Watanzania tuanzishe utaratibu wa kuchangia vijana kama mtaji au fursa

Acha mkuu.Cyo powa walijinyonga?
Inasemekana walikunywa Sumu. Ila kwenye msiba walidanganya wakasema waliumwa ghafla. Ila ili kulinda heshima ya familia na standards zao walidanganya kuwa "marehemu aliumwa ghafla na akafariki"
 
Mimi nimekutana na kinyozi amesomea masuala ya upasuaji, surgeon. Nikadhani ni kamba. Jamaa katuonesha pdf ya vyeti kwenye simu yake. Sikuwahi kudhania mtu kasomea upasuaji/surgeon akakosa kazi.
 
Duh cio powa mzee.we unazan saikolojia yake iko sawa maan beki tatu wengi ni walioishia la 7 afu salary n 70-100k af na mentality ya jina beki tatu,bd kutuknwa,kaz kibao aisee.
 
Mimi nimekutana na kinyozi amesomea masuala ya upasuaji, surgeon. Nikadhani ni kamba. Jamaa katuonesha pdf ya vyeti kwenye simu yake. Sikuwahi kudhania mtu kasomea upasuaji/surgeon akakosa kazi
Iyo coz ipo Tz?
 
Viongozi wa dini hawatasaidia chochote kwenye hilo wazo lako maana hizo fedha wanazitaka wao wafanyie mambo yao.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] chief hustling kwakiswahili ni nini?
 
Wahindi kufanya biashara siyo lazima awe na mtaji.

Akishakodi godown au frame anaweza kuchukua bidhaa za kuuza kwa mali kauli kwenye viwanda vya wahindi wenzao.
Ndio support inayozungumzwa hapo sasa
 

Wewe ndio umeandika logic kuliko hata mwenye uzi mwenyewe, wasomi wengi spirit ya upambanaji hawana kabisa, mfano mtu anatoka mtwara kwenda mwanza interview kwenda na kurudi kama 300000k , kosa hiyo aende newala aoke korosho safi afunge hata vipaketi akatege mbezi mwisho atauza tu vitaisha au achomoke akanunue kuku tandahimba apeleke mtwara mjini kwenye masoko asome mchezo hawezi au ajiongeze afike njombe achukue viazi vya chips apeleke hata masasi baada ya tafiti lakini wapi kila leo anazurura mikoani kwenye usaili haya umri unasogea tu kila leo
 
Elimu yetu inafanya mtu awe muoga na kuamini kazi za ofisini ndio maisha wakati ni kujilemaza Angalia mtu kamaliza stashahada au shahada yake huyu anaufahamu anakubali kulala ndani muda wote huku akifanya application za hapa na pale wakati alitakiwa aende mtaani kwa mafundi pikipiki ajifunze hata idea za bodaboda akishajua atapata pa kuanzia au kwa sababu ana uelewa atafute hata mafundi wa umeme wa magari akiweka nia atajua kwani atafundishwa mtaani huku akijisomea kwenye mitandao ili aimarike zaidi, lakini anaomba kazi miaka 6 au 7 hajapata na hana ujuzi wowote ambao hautaki hata ada unataka tu ajichanganye apige sendo na jinzi azame kijiweni apambane hakuna atakae kusupport kama hajaona la maana unalofanya hayupo. Kikubwa umemaliza chuo ingia mtaani saka ujuzi wowote ule
 
Serikali na TRA wajibu wao ni upi?

Serikali hawana mchango wowote au wao ni kuwakamua watu tu? Rejea Diamond na saga lake.

Rejea mikopo ya elimu ya juu Kwa ajili ya kulipia elimu kwenye vyuo vya umma kuliko vyuo private. Rejea msururu Kodi na tozo.

Rejea zinazoitwa bima za afya kuhakikisha wazima wamo ili.kulipia wagonjwa.

Rejea ajira na vyeo kuwa na hati miliki ya walio navyo na familia fulani fulani.

Rejea malipo na marupurupu manono kwa vigogo na kutolipa kwao kodi.

Rejea vigogo kutostaafu. Kina Lukuvi, Chikwette na wenzao wamekuwapo maofisini tangu lini?

Nk, nk.

Serikali haina afueni yoyote Kwa watu wake?
 
Uko kijijini wanatengeneza barabara, unaona kuna. Mitambo greda, skaveta, unashindwa kumfuata hata operater kumuomba akuelekeze japo umlipe chochote upate ujuzi ili ubaki unatafuta namna ya kupata leseni na cheti plus elimu uliyonayo utapata michongo huku ukitafuta ujuzi wa mitambo mingine lakini anzia mtaani, sasa wenzako wanashangaa mitambo na wewe unatoka kuishangaa huku mkipiga story za simba ya yanga au dimond na kiba elewa mtaa ndio utakutoa hakikisha una potential zaidi ya moja usikubali kumiliki vyeti pekee bila ujuzi wowote huyo baba yako anaejiweza ukishapata ujuzi halafu mweleze naomba niende shinyanga chuo cha serikali cha mitambo nikazuge miezi miwili nipate cheti ili niwe na leseni maana kuoperate mitambo naweza atakupa support kabisa na connection atatafuta bila hiyana
 
Tatizo sisi ngozi nyeusi hatuna akili. Yaan Kila kikundi kiwe cha ukoo, kazini, familia, ni kujadili michango ya kusaidiana kwenye misiba tu. Hata hivyo vinavyoitwa vikoba sometime ni upuuzi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…