Heshima kwenu wakuu,
Kuna habari zinasambaa kwamba rais wa Tanzania John Magufuli anaumwa wengine wanasema amekatiza Ziara ili kushughulikia Maswala mengine ya Kitaifa. Hili sina tatizo nalo.
Kinacho niumiza ni kuona Taasisi ya rais akiwemo Msemaji mkuu wa Ikulu na Msemaji wa Serikali kutokanusha au kuweka sawa habari hizi zinazo sambaa.
Ukiacha uongo ukaendelea kuongelewa unageuka kuwa kweli
Rais sio mali ya Ikulu bali ni Mali ya Watanzania wote.
Msemaji wa Ikulu Gerson Msigwa huwa ni mwepesi kukanusha na kutupa update za rais.
Tunapata wakati mgumu kuelewa.
Maradhi kwa binadamu ni kawaida, kama anaumwa ni haki wananchi wake wakajulishwa na maendeleo yake yakaelezwa kwa uwazi.
Tumefanya hivyo kwa Baba wa Taifa Nyerere, skofu Mkuu Mwandamizi Yuda Thaddeus Ruwa'ichi, Benjamin Mkapa na wengine wengi.
Kama yu mzima wa afya tujulishwe ili roho zetu zitulie.
Ni haki yetu kujua rais alipo na maendeleo yake sababu anaishi kwa kodi zetu na tulimchagua wenyewe. Ndo maana Televisheni ya Yaifa inamuonesha popote aendapo bure ili wananchi wajue anachofanya rais wao.
Hata kama kapumzika Ikulu, hakuna sababu ya kuzua taharuki.
Tunajua rais wetu anapenda mpira hasa timu ya Taifa, Janana timu yetu imeshinda hatunaona anapongeza na kushangilia kama kawaida yake.
Hata Msemaji wa Ikulu hajatuma picha akiangalia mpira wa watoto wake kama kawaida yao.
Tunamtaka rais wetu.
Asanteni sana