Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.

Kwanza kabisa yeye hakuahidi katiba mpya, yeye kwanza anapambana na umaskini, na kuhakikisha elimu elimu elimu kwa watoto wote, umeme kila kijiji na mengine mengi.
Mafisadi wamebanwa wanarejesha hela, cha msingi matokeo ndio muhimu.
 
Mimi nasema hao unaoita watumishi ni wapumbavu kupoteza nguvu zao kuombea kitu ambacho hakipo.

Nachokiona mimi hapa mtandaoni ni waTz wengi wanahamu ya msiba wa kitaifa. Labda zile swaga za kujionesha wanahuzuni ndani ya miwani mweusi mawezimisi
 
Mnaosema nchi ina chuki,hivi chuki mnayosema itakapofika nadhani watu tutaftana,nadhani mnaotamka kuhusu chuki,mnaitaka,kwani mlinenalo ndilo mnalopewa.

Chuki zipo nchi za Somalia,DRC Congo,Libya na nyinginezo ambazo kila kukicha kunasikika milio ya risasi na mabomu,hivyo raia hawawezi hata kupata usingizi.

Wewe ambaye unauhakika wakulala bila wasiwasi,ukaenda mahali popote ukarudi nyumbani usiku wa manane kwa usalama kabisa bado unasema nchi ina chuki kweli umefikiri sawasawa?

Nchi ipo salama kabisaa
 
Tatizo la nchi yetu imelelewa ktk misingi ya kijamaa, ambayo ndani ya mifumo yake kuna usiri uliokithiri. Rais wetu anatambulika kabisa imani yake ya kidini. Kitendo cha kuficha kuhusu lililotokea juu ya afya yake akiwa ziarani kikazi ktk mikoa ya kusini, kimekosesha fursa ya kumuombea ktk siku hii ambapo makanisa mengi ya Kikristo hukusanya waumini wao kwa ajili ya ibada. Maombi na ibada ni vitu vya maana sana kwa waumini.
 
Kwa ujinga wako unamuona jiwe kama immortal, wait and see
 
Mimi mwenyewe Mkristo na tunakesha tukiomba ila sio uku mitandaoni kama ufanyavyo ww. Amin nakwambia mheshimiwa Rais atapona lakini sio kwa maombi yako ww mnafiki wa uku mitandaoni kutwa upo mtandaoni unamuombea saa ngapi au unahisi unavyo andika hapa ndio maombi hayo.?
Mimi mkristo naambiwa ktk biblia kuomba bila kukoma,kama nakukera mkuu zima data wewe
 
*Wapiga madili

*Wapinzani

*Wasomi wanaosubiria ajira zaidi ya miaka mi4

*Waliotumbuliwa

*Vyeti feki

*Wasifiaji wanafki wenye uchu wa madaraka

Bado tu unadhani ataendelea kupendwa na kila Mtu ?

Tumuombee Rais wetu maana vita aliyonayo si ya kitoto hata kidogo.
 
Mungu baba uketiye mahali pa siri palipotukuka licha ya kwamba binadamu kifo kaumbiwa,nakemea mabaya yote yanayonenwa dhidi ya mtumishi wako JJ,Magufuli ,mpe maisha marefu ,wabaya waspate pa kusemea,mlinde daima .mjalie afya njema huko aliko,Amen.
Yaani ningeweza kulike hapa mara milion nyingi ningefanya hivyo! Kama Ni mgonjwa Mungu kwa rehema zake amponye amrejeshe ktk Khali yake ili aeendelee na majukumu ya kuliongoza taifa.
 
Pole sana ndugu.
Kulia kunapunguza stress. Lia tu upate nafuu.😭😭😭
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…