Watanzania tuchutame, Uchaguzi Mkuu nchini Kenya umetuacha uchi

Watanzania tuchutame, Uchaguzi Mkuu nchini Kenya umetuacha uchi

Kwa kweli uchaguzi wa Tanzania, chini ya serikali ya CCM, na yule mwovu mihela, ni alama ya uovu unaokosa jina stahili.

Kenya wapo juu, wapo mbele, wamestaarabika, ni binadamu kamili waliohitimu evolution, siyo hapa kwetu ambapo eti ukipiga kura ukakae mbali, usione wanavyoiba na kubadilidha matokeo.

Sisi katika demokrasia, tumekuwa nchi mkia. Tume ya uchaguzi inajua kuwa jukumu lake kubwa ni kukata majina ya wagombea wa upinzani!!
Kuna nyakati Tanzania ilikuwa ni nchi ya kupigiwa mfano na hadi kwenye mikutano ya UN mjumbe wa Tanzania akisimama, kila mtu anatulia kusikiliza.

Siku hizi hali ni tofauti hadi inahitaji eti Royal Tour kuitambulisha Tanzania...inashangaza, inasikitisha na inaudhi. Where did we go wrong?

Kila mtu anajua sababu isipokuwa wapuuzi ndani ya ndani ya chama tawala CCM. Katika muda mfupi tumesukumiziwa viongozi wasio na sifa, uwezo wala weledi na matokeo yake tunayashuhudia!

Tunaongozwa na wanafiki na walafi hadi wakati mwingine unaona aibu kujitambulisha kama Mtanzania. We are a laughing stock!
 
Swali gani ulitaka majibu boss? Ujue humu sio chumba cha mtihani hivyo uwe unapitia marking scheme yako.
Kwa hiyo unaposoma na ku'quote' yaliyoandikwa na mchangiaji hutilii maanani kilichoandikwa?

Hapo juu uli'quote' niliyoandika mimi, na kutokana na ulichoweka ili nikisome, nikauliza swali. Sasa unauliza ni swali gani nililokuuliza?
Kitu muhimu kwako ni mambo ya "mitihani", ambayo hayapo hapa jukwaani!
 
Kwa hiyo unaposoma na ku'quote' yaliyoandikwa na mchangiaji hutilii maanani kilichoandikwa?

Hapo juu uli'quote' niliyoandika mimi, na kutokana na ulichoweka ili nikisome, nikauliza swali. Sasa unauliza ni swali gani nililokuuliza?
Kitu muhimu kwako ni mambo ya "mitihani", ambayo hayapo hapa jukwaani!

Hatuchukulii kila mchango kwa umuhimu huo bro, ukiuliza swali kama halijajibiwa ni jambo la kawaida kabisa maana sio mtihani. Fahamu humu ni mitandaoni, sio kwenye chumba cha mtihani useme kwamba kila swali lina marks kadhaa.
 
\
Kenya wametupiga za uso'
MICCM inatamani Kenya wapigane yapate cha kusema.🤣🤣
Ni jambo la kustaajabisha sana kwamba wapo baadhi ya Watanzania wanakesha wakiomba na kutamani machafuko yatokee Kenya.

Kinachawafanya wawe na fikra hizo za kishenzi ni ili wapate nafasi ya kuhalalisha chaguzi zetu ambazo huandamwa na uchafuzi na udanganyifu.

Vyombo vyetu vya dola na hasa polisi vimekuwa mstari wa mbele kuwalinda wezi wa kura na kuwa chanzo cha vurugu kwenye vituo vya kupigia kura
 
Lakini toka lini nyani akaona kundule? CCM haijawahi kuwa na aibu hata mara moja. Hebu tazama viongozi tuliowahi kusukumiziwa na CCM!
Communists will never give you a free and fair election.

CCM + CCP = Disaster.
 
Communists will never give you a free and fair election.

CCM + CCP = Disaster.

Basi angalau tuwe na ujasiri wa kukiri hii nchi si ya kidemokrasia. Mbona zipo nchi nyingi tu zina katiba isiyoruhusu mawazo mbadala?

Tatizo la Tanzania ni unafiki unaorutubishwa na ujinga. Mtu unaingia madarakani kwa nguvu ya Katiba na unaapa kuiheshimu, kuilinda na kuitetea.

Unaapa leo, kesho unaanza kusigina huku wananchi wako kimya wanakuangalia tu. What is wrong with us Tanzanians? Tunategemea nini?
 
Lile nduli lililokufa ndio liliharibu demokrasia yetu. Wachomaji huko jehanamu waongeze kuni
Lini mlikuwa na demokrasia kabla na baada ya huyo unae muita nduki😂😂😂
 


Sina la kusema, nimepigwa butwaa. Najiuliza kama ule nilioushuhudia nchini Tanzania mwaka 2020 ulikuwa ni uchaguzi kweli.

Tukubali tusikubali, huu uchaguzi nchini Kenya umetuvua nguo na kutuacha uchi wa mnyama na kama bado tunazo tuchutame.

Nafuatilia matokeo yanavyotiririka kwenye TV na kushuhudiwa na Dunia nzima, bila kusubiri ruhusa.

Eti siri katika kuhesabu kura, really? Kura zikishapigwa kuna siri gani tena? Si ni kutangaza tu matokeo? Huu ujinga aliuanzisha nani hapa Tanzania?

Salaam zetu kutoka Twitter

View attachment 2320157
Kwa kweli tumevuliwa nguo...

Kenya walianza kubadili katiba, Bongo hamtaki kabisa mambo ya katiba ili muendelee na hila zenu. CCM wanajua wanachokiogopa na sio uchaguzi mfumo mzima wa kufanya siasa ni wa kiwaki hapa bongo
 
Namuona Kenyata anaenda kupiga kura akiwa hana rundo la maaskari na wanajeshi waliojihami kwa bunduki wakimzonga zonga

Huku kwetu wkt wa upigaji kura kule Dodoma tuliona Magu akiwa na lundo la wanajeshi wenye silaha za kivita utafikiri tupo Afghanistan
Uliona wanaacha kulinda raiya na Mali zao na badala yake wanalinda watawala na vyeo vyao ujue SI salama Tena.
 
Uchaguzi wa Kenya unasimamiwa na JK wa Tanzania, usisahau hilo
JK anasimamia Uchaguzi Kenya kwani yeye ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya? Yeye ni kiongozi wa Timu ya waangalizi wa Uchaguzi kutoka Afrika Mashariki. Zipo timu zingine nyingi zinazoangalia mwenendo wa Uchaguzi huu wa Kenya. Fuatilieni mambo kwa kina sio kudokoa vitu vichache.
 
Hapa Tanzania ni nchi ya makondoo, huku wajinga wakiwa ndio wameshika madaraka. Kitu pekee Kenya wamekosea na kukubali akina JK kwenda kuwa wasimamizi wa uchaguzi wao, wakati akina JK ndio mabingwa wa siasa za kihayawani hapa nchini.
JK na wenzake wameenda kuwa waangalizi wa Uchaguzi.....Wamekosea sana Tanzania Viongozi hawachaguliwi na wananchi. Wanachaguliwa na watu fulani tu wachache. CCM wanatuchagulia Viongozi sisi wananchi. Bado tunasafari ndefu sana ya demokrasia Tz.
 
Namuona Kenyata anaenda kupiga kura akiwa hana rundo la maaskari na wanajeshi waliojihami kwa bunduki wakimzonga zonga

Huku kwetu wkt wa upigaji kura kule Dodoma tuliona Magu akiwa na lundo la wanajeshi wenye silaha za kivita utafikiri tupo Afghanistan
Na bado akafa kirahisi pamoja na rundo la walinzi. Waliopo wajifunze
 
Eti siri katika kuhesabu kura, really? Kura zikishapigwa kuna siri gani tena? Si ni kutangaza tu matokeo? Huu ujinga aliuanzisha nani hapa Tanzania?
Kabisa. Eti kura za majimboni Tz hazitangazwi mpaka zitangazwe na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi. Wenzetu kule wamesema kila anayetaka kujua na kujumlisha kura afanye ilimradi asitangaze mshindi, kazi hiyo itafanywa na Tume. Huku kwetu mambo ni ya hovyo mno. Rais Tz hachaguliwi na Wananchi kabisa. Tuna mifumo mibaya sana.
 
Back
Top Bottom