Watanzania sasa tuulizane; Rais bado anasafiri duniani kutafuta misaada?

Ingawa siwaeli watanzania wenzangu wanataka rais type ipi lakini una point mkuu.
 
Naona umehama kwenye mikopo unaleta ligi.

1. Covid Tanzania ni 2020, mwaka wa mwisho full wa Magu, vipi kuhusu 2015-2019 si uchumi vile vile ulikua hohehahe?

2. Miradi mingi ya Magu ni ya Ovyo
-SGR ni mradi Luxury
-uwanja wa Chato, mbuga na mambo mengine huko kwao
-Air Tanzania etc

Vyote vinakula hela havina maana yoyote atleast kidogo bwawa la umeme lina tija.

3. Gdp sasa haikui sababu ya Magu, bali inakua kwa kureverse alivyofanya nakupa mifano michache.

-Magu aliua kabisa kilimo kuanzia, Korosho alivyofanya mjuaji, Mbaazi zikaenda hadi 200, tumbaku, Pamba etc sasa hivi Mazao wa kulima wengi ni neema, So kureverse Policy zake za kilimo kumesaidia.
Soma hapa Exports za Nchi,

Ukiangalia Kikwete anaacha Nchi Tayari Exports zinafika 5B usd ila alivyoingia Magu tu Ghafla zikashuka hadi 4B na hali ikaendelea hivyo hadi 2018, ni 2020 pekee akafanikiwa kufika 6B usd, so it take him 5 year angalau kumpita Kikwete, Ila kuanzia 2021 mpaka leo Export inaongezeka toka 6.3 mpaka 7.6B usd 2023.

-kuzinguana na Majirani, wote tunajua Magu alivyoa biashara na Majirani zetu Kuanzia Kenya hadi Congo, wafanyabiashara hali ilikua tete, mama wa watu alivyoingia cha kwanza ni kutembelea majirani na kurudisha uhusiano, To the stage mpaka Tatizo likawa si wageni tena kuja Tanzania bali Polisi na Tra kuomba Rushwa kwa dola, mpaka kupelekea Mgomo wa Wafanyabiashara.

-Utalii, wakati wa Magu Arusha walikua hoi, Utalii Kikwete aliacha pato lake around $2B usd na wakati wote wa Magu hatujawahi. Vuka 2.6B usd sometime ulikua unashuka hadi chini ya 2B usd, ila Ghafla sasa hivi pato la Utalii ni 3.3B usd Record high toka nchi ipate Uhuru.

Kuna mambo mengi yamechangia Gdp kuongezeka, ila definitely Miradi ya Magu si kigezo, bali yeye ndio katuchelewesha sana tu.
 
Saiz majirani wamemchoka mwigu, wakisikia anakuja wanafunga milango apite!
 
Na huyo kikwete akatuambia mtwara itakuwa kama Dubai na kwa gesi iliyopo umeme tutakuja kuuza mpaka nchi za jirani...hawa ndio wanasiasa na sisi ndio wadanganyika
 
MwanaJF, yaani mara hii umeshayaona maendeleo ya traore?!!!😄😄😄😄

Tuambie ameshaiendeleza vp nchi yake?!!!! Umesimuliwa na nani, lissu au?!!!
Kwamba wewe si mfatiliaji wa habari za kimataifa?,Umejifungia tu Tanzania au vipi!!!
 
Na huyo kikwete akatuambia mtwara itakuwa kama Dubai na kwa gesi iliyopo umeme tutakuja kuuza mpaka nchi za jirani...hawa ndio wanasiasa na sisi ndio wadanganyika
Kwa Vision zake, Aliekuja baada yake hakuwa na Vision hio, utamlaumu Vipi Kikwete?
 
Kwani alikuwa anasafiri kwenda kutafuta misaada.
2025,tupo na Mama
 
Ndio, bado tunaombaomba! Tusipoomba kwa mzungu tunaomba kwa yesu na mtume! sio lazima kusafiri mbali, tunaenda kawe tu
 
Kama ilivyo kawaida kwa makusudi na kwa kudhamiria umeamua kuweka uongo wa kiwango cha juu

Magu anaingia madarakani Deni lilikua $18b na sio $16b

Gdp 2015 ilikua $47b na sio $49b

Magu na mama Samia hawajakopa sana kuliko kikwete. Kikwete kaingia madarakani, 2006 Deni lilikua $4b, katoka madarakani Deni lipo $18b, hivyo kakopa $14b.
Angalia kila mwaka hapa chini

and 100 others kuwa makini na data anazoweka baba mwajuma. Anawekaga mauwongo mengi
 
Kama Ndungai ni smart why hakulalamika hilo wakati wa Magu? Wote Magu na Samia wanachuana kwenye Kukopa, Ukumbuke Magu miaka michache nae Alikopa zaidi ya Trilioni 30 tena zisizo na Tija maana ongezeko lake la uchumi halikuakisi huo mkopo.
Trillion 30?? Hapo juu umetoka kusema ni kwa kipindi chake alikopa $9b, ambayo kwa rate iliyokua ya 2300 ni trillion 20

Kwa nini hapa unasema ni trillion 30??
 
Kutaja namba tu bila context haina maana yoyote. Kama mimi nilivyoweka context na wewe unaweza weka?

Na kama Unaweka mwaka 2015 ni wa Kikwete (Japo kuanzia katikati ya mwaka Biashara zilianza kufungwa toka Magu alipochaguliwa na CCM) basi jumlisha pia na Debi la 2011.

Kwenye data zangu deni la 2011 sijaliweka kwenye data za Magu. So utarudi pale pale round.

Pia Ukipiga mahesabu hapo
1. Deni per year
Kutoka 4B mpaka 18B kwa miaka 10 ni around 14B ambayo ni roughly 1.4B kwa mwaka, wote Samia na Magu wamekopa zaidi ya hicho kwa mwaka.

2. Deni vs Gdp ratio
Ukiweka hilo deni 14B Kikwete Gdp kaikuta around 18B kaiacha around 49B unapata around 31B ambayo ni ratio roughly 2.21 still better value.
 
Link uliyoweka inapingangana na ulichoandika, export iliongezeka kwa $2b, maelezo yako data zilipaswa ziwe zimeshuka na sio kuongezeka

Korosho haikushuka, ndio ilikwenda juu kuanzia uzalishaji hadi mapato

Kwenye cashewnuts umesema uongo wa hali ya juu. Korosho wakati JK anaingia iliporomoka hadi kufikia $25m kutoka $68m aliyokuwa nayo mkapa, japo baadae ilianza kupanda. Kikwete nae alifanya nn korosho ikaporomola hivyo 2007, aliua wakulima?

Jk anaondoka export value ya korosho ilikua $196m, but magu aliipeleka hadi $500m, hatujawahi kufika hiyo level hata kwa Sasa. Hapo utaweza vipi kusema aliua hiko kilimo?
Pitia hapa usome tena vizuri trend ya korosho kutoka BOT, urudi uje ufute ulichoandika


and 100 others kuwa makini tena na taarifa za baba mwajuma. Anaweka uongo mwingi
 
Hahaha
 
Context ipi? Nimerekebisha namba ambazo umeamua kuongopa

Nijumlishe debi la 2011? Sijakuelewa

Kikwete alikopa kuliko hao wawili, hii ni data ulizoweka mwenyeweaana umesema magu alikopa $9b ,na Samia kakopa $7b

Wote hao hawajamfikia jk hiyo $14b

Unapata mahangaiko ya bure unaamua hadi kupika data ili kujiridhisha ya nini? Wenyewe wote hao hakuna anayejali hilo
 
Trillion 30?? Hapo juu umetoka kusema ni kwa kipindi chake alikopa $9b, ambayo kwa rate iliyokua ya 2300 ni trillion 20

Kwa nini hapa unasema ni trillion 30??
Sababu 2021 ipo shared kati ya Samia na Magu, nimeweka tu kwa Samia sababu shared ya Magu na Kikwete nimeweka kwa Magu. Ukiangalia data za Bot Q1 2021 ambayo uongozi wa Magu bado ulikua madarakani deni ni Trilioni 61.8


Hakuna data nzuri za miezi 2015 ila tulianza na Trilioni 20 tu kamaliza na Trilioni 34, so fanya hesabu zako mwenyewe kilichokopwa na Magu ni between Trilioni 27 mpaka 40, kama una data za Quarter za 2015 Niwekee.


Hii video ya Tundu Lisu ikisisitizia Nilicho ongea.


View: https://x.com/bavicha_taifa/status/1361397249331392514/mediaViewer?currentTweet=1361397249331392514&currentTweetUser=bavicha_taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…