Ndio nyie hao tunaowasema, hebu angalia hii procedure ambayo kwa hapa kwetu ingekuwa kama kwenda sayari ya Pluto na kurudi...
View attachment 2320886
Na hii ni safari ya kwanza wanaitumia...teknolojia hii...
Kwa hapa kwetu tumeunda taasisi ya teknolojia ambayo kazi zake ni kufuatilia wakosoaji wa serikali wanaandika nini mitandaoni na kuwatoza fedha maradufu watumiaji wa mitandao wanaotafuta tu namna ya kujiajiri katika ulimwengu huu wa utandawazi unaoenda kasi.
Tunapenda mno vya bure. Tunavuna kwenye mashamba ya wenzetu. Tumeletewa bure mitandao kurahisisha mawasiliano, sisi tuna watu wameajiriwa wakilipwa mamilioni eti kupanga bei katika kutumia mitandao hiyo. Je kama Watanzania tuliwekeza nini katika mitandao hii hadi tuvune?
Afrika Mashariki tulikuwa wa kwanza kupewa, na si kupigania uhuru kama wenzetu, lakini tutakuwa wa mwisho kutetea na kulinda uhuru wa watu wetu....shame, shame, shame!