Watanzania tuelewe nafasi ya Rais kama Kiongozi wa nchi na tumheshimu Rais Samia Suluhu Hasani

Watanzania tuelewe nafasi ya Rais kama Kiongozi wa nchi na tumheshimu Rais Samia Suluhu Hasani

If your Happy to take Credit which you don't Deserve..., You shouldn't get mad when things go Opposite....

Hakuna mtu anayetukanwa na kudharauliwa kama common man Kitaa, cha ajabu hana hata mtetezi...,
 
Kwa post yako hii hakikisha kila unaposhindwa kufanya kile wanachotaka mke wako au mume wako au watoto wako na familia yako kwa ujumla unawahimiza wakutukane

itapendeza sana ikianzia kwako
Mfano hauko relevant, mimi sijaisaliti familia yangu. Nikishindwa jambo mke wangu atanisaidia bila hiyana kabisa. Hakuna siku ntatukanwa sababu sijatengeneza mazingira ya kutukanwa.
 
Watanzania tumheshimu na kumuombea sana Rais wetu Samia Suluhu Hasan tusisahau kwamba Rais wa nchi amebeba hatma ya nchi na wananchi wake

Nimesikia na kufuatilia kwa uchache sana mambo yanayoendelea mitandaoni na vile yanavyopokelewa na jamii ya watanzania nimejifunza mambo muhimu moja kubwa likiwa ni kukosekana kwa uzalendo na maadili kwa watanzania, na pili udhaifu wa fikra au ujinga pamoja na matumizi mabaya ya teknolojia haswa kwa habari za mitandaoni.

Mtu yeyote mwenye mdomo au uwezo wa kuandika anaweza kuongea au kuandika na kupost kitu chochote mitandaoni - ila inahitaji mtu mwenye akili na uwezo wa kuchambua mambo kujua kwamba bila uthibitisho, sio kila kinachoongelewa au kuandikwa ni cha kweli!
Kama ambavyo mtu anashabikia jambo ambalo limeandikwa au kuongelewa, na ambalo hajathibitisha ajue hata yeye watu wanaweza kushabikia jambo linaloongelewa au kusemwa kuhusu yeye ambalo hata yeye halijui!

Watanzania tubadilike, kuwa kwetu nyuma ya keybords kusitufanye tukaongea na kushangilia mambo maovu yanayoumiza nchi yetu, viongozi wetu na hata sisi wenyewe na vizazi vyetu...

Ni wakati muafaka sasa kwa kila mzazi na kila mwenye nafasi ya kusimama kama mlezi kwa watoto na vijana wa Kitanzania kuwakumbusha na kuwafundisha kuwa wazalendo na kuwa na heshma, kukumbatia upendo kwa ajili ya kujiletea maendeleo wao wenyewe na nchi.

Tuwakumbushe na kuwafundisha watoto na vijana kuipenda Tanzania, kuwapenda watawala na viongozi wetu, na kujipenda wao wenyewe kwa kusimama katika kweli na haki, kutofuata na kutoamini mambo yasiyo na ukweli au ushahidi na kutojkujihusisha na tabia mbovu kwani wanapojipenda na kujitunza, hawatoingia kwenye matatizo.

Tuwalinde watoto na vijana wetu kwa kuwapa elimu na kuwatia ufahamu wa kuacha mihemko ya kingono kwa kuachana kabisa mitandao inayosambaza habari za ngono na kila uchafu kama wenyewe wanavyoziita "connection".
Vijana wanapaswa kukua wakielewa kuwa ngono haifai, na kujamiiana kunapaswa kuwa na nidhamu na kutumika kwa makusudi ili kuzalisha binadamu wapya na sio kutumika kwa kitu cha kufurahisha."

Kijana anatakiwa kujua kuwa "Uzalendo ni upendo kwa nchi yake na watu wake, lakini pia anatakiwa kujua hilo haliwezekani bila kuwa na subira na kujiepusha maovu huku akitoa maoni na kukemea maouvu kwa njia ya staha bila kusema uongo au kutumia matusi au kutoa maneno ya kuudhi."

Uzalendo ni hisia ya upendo, kujitolea, na hali ya kushikamana na nchi au serikali. Kiambatisho hiki kinaweza kuwa mchanganyiko wa hisia tofauti kwa mambo kama vile lugha ya nchi ya mtu, na nyanja zake za kikabila, kitamaduni, kisiasa au kihistoria.

Unachohitaji kujua; ni pamoja na wale wanaoamini Mungu yupo kumpenda Mungu, kuipenda nchi yetu Tanzania, kuwapenda wazazi wetu, kuwapenda watoto wetu, kuwapenda ndugu zetu; tunatakiwa kujua jinsi wanadamu wanavyobadilika, na kujipenda mwenyewe pia.

Tamaa ya mamlaka, mali na pesa imewafanya watu wengi wakiwamo watanzania kukosa kabisa utu hata kufikia hatua ya kuliumiza taifa ili tuu wapate kile wanachokitaka.

Kabla ya kutukana na kuongea maneno ya kuudhi simama kwenye nafasi yake, au msimamishe mama yako mzazi, mke wako, binti yako, shangazi yako au bibi yao kwenye nafasi hiyo halafu uone kama ingekuwa rahisi kwao kuongoza hili taifa wa amani na utulivu uliopo.

Tendelee kumuombea Rais wetu na Mama yetu Samia Suluhu Hasan na kuliombea taifa letu.

Kwa wale waamini wa Mungu tunakumbushwa​

1. Kutii Mamlaka​

Warumi 13: 1-5​

"Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu.
Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri."

2. Utii na heshma kwa wazazi - Mzazi ni yule aliyekuzaa pamoja na yule mwenye rika sawa na alieyekuzaa​

Kutoka 20:12​

“Waheshimu baba yako na mama yako, ili uishi maisha marefu katika nchi ninayokupa mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako."

Quran inatukumbusha kuheshimiana​


Utu wa kila mtu aliopewa na Mungu lazima uheshimiwe, bila kujali imani yake, rangi, asili ya kabila, jinsia, au hali ya kijamii (Quran, 17:70). Kwa sababu kila mtu ameumbwa na Mungu Mweza-Yote, Muumba wa wote, ni lazima wanadamu watendeane kwa heshima, staha, na fadhili-upendo kamili.
70. Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchikavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilishakwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba
Asante sana, mama D.
 
Mfano hauko relevant, mimi sijaisaliti familia yangu. Nikishindwa jambo mke wangu atanisaidia bila hiyana kabisa. Hakuna siku ntatukanwa sababu sijatengeneza mazingira ya kutukanwa.

Kama wewe unavyojitetea kwamba hujaisaliti familia yako huku wanafamilia wanalalama
Rais nae ukimuuliza atakujibu kwamba hajakusaliti

Utatukanwa tuuuuu kama unabisha weka mawasiliano yao hapa uone familia yako wanavyolalama
 
Heshima na Maadili yote ya Kitanzania yangekuwa yamelindwa hata wewe muda huu usingekuwepo mtandaoni unabishana na wanaume.

Yoda kwani wewe ni mwanaume??? Mbona na mimi ni Mwanaume pia hahahaha

Hahahaaaa
 
Kuna matumizi mabaya sana ya neno "uzalendo", maana inaoneoana uzalendo ni kuwa Sawa na viongozi,kinyume chake ni kosa kubwa.Hii haiwezi kuwa Sawa,binadamu lazima wawe na fikra huru na sio kuendeshwa na matamko.

Tunapo weka mkazo juu ya uzalendo,basi hatuna budi kufanya ya kizalendo pia,huwezi kuiba Kura na kuidharau sheria mama ya taifa alafu ukajiita Mzalendo.shida kubwa ya Watanzania ni kuishi maisha ya kinafiki.
 
If your Happy to take Credit which you don't Deserve..., You should when things go Opposite....

Hakuna mtu anayetukanwa na kudharauliwa kama common man Kitaa, cha ajabu hana hata mtetezi...,

Simama uwe mtetezi mkuu
 
Hiyo Katiba inayokuongoza imetoka kwenye biblia na Quran

Tulia ujifunze
Hii katiba imeshindwa kushughulikia wezi wa kura, wezi wa pesa za walipa kodi.

Je hivyo vitabu vyenu vya Quran na Biblia ndio vinafundisha hayo??
 
Kujiita Muslim au Christian hakumfanyi mtu kuwa mwema na mwaminifu kwa watu na kwa Mungu
Wengi wanaabudu dini na madhehebu ila hawafuati sheria ya Mungu wala kumuabudu Mungu

binafsi katika haya maisha kama kuna kitu nimejifunza ni kutokuingilia ugomvi nisiouelewa chanzo chake, for sure kuna sababu kwa nini wanaotukana wanafanya hivyo with impunity na hata usikute sababu hazina uhusiano wowote ule na manufaa ya nchi kama wasemavyo, usikute kwenye wizi wamezibiana na wameamua kumwaga mboga, hivyo mnaotetea mnatumika tu na wakishaelewana utasikia kimya na si bandari wala ardhi yetu itarudishwa ktk kwa waarabu…
 
Kuna matumizi mabaya sana ya neno "uzalendo", maana inaoneoana uzalendo ni kuwa Sawa na viongozi,kinyume chake ni kosa kubwa.Hii haiwezi kuwa Sawa,binadamu lazima wawe na fikra huru na sio kuendeshwa na matamko.

Tunapo weka mkazo juu ya uzalendo,basi hatuna budi kufanya ya kizalendo pia,huwezi kuiba Kura na kuidharau sheria mama ya taifa alafu ukajiita Mzalendo.shida kubwa ya Watanzania ni kuishi maisha ya kinafiki.
Nyongeza: huwezi kuwa mzalendo kwa kuishi maisha ya anasa halafu unaowaongoza ni mafukara!

Wao wakiugua, wanaenda Ulaya kutibiwa. Akina sisi tukiugua, tunapambana hapa hapa.

Uzalendo uko wapi hapo?
 
Watanzania tumheshimu na kumuombea sana Rais wetu Samia Suluhu Hasan tusisahau kwamba Rais wa nchi amebeba hatma ya nchi na wananchi wake...
Upuuzi, mtupu, tumuheshimu kwa lipi? Sio, lazima kila mtz ampende rais! Huyo sio mama yetu, sio shangazi,tumempa kazi, tunamlipa mshahara, hatufanyii hisani kuwa ikulu, kwanza, ni manufaa, kwake anakula mokoto makubwa, kila anachokifanya sio hisani, ni, wajibu wake, tutamkutana kwa uraisi wake, hatutamtukana kwa jinsia, yake, madudu mengi yanayoemdelea, nchi hii, CAG kasema mashirika yote ya, umma yanafanya hasara! Rais yupo Kimya, hakuna mtu kafukuzwa , kafungwa, anacheka Cheka tu,! Hapo, lazima, tutampopoa kwa, matusi,kama, anaona kazi, ngumu, si aache tu!

PM wa Israel, ni war hero, amepigana, Vita, ni veteran wa elite IDF unit, ameipambania nchi yake kwa, miaka, mingi, lakini amefanya makosa, ya, ufisadi na nchi ipo vitani,wananchi, wanataka, aachie ngazi! Sembuse hawa wa kwetu wamekuwa raisi kwa mserereko, hakuna jema wametufanyia zaidi ya kuibq na kuifisadi nchi, escrow, Richmond, meremeta nk, harafu wanataka tuwachekee tu, fuckers assholes
 
Back
Top Bottom