Watanzania tuelewe nafasi ya Rais kama Kiongozi wa nchi na tumheshimu Rais Samia Suluhu Hasani

mama D

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
19,981
Reaction score
35,581
Watanzania tumheshimu na kumuombea sana Rais wetu Samia Suluhu Hasan tusisahau kwamba Rais wa nchi amebeba hatma ya nchi na wananchi wake

Nimesikia na kufuatilia kwa uchache sana mambo yanayoendelea mitandaoni na vile yanavyopokelewa na jamii ya watanzania nimejifunza mambo muhimu moja kubwa likiwa ni kukosekana kwa uzalendo na maadili kwa watanzania, na pili udhaifu wa fikra au ujinga pamoja na matumizi mabaya ya teknolojia haswa kwa habari za mitandaoni.

Mtu yeyote mwenye mdomo au uwezo wa kuandika anaweza kuongea au kuandika na kupost kitu chochote mitandaoni - ila inahitaji mtu mwenye akili na uwezo wa kuchambua mambo kujua kwamba bila uthibitisho, sio kila kinachoongelewa au kuandikwa ni cha kweli!
Kama ambavyo mtu anashabikia jambo ambalo limeandikwa au kuongelewa, na ambalo hajathibitisha ajue hata yeye watu wanaweza kushabikia jambo linaloongelewa au kusemwa kuhusu yeye ambalo hata yeye halijui!

Watanzania tubadilike, kuwa kwetu nyuma ya keybords kusitufanye tukaongea na kushangilia mambo maovu yanayoumiza nchi yetu, viongozi wetu na hata sisi wenyewe na vizazi vyetu...

Ni wakati muafaka sasa kwa kila mzazi na kila mwenye nafasi ya kusimama kama mlezi kwa watoto na vijana wa Kitanzania kuwakumbusha na kuwafundisha kuwa wazalendo na kuwa na heshma, kukumbatia upendo kwa ajili ya kujiletea maendeleo wao wenyewe na nchi.

Tuwakumbushe na kuwafundisha watoto na vijana kuipenda Tanzania, kuwapenda watawala na viongozi wetu, na kujipenda wao wenyewe kwa kusimama katika kweli na haki, kutofuata na kutoamini mambo yasiyo na ukweli au ushahidi na kutojkujihusisha na tabia mbovu kwani wanapojipenda na kujitunza, hawatoingia kwenye matatizo.

Tuwalinde watoto na vijana wetu kwa kuwapa elimu na kuwatia ufahamu wa kuacha mihemko ya kingono kwa kuachana kabisa mitandao inayosambaza habari za ngono na kila uchafu kama wenyewe wanavyoziita "connection".
Vijana wanapaswa kukua wakielewa kuwa ngono haifai, na kujamiiana kunapaswa kuwa na nidhamu na kutumika kwa makusudi ili kuzalisha binadamu wapya na sio kutumika kwa kitu cha kufurahisha."

Kijana anatakiwa kujua kuwa "Uzalendo ni upendo kwa nchi yake na watu wake, lakini pia anatakiwa kujua hilo haliwezekani bila kuwa na subira na kujiepusha maovu huku akitoa maoni na kukemea maouvu kwa njia ya staha bila kusema uongo au kutumia matusi au kutoa maneno ya kuudhi."

Uzalendo ni hisia ya upendo, kujitolea, na hali ya kushikamana na nchi au serikali. Kiambatisho hiki kinaweza kuwa mchanganyiko wa hisia tofauti kwa mambo kama vile lugha ya nchi ya mtu, na nyanja zake za kikabila, kitamaduni, kisiasa au kihistoria.

Unachohitaji kujua; ni pamoja na wale wanaoamini Mungu yupo kumpenda Mungu, kuipenda nchi yetu Tanzania, kuwapenda wazazi wetu, kuwapenda watoto wetu, kuwapenda ndugu zetu; tunatakiwa kujua jinsi wanadamu wanavyobadilika, na kujipenda mwenyewe pia.

Tamaa ya mamlaka, mali na pesa imewafanya watu wengi wakiwamo watanzania kukosa kabisa utu hata kufikia hatua ya kuliumiza taifa ili tuu wapate kile wanachokitaka.

Kabla ya kutukana na kuongea maneno ya kuudhi simama kwenye nafasi yake, au msimamishe mama yako mzazi, mke wako, binti yako, shangazi yako au bibi yao kwenye nafasi hiyo halafu uone kama ingekuwa rahisi kwao kuongoza hili taifa wa amani na utulivu uliopo.

Tendelee kumuombea Rais wetu na Mama yetu Samia Suluhu Hasan na kuliombea taifa letu.

Kwa wale waamini wa Mungu tunakumbushwa​

1. Kutii Mamlaka​

Warumi 13: 1-5​

"Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu.
Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri."

2. Utii na heshma kwa wazazi - Mzazi ni yule aliyekuzaa pamoja na yule mwenye rika sawa na alieyekuzaa​

Kutoka 20:12​

“Waheshimu baba yako na mama yako, ili uishi maisha marefu katika nchi ninayokupa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako."

Quran inatukumbusha kuheshimiana​

Utu wa kila mtu aliopewa na Mungu lazima uheshimiwe, bila kujali imani yake, rangi, asili ya kabila, jinsia, au hali ya kijamii (Quran, 17:70). Kwa sababu kila mtu ameumbwa na Mungu Mweza-Yote, Muumba wa wote, ni lazima wanadamu watendeane kwa heshima, staha, na fadhili-upendo kamili.
70. Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchikavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilishakwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba
 
mama D umefanya jambo jema sana kuwakumbusha watanzania
 
Kabla huja claim heshima kwa watu lazima uwe katika hali ambayo inakuheshimisha. Huwezi kuwa raia namba moja halafu ukawasaliti wananchi ukaungana na makundi yanayohujumu taifa na kuleta matabaka kisha utegemee umma ufurahie hilo. Hakuna mkamilifu duniani hapa ila pia hakuna mtu ataanza kukutukana ikiwa hamna sababu iliopelekea wewe utukanwe.
 
Kwa umri wake hata asingekua na cheo chochote,anastahili kuheshimiwa Kama mama mwingine yeyote,sio busara kumtolea Maneno machafu mtu mzima kukuzidi,na hata ambae mnalingana,sio busara pia kumtolea matusi ya nguoni,hapo tupo pamoja,

Kuhusu Kumuombea Hapana,sijawahi kuelewa anavyoongoza na hatua anazochukua kukabiliana na changamoto zinazotukabili,ombi langu asipate nafasi nyingine ya kuongoza maana tutakua pabaya zaidi ya hapa,..

UZALENDO,why mnapenda sana kutumia Neno UZALENDO kila mnapo taka ku please wananchi?? Je sisi tu ndio tuwe wazalendo Ila watawala wao wale mema ya nchi kwa wizi,ufisadi,dhulma,??Kama Kuna watu inatakiwa watuoneshe UZALENDO ni Nini,wa kwanza awe Rais,wabunge,mawaziri,...

to hell with UZALENDO,I'll deny this country kwa sahani ya chips yai
 
ni muislamu na wanaomdhalilisha ni waislamu wenzake, sasa sisi tufanyeje hapo?

Kujiita Muslim au Christian hakumfanyi mtu kuwa mwema na mwaminifu kwa watu na kwa Mungu
Wengi wanaabudu dini na madhehebu ila hawafuati sheria ya Mungu wala kumuabudu Mungu
 
Kwa umri wake hata asingekua na cheo chochote,anastahili kuheshimiwa Kama mama mwingine yeyote,sio busara kumtolea Maneno machafu mtu mzima kukuzidi,na hata ambae mnalingana,sio busara pia kumtolea matusi ya nguoni,hapo tupo pamoja,

Kuhusu Kumuombea Hapana,sijawahi kuelewa anavyoongoza na hatua anazochukua kukabiliana na changamoto zinazotukabili,ombi langu asipate nafasi nyingine ya kuongoza maana tutakua pabaya zaidi ya hapa,..

UZALENDO,why mnapenda sana kutumia Neno UZALENDO kila mnapo taka ku please wananchi?? Je sisi tu ndio tuwe wazalendo Ila watawala wao wale mema ya nchi kwa wizi,ufisadi,dhulma,??Kama Kuna watu inatakiwa watuoneshe UZALENDO ni Nini,wa kwanza awe Rais,wabunge,mawaziri,...

to hell with UZALENDO,I'll deny this country kwa sahani ya chips yai
Nakuunga mkono kwenye matumizi ya neno uzalendo. Matumizi yake yamegeuzwa kutimiza matakwa ya watawala dhidi ya watawaliwa
 
Kabla huja claim heshima kwa watu lazima uwe katika hali ambayo inakuheshimisha. Huwezi kuwa raia namba moja halafu ukawasaliti wananchi ukaungana na makundi yanayohujumu taifa na kuleta matabaka kisha utegemee umma ufurahie hilo. Hakuna mkamilifu duniani hapa ila pia hakuna mtu ataanza kukutukana ikiwa hamna sababu iliopelekea wewe utukanwe.

Kwa post yako hii hakikisha kila unaposhindwa kufanya kile wanachotaka mke wako au mume wako au watoto wako na familia yako kwa ujumla unawahimiza wakutukane

itapendeza sana ikianzia kwako
 
Back
Top Bottom