Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
Imetoka nyingine kuwa kuna mkutano unaanza j3 na yeye alipaswa kuwa mgeni rasmi ila hatokuwepo badala yake atawakilishwa na makamu wa Raisi.


Hapo vipi?
Mwenyekiti wa mkutano anajulikana,
Mgeni rasmi amejulikana.
Nafasi yake haipo tena.
( Naiwe hivyo. Wote sema Amina.
 
Naona mods wameunganisha nyuzi zote za taharuki
 
Sky Eclat kuna kitu unafahamu au umeamua kutibua watu tuuuuuuuuu,post zako zote kama horror movie
1571544949924.jpeg
 
Jiweke kwenye nafasi ya mhusika.

Umekaa mahali umetulia kuyasoma yote yanayoelekezwa kwako, kama haya yanayowekwa JF.

Je, yatakusaidia kujitafakari na kujaribu kufanya tofauti na vile ulivyokuwa ukifanya kabla?

'Obviously', si rahisi kubadili tabia, lakini unaweza kuweka juhudi kurekebisha mengine kwa utashi wa moyo.
natamani sana ayaone haya namuombea uhai kwenye nyama damu na mifupa
 
Hahahaha Bawacha ni muda tuu mtaumbuka
Ni muda tuu mtaumbuka endeleeni kujifariji....
 
Nilipata Ghadhabu sana, nikiwa kama mdau wa Demokrasia na haki za binadamu kuona kuna kiongoz anathubutu kuwaita Watanzania wenzake "wadudu " tena mbele ya kadamnasi na mbele ya media

Niliona hii ni dalili nyingine ya vijana walio aminiwa na Mh Rais JPM, lakin wanajimwambafy na kujivika mamlaka wasio kuwa nayo

Ila leo nimeamini jamaa hakukosea sana, nafuta kauli zangu za kejeli nilizotoa kwake siku ile,

Na inawezekana neno wadudu lilikuwa ni understatement

Nimeelewa kuwa

1)Ni Wadudu tu, wanaoweza kushinda mitandaoni wakifurahia jambo na wakifurahia au kusubiri kwa hamu ujio wa taarifa mbaya za mwanadamu mwenzao, tena kiongoz wao. Na tena wadudu hao sio jamii ya Nyuki, Siafu au jamii nyingine ya wadudu wenye akili, siafu, Nyuki na baadhi ya wadudu wana upendo, Ushirika, uzalendo kwa makundi na vichuguu vyao kuliko wapinzani wa Tz, wanaheshimu viongozi wao balaa, nawaza labda wadudu jamii ya nzi,mende na wengineo ambao hawana ustaarabu wa kuishi kijamii ndo watakuwa na sifa za wapinzani tulio nao Tz.

2) Ni wadudu tu ndo ambao kila kitu hupiga kelele ,liwe jema au baya, Mchukulie nzi, kutwa kucha yeye ni nzeee, nzeee, nzeee, anapiga kelele, anacholilia hukion, hujui kuwa anafurahia au anahuzunika, na mbaya zaid ni kuwa anapiga kelele bila kufanya hatua yoyote, Nzi hang'ati,
Ni aheri kama nyuki, akitulia anatengeneza asali, ukimzingua anapiga yowe kidogo, huelewi anang'ata. Sasa kuwalinganisha wapinzani wa Tz na wadudu aina ya Nyuki sio sawa, hawa hawang'ati ,na wala hawatengenezi asali ,kazi kupiga domo tu, yee yee yee ,hawa ni wadudu jamii ya nzi na mende

3)Ni wadudu tu ambao watakuwa na usahaulifu kama walio nao wapinzani wa Tz

Juzi juzi tu mtu wanae muona leo ni hero kwa kuwaletea habar za uzushi, alikuwa ameweka kambi la mashambulizi kwa mwenyekiti wao,

Mwenyekiti wao hajajibu hata hoja moja, na wala halijawa tatizo, leo hii mtu huyo kazusha ya kuzusha, Msigwa ameendelea na majukumu yake ya kutangaza teuzi, wanabak wanalalama, mbona tuhuma hazijawekwa sawa? Wadudu mbona mnakuwa wasahaulifu? Tuhuma za mwenyekiti mliweka lini sawa? Na imagine tuhuma za mwenyekiti zilikuw zinahusu majukumu yake ya kazi, tuhuma hiz za leo ni binafsi (afya ni mambo binafsi) .

Au ndo muendelezo wa yale yale ya double standards, chama mnataka kitawaliwe kidikteta, miaka nenda rud,mwenyekiti ni huyo huyo, et hakuna mwingine mwenye vigezo, ila mkiambiwa na sisi kama nchi hatuoni mwenye vigezo vya kumpokea JPM tunataka aendelee, mnaanza kung'aka kuwa haiwezekani ktk watanzani m50 akosekane mwenye vigezo, wadudu mbona mnashindwa kutumia logic ndogo tu?

Hivyo kwa heshima na taadhima, naomba nimtake radhi yule mheshimiwa alie waita wapinzani wa Tz kuwa ni wadudu, sababu siku ile nilimlaani vikali kwa kutumia maneno yasiyo na staha kwa watanzania wenzake

Ila kwa yanayoendelea leo, yamenifanya nitafakari, na kugundua kuwa jamaa alikuwa anajua kitu cha ziada ambacho mimi sikuwa na najua kwa wakati ule

Hivyo namtaka na kumtia moyo, ajitokeze aongezee na kutolea ufafanuzi kwa msisitizo kuwa wapinzani wa Tanzania ni wadudu wa jamii ya nzi Na mende, sio wadudu wa jamii zinazojielewa kama Siafu wanaopiga kazi balaa(hapa kazi tu), nyuki wanaotengeneza asali (wanaunga mkono serikali ya viwanda) Vipepeo wanaoruka na kusaidia ktk pollination (kama Bombadier zetu tu)Na wadudu wengine wa aina hii.

Viva JPM, Viva Tanzania.

Disability is best defined as the inability of someone to see an ability of someone else!!

Tukubali tu kuwa wewe na hao "wadudu" hamna tofauti rasmi... Wote lenu moja... Na mmeligawa Taifa letu!
Cha ajabu sasa... kufa hao wadudu...sawa... mnachekeleaga sana "kuwaua"...
Ila matatizo yakiwabishia hodi ghafla mnataka ushirika na wale wadudu "mnaowaua" ili kujifariji!
Shame on!¡
 
Pamoja ya kwamba Mh Rais amefanya mambo mengi ambayo si ya kibinadam(hasa kuwatesa watu pasipo na sababu),lakini pia amefanya machache mazuri na yatakumbukwa..siombei kimkute kifo wala ugonjwa mimi nahitaji atoke kwa amani ili baadae warithi wake wamchukulie hatua huku akiwa ana shuhudia.

Popote ulipo Mh Rais nakuombea afya njema na uzima ili nawe kikombe ulichowatengenezea wenzako kikirudie ukiwa hai.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom