Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
Ni kweli MTAZAMO, kapotea siku mbili tuu maneno mengi ooh yuko wapi mtukufu, mara ooh tuambiwe ukweli.
Wakati Ben Saanane miaka mitatu sasa hajaonekana wala nguo zake hazijaokotwa. Azory miaka miwili katoweka kama ndege ya Malaysia.
Mie naamini sana katika maombi, najiuliza hivi yule Mkurugenzi wa Nachingwea kama hana kosa na hakusikilizwa bali alipokea matusi hadharani, jee akiwa mtu wa maombi na akawa kaomba kwa Mungu wake amlipie uonevu ule itakuwaje? Sio yeye tuu wako wengi kama yeye maombi yao hayawezi kutimia kwa sababu Mungu anaona kanunua Airbus? Au Bombardier?
Tafakari!
Uliona au ulihadithiwa.? Tafuta clip uone kama aliitwa tu akaanza kufokewa bila kuulizwa.
 
Kuna wahuni na baadhi ya wanasiasa tuliowaheshimu wameonesha kushangilia tetesi hizo! Tabia za kichawi kabisa hata kama huwangi usiku.

Rais wetu ametenda mambo makubwa na yenye manufaa kuliko madhaifu mnayomhukumu nayo na kumtakia mabaya.

Serikali itoe taarifa rasmi badala ya kuacha redio mbao ziendelee kulisha jamii chuki na tabia mbaya kabisa kuombeana mabaya kwa matamanio binafsi.

Ukweli haupiganiwi bali unajipigania.

Kama amefanya Mema mengi unafikiri ni kwa nini wafurahie Habari mbaya juu yake Mkuu ?
 
Huyu kigogo ashtakiwe kwa uhaini.simpendi magufuli kwa baadhi ya matendo yake lakiini kumuombea kifo huo ni zaidi ya unyama.
...hakika mkuu kumtangazia kiongozi mkuu wa nchi uzushi wa namna hii nisawa na uhaini...sheria ichukue mkondo wake ili iwe fundisho kwa wapumbavu wengine
 
Chuma
IMG_20191019_155934.jpeg
 
Siku hizi Twitter ni zaidi ya Facebook na Instagram imekuwa na umbea, uzushi wa kutosha

Kwa taarifa yenu Rais Yuko imara zaidi ya siku zote

Endeleeni kuota anapiga miaka 10 net halafu anaacha jembe
 
Akishika Samiha anawatoa wote
Watajimwambafaia wapi sijui.Mtu aliyeelimika utazama kesho yake.Suleman Jaffo,Jokate,Mtaka ni hazina bora ya kesho,malaya wa kisiasa watafurushiwa madirishani
 
Unavyoishi na watu pindi unapopata matatizo ndio muda muafaka wa kupata mrejesho. Haya ni automatic by nature. Kama kuna mazuri kafanya huo ni wajibu wake, ila hilo halizuii watu kuonyesha hisia zao, hasa kama hakuwatendea sawa. Kama wewe unaona ana mazuri muombee maana hiyo ni haki yako, sio lazima na wengine nao wafanye utakavyo ww.
Hata JK aliwahi kuombewa itikafu ili afe, ila leo tunaambiwa na rais bora kuwahi tokea. Hakuna jipya kwa akili za watanzania
 
Siku hizi Twitter ni zaidi ya Facebook na Instagram imekuwa na umbea, uzushi wa kutosha

Kwa taarifa yenu Rais Yuko imara zaidi ya siku zote

Endeleeni kuota anapiga miaka 10 net halafu anaacha jembe
Asante

Ila aki R.I.P Unitag mkuu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom