. Tuzidi kuchukua tahadhari. Na tuzidi kuomba kesho njema maana kama maji tushayavulia nguo na kuanza kuyaoga
 
Siyo sheria lakini raia walizoeshwa kupata taarifa walau ndani ya wiki mara moja.
Inapotokea hakuna taarifa yoyote watu wanaanza kubuni taarifa zao kutokana na wanayosikia na kuona.

Hata hivyo, ukweli una tabia ya kupenda kujidhihirisha kwa kishindo. Muda ndio muamuzi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusidanganyane Covid 19 inamaliza watu silence na kwakuwa serikali yetu imeamua kufanya siri na kuficha kila kitu basi ndugu zangu vifo vitatuumbua nataka kuwaambia dunia itakuja kuangalia nini kimetokea Tanzania.

Watu watakufa na watashindwa kuzika mbaya zaid watakao jifanya wanaume kuzika nawao watazikwa.

Kwakuwa mambo yanaenda kwa siri huduma za afya zitakuwa mbaya why? Hakuna anaye taka kufa na kwakuwa serikal imeficha taarifa basi tumekwisha.

Nani jasiri atamwambia Rais ukweli kauli yake inaliangamiza taifa silence na mwisho hata yeye hatokuwa salama na serikali yake? Nina alie mshauri ? Na nikwamasilahi gani?
Mimi nitaamini nikiona hapo kwenu wameondoka na corona kama watano hivi. Mhudumu ongeza bia!
 
Corona ni kama mimba huwezi kuficha.Watazaa tuuu licha ya kukimbilia chattle!
 
Narudia tena ukiumwa serious Tafuta daktari wako private akusaidie mahospital Dar es Salaam yamejaaa mpaka basi na kuna folen kuliko maelezo, inawezakuwa kinachowaua watu wengi sio ugonjwa wa corona ila corona ndio imesababisha hii jam.

Na observation nlofanya ni kwamba ndugu zetu wa mikoan tukiwaambia bado hawaelew na hawaamini yan wanadhan kama ni ugonjwa wa instagram aisee nasikitika sana yan ugonjwa umetoka wuhan utashindwa kufika namtumbo ? aisee mungu atusaidie


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mfumo wa uendeshaji wa nchi hii si mzuri.
Unaachaje maisha ya watanzania mil 56 mikononi mwa mtu mmoja??
Kwamba yeye ndiye anayeamua kila kitu, kuhusu tiba, elimu, kazi, fedha, ulinzi nk??

Sisi sote ni binadamu, tunaweza kuugua ama kufa.

Mfano huyu mtu akawa ameugua ugonjwa wa akili bado tunaendelea kutii na kufuata matakwa yake tu??

Ikitokea hivyo, na dalili zinaonesha hivyo basi Watanzania tumekwisha.

Wote huko kwenye mihimili ya sheria, bungeni, na vyombo vya ulinzi na usalama hakuna wenye nazo wakaamua kwa ajili ya ndugu zao watanzania mil.56 wanaokufa bila huruma na gonjwa hili baya la corona????

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah! Umeandika kwa masikitilp kweli!
Nasikiasikia watu wa mitandaoni wanasakwa.
Naamini nimeeleweka!
 
Back
Top Bottom