Watanzania tuelezwe ni wapi alipo Rais wetu Mpendwa John Magufuli, ni haki yetu kujua

Status
Not open for further replies.
Ukweli ni ukweli tu...tetesi hazipuuzwi.... Na sio mambo ya Roho ya kufurahia tetesi...wake up stand up...bi dada

Hongera kwenye kua bi dada, ila mie ni man.
Pia haya mambo ni maamuzi binafsi. Ni kweli kija jambo huanza kama tetesi lakini ikitegemea na chanzo cha taarifa na mazingira vinaumuhimu sana.

Kama umenisoma vizuri tatizo langu ni hapo kwenye chuki ya kupindukia. Roho mbaya inamtafuna mhusika na ni hatari kwa ustawi wa afya.
 

Kama amefariki alale pema peponi maana syo wa kwanza kufariki, mochwari zote nchini zina maiti, na ni binadamu kama yeye pia
 
Very strange,hizo habari nzito bila kudhibitishwa kwanza ni hatari sana hata kufikiria vile.
Lakini hakuna mtu atakakaeishi milele.
Ila Magufuli atakuwa amepata mtihani mkubwa sana.
Na kama hizi habari ni za kutungwa au kama zina aina ya ukweli ndani yake,Tanzania haitakuwa ile ya jana.
 
Kutakuwa na misosi wa bure katika kipindi chote cha maimbolezo. Ni wakati wa kwenda kula vizuri Ikulu.
 
Iwapo leo Jumapili tarehe 20-Oct-19 hatutahabarishwa Mhe. Rais wetu Mpendwa amesali kanisa gani kama tulivyozoeshwa na bwana Gerson Msigwa, ninawaomba Mlioko Chato mtuambie ni nini kinaendelea ikiwa ni pamojana kutujuza kama Kipenzi cha wengi,Rais wetu JPM yupo huko Likizo.

Hatujamsikia siku tatu au nne sasa na kwa style yake ya kutaka kuadress mambo kupitia live streaming pamoja na live coverage ya radios na television inatupa mashaka iwapo Mhe. yupo Chato kapumzika au vipi.

Kwa tunaomfahamu,Mhe. anaipenda Chato vibaya mno. Ameifanyia makubwa chato na mara zote huenda Chato mapumzikoni.

Kwa kuwa tumezoea kila mahali anakokuwepo lazima kishindo hasa cha wana usalama kiwepo inawezekana safari hii kaamua kwenda kimya kimya na kama mkuu wa nchi halazimiki kila anakokwenda itolewe taarifa. Lakini pilika pilika zisizo za kawaida pamoja na ulinzi wa kishindo vitadhihirika. Mlioko Chato tuambieni, Mhe yupo huko? Pale kwake kuna pilikapilika zipi? Ni Kipi kinaendelea huko?

Kama Mhe. yupo mapumzikoni namtakia mapumziko Mema, Mungu azidi kumpa nguvu, arejee kwenye majukumu yake kwa kasi na ari mpya.

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…