Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Ni tamaa tu. Kila Rais akiingia anaangalia cha kupiga mnada. Nini kimetushinda kwenye bandari zetu hadi za Maziwani huko? Tunashindwa kufanya maamuzi na kujiendeleza, tunamchukua mwekezaji ambaye naye anataka profit. Mwekezaji ndio mwenye kutupenda? mwenye kuipenda Tanzania? Mwenye uchungu na TZ? Mwenye kuijivunia Tanzania? This will be one of the riskiest decision kufanywa na Taifa hili kupitia kwa viongozi wake vilaza. Kwani waliounda DP World sio binadamu? Kwanini tunaamnini katika kufanyiwa vitu? Kwanini tunaamini katika kuendelezwa na siyo kujiendeleza?
 
Hakuna anayeipenda Tanzania hata ukiweka watanzania ni mwendo wa kuiba mwanzo mwisho hakuna cha maana watakachofanya
 
Ubinafsishaji wa enzi zile uliinufaisha Serikali, mashirika yake na makampuni binafsi. Wananchi, mmoja mmoja au makampuni yao binafsi hawakuwahi kushirikishwa Kama ilivyo kwenye yale machache ya Twiga Cement, TCC CRDB....nk.

Kama TPA imepata mwekezaji wa kimkakati basi apewe hisa 50+1.... Hisa 49 zinazobaki Serikalini .... Zigawanywe kwa wananchi na makampuni binafsi kwa asilimia 25, Serikali ibaki na asilimia 24 tu. Iwe hivyo kwa mashirika yote yanayoitwa ya umma.....kwa kufanya hivyo mwananchi ambaye ndie mmiliki wa mali za nchi hii atakuwa na sauti.... Vinginevyo ni mipango ya ubadhirifu tu inaendelea.
 
Ukishauza bandari, ndio unakuwa umeuza nchi. Bandari mpaka wa Kimataifa wa nchi. Kitakachofuata ni viwanja vya ndege. Kuna mtu atakuja kuuza maeneo yetu katika maziwa kama vile Viktoria, Tanganyika, Nyasa. Na hata maziwa madogo kama Rukwa, Manyara, Eyasi na Nakuru.
 
Kwa ufupi tu Pascal Mayalla ni kwamba serikali imeshindwa kusimamia sehemu nyingi sana kwa mfano wizara ya Elimu. Je, kuna mtoto wa waziri anasoma shule ya Serikali?

Kama viongozi wanajua kabisa kwamba wameshindwa kusimamia Elimu kwa nini wizara ya Elimu isibinafisishwe ili kuleta ufanisi. Shule nying za serikali ufaulu ni duni mno tena sana.

Kama suala la ubinafisishaji lina tija kiasi hicho kwa nini serikali yote isibinafisishwe?

Hii serikali kweli inamnufaisha mwananchi wa kawaida anayekatwa TOZO au inawanufaisha viongozi tu. Na kibaya zaidi hata rasilimali za asili zinazowasaidia wananchi wa kawaida kama NGORONGORO wanaziuza ili waendelee kuishi maisha ya peponi hapa duniani.
Je, Mwananchi ananufaika na nini na hii serikali? Huduma za serikali ni mbovu mno tena sana.
 
Haijapita hata miaka 5 toka tumetoka kwenye itikadi za uzalendo, mabeberu wabaya, na kuimba nyimbo za kujiamini na tunaweza. Na pengine baadhi yetu tulishiriki kubwagiza hayo. Leo yameshakuwa haya.

Hivi tuna fikra huru kweli kwenye jamii yetu ama hata free thinking tukubali imetushinda tuwaachie wengine?
 
Sema ccm awawezi waachie vyama vingine waongoze nchi. Bandari inakazi gani kuendesha?

Maji yanafanyiwa services gani? Je yangekuwa yanapakwa rangi ingekuwaje? hapa shida ni ccm imechoka tuitoe kwanguvu madarani.
 
Sasa yakibinafisishwa unadhani itasaidia nini,Mashirika mangapi yamebinafisishwa na Mkapa Leo yapo wapi??????????
Yote yaorodheshwe kwenye soko la hisa ili wananchi tununue hisa tuyamiliki, ili tusimamie kiasi cha hisa tulizo nunua. Serikali inayotokana na watu kujimilikisha hisa zote kwa asilimia mia ndio mwanzo wa mipango ovu ya ubadhirifu.
 
Serikali haikuwa kunufaika na ubinafsishaji. Mashirika mengi yalikufa kabisa, mengi tukaja kushtuka yapo hoi trc, tanesco, atcl, ttcl
 
Hata serikali hatuwezi kuiendesha; tutafuta watu wengine watusadie.

Juzi nilikuwa naangalia documentary ya maendeleo ya Singapore, sikuona walipokodisha sehemu yoyote ya nchi yao na walikuwa maskini kuliko sisi wakati tunapata Uhuru.

Watanzania tunasumbuliwa sana na mediocracy, kila mara viongozi hawajiamini na huwa wanajiwekea low expectations tu. Miaka takriban ishirini tu iliyopita mashirika yetu mengi (mfano ATCL, TRC) yalibinafsishwa kwa madai ya kuleta ufanisi, yakafa yote na wala nchi haikupata faida yoyote ikabidi Magufuli ayaanzishe upya. Leo hii mediocracy inataka kuturudisha tena huko huko.

China ina mashirika mengi sana ya serikali, lakini mbona yenyewe hayafi? Mtu akipewa shirika akshindwa kuperform anavikwa kitanzi tu, siyo kubembelezana.
 
Natamani liwe bunge kwanza tusaidiwe.
 
Paschal toka mwaka 1961 mpaka leo hatujiwezi kusimamia bandari, raslimali kama gesi,dhahabu,mafuta n.k.,tumeshindwa kusimamia wenyewe viwanda, mbuga zetu na mashirika yetu mengi tu?? Kuna haja ya kuwa na serikali sasa? Ni kama nchi nchi ni " state of nature" Masikini Tanzania🇹🇿🤔🤔🤔🤔!!!
 
Paskali, kusaidiwa siyo jambo baya, lakini ili usiingie mkenge zaidi lazima ujitathmini ulikwama wapi. Bila tathmini ya kina hata unachokitaka katika huo usaidizi hakitatimia. Jee muundo na Uendeshaji wa mashirika ya umma uko je? Tunajua vigezo vya teuzi za watendaji wakuu unaofanywa na serekali bila ushindanishi wowote? Je hao wateule wana ubavu wa kusema hapana kwa watendaji wakuu wa serikali bila kutumbuliwa? Nachelea kusema bila kujitathmini kwa kina hata wizara zafaa kubinafsishwa.
 
Naunga mkojo hoja naomba mpaka mke wako hauwezi kummiliki pia naomba nije kukusaidia kumla
 
.... kwa maoni yangu, baada ya Bandari, hata ATCL peke yetu hatuwezi, lazima tongue ubia!. Tukija kwenye SGR ndio kabisa!
Tutashindwa kujiendesha kwa sababu, mapato yetu kwa asilimia kubwa yako kwenye sarafu ya Tsh. wakati gharama za matengenezo (maintenance cost) ziko kwenye sarafu ya kigeni; sasa utatumiaje fedha za kigeni ambazo hukuzizalisha? Hii ndio kudidimiza uchumi pamoja na kupoteza fedha za kigeni zilizotokana na sekta zingine mfano utalii na madini.
Uwekezaji au ubia kwa asilimia kubwa unalenga kuongeza zaidi fedha za kigeni, ambazo kwa sasa zinahitajika kwa hali na mali.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…