Taifa, Afrika na Dunia nzima, tunamhitaji JPM akiwa Hai, mwenye afya na nguvu. Amefanya mengi tangia akiwa waziri na sasa akiwa Rais. Ni mfano na kielelezo bora kwa uwezo wa waafrika kupanga na kusimamia maendeleo yao wenyewe.
Tungepata viongozi watano tu kama yeye, Afrika ingeendelea kwa kasi.
Kwa mdodroro wowote wa kiafya, tunamuombea afya njema, hali na nguvu ya kuendelea kuliongoza taifa sasa na kuwa mshauri mkuu wa viongozi wa kiafrika baada ya kung'atuka.
Mtazamo kwamba wengi wanamchukia sio kweli, hao ni mafisadi, wenye vyeti feki, wahujumu uchumi, majangili, na vibaraka wa mabeberu.
Naamini Mungu atamlinda, atamkinga na kumuongoza vyema Daima.