Watanzania tuelewe nafasi ya Rais kama Kiongozi wa nchi na tumheshimu Rais Samia Suluhu Hasani


Uko sahihi sana
Ugomvi na matusi yanayorushwa sio kwa maslahi ya nchi
 
Simama uwe mtetezi mkuu
Wa Nani anayehitaji Mtetezi au asiyehitaji ila ndio wote tunatumia muda wetu kufanya hivyo ?

Huenda kwa mimi ku-kukumbusha ndio ninavyomtetea; kwamba hii talanta yako ya kuweza kuandika makala ukimaliza hapa labda shusha nondo za vipi huyu jamaa kitaa tunayemyonya matozo na maisha yake magumu tunamkatia umeme anaendelea kukaa gizani na bado tunamuachia madeni tele kwa kuendelea Kukopa huku na kule alafu tuna-insult intelligence yake kwamba maisha ni mazuri leo kuliko jana....
 
Kama wewe unavyojitetea kwamba hujaisaliti familia yako huku wanafamilia wanalalama
Rais nae ukimuuliza atakujibu kwamba hajakusaliti

Utatukanwa tuuuuu kama unabisha weka mawasiliano yao hapa uone familia yako wanavyolalama
Naona unaweka ushabiki mandazi mbele kama vile una vinasaba vya kizimkazi kumbe shobo tu.

Hajasaliti raia wakati kakumbatia wezi aliowateua kama viongozi wasaidizi kwake. CAG report inaongea kila mwaka
 

Okay ni sawa kama kwako kumheshimu ni upuuzi ila kumtukana ni makosa na itakugharimu
 
Watanzania tumheshimu na kumuombea sana Rais wetu Samia Suluhu Hasan tusisahau kwamba Rais wa nchi amebeba hatma ya nchi na wananchi wake
...
Umenena vyema,

Rais ni mwajiriwa wa wananchi,

Tumseme na kumshauri HEKIMA.

Tanzania yangu, Nchi yangu.
 
Hao viongozi hawastahili kuheshimiwa hata kidogo, kwa sababu wamewatumbukiza wananchi katika lindi la umasikini na ujinga huku wao wakijineemesha, na badala yake wanatakiwa kuzomewa, kugomewa na kuondolewa madarakani kwa njia yoyote. Wameshindwa kuwa viongozi na wamegeuka kuwa parasites kwa wananchi, heshima itoke wapi.
 
Uko sahihi sana
Ugomvi na matusi yanayorushwa sio kwa maslahi ya nchi

lkn hawajawahi kuwa kwa maslahi ya nchi from day one hivyo ni muendelezo tu wa failure na incompetence kila mahali, garbage in, garbage out …
 

Hawastahili kutukanwa pia
 
Kujiita Muslim au Christian hakumfanyi mtu kuwa mwema na mwaminifu kwa watu na kwa Mungu
Wengi wanaabudu dini na madhehebu ila hawafuati sheria ya Mungu wala kumuabudu Mungu
Hu
Huwezi kuwaibia wananchi bila huruma halafu utegemee kuheshimiwa. Ninamuombea mabaya tu
 
Urais kwenye nchi za kidemokrasia huja na gharama zake.

Moja ya gharama hizo ni kusemwa vibaya, ikiwemo kutukanwa na raia...
Unaweza kuwa sahihi, lakini kwa mila na desturi tuna namna bora ya kuheshimu wakubwa wetu kwa umri ama madaraka waliyonayo. Tusilete umagharibi kisa uhuru wa kusema chochote. Moja ya tunu zetu kama taifa ni kuwa na utu.

Hii ni bila kujali nani amewahi kuvunja utu wa mtu, halileti haki kwa namna yeyote ile kuvunja utu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…