Kite Munganga
Platinum Member
- Nov 19, 2006
- 1,773
- 952
Barua ya uteuzi pekee haitoshi kutuwaaminisha wananchi kuwa Mzee baba ni mzima waafyackabisa.
Wanaomzushia kuwa anaumwa wamekuja na hoja zifuatazo.
1: kusitisha ghafla ziara kanda ya kusini
2: Kubadilishwa wahusika kwenye matukio zaidi ya mawili ambayo ililipotiwa kuwa atakuwepo yeye mwenyewe.
3: Reaction yake baada ya wizi wa vipande vya komputa. Kwa ninavyomjua asingeligumbia macho.
4: Barua ya uteuzi imekuja ikiwa na makando kando mengi. Miongoni ni location ya mheshimiwa wakati wa uteuzi, tarehe ya kuanza uteuzi na tarehe ya kuapishwa katika maeneo yao, sahihi kupishana na za awali.
Vile vile barua hiyo nimekuja na sambamba na taarifa ya TAKUKURU ambayo inaonesha maagizo ni ya tar 15 Oct 19. Sasa huenda na hili la uteuzi lilifanyika kabla.
Tuombe wahusika watafute chakula cha kutushibisha hii barua ni Sawa na kuwapa chipsi wapasua mawe. Tunahitaji kushibishwa la sivyo tutaendelea kula matango pori kwa kukosa mlo mhusika.
Barua ya uteuzi imeshindwa kufanya kazi kwani ilitakiwa pia iendane na kanusho la uvumi uliopo kutoka Idara hiyohiyo kitu ambacho hakikufanyika, lakini turudi nyuma hebu angalia kwa Nyerere kuna lugha ilitumika "Hali ya baba wa taifa ni mbaya" hii ilifanya watu wasiwe ndege wala wanyama tofauti na hawa wenzetu ambao nafikiri hawajaamua kuvaa nguo au kutupa nguo