Watanzania tujiulize: Ikiwa sisi ndiyo wenye mali, nini kinatukimbiza nje kutafuta wa kuja kuzila (eti kuwekeza)?

Hakuna anayekulazimisha kumpenda JPM ila JPM atakumbukwa na mambo na uwezo wake wa kazi na wala sina chuki na mama nipende nisipende ndo Rais wangu. Nitafurahi zaidi kwa Rais wangu akiwa creative wa mambo sio kutegemea wawekezaji sanaa hawana tija cha msinge akupe tupate mitaji,akusanye kodi bila kuangalia sura ya m2 na kusimamia rasilimali zetu kama chanzo cha mapato.Hakuna mwekezaji atakayeleta viwanda Africa sahau Wataleta low scale industry.sisi ni wazalishaji wa mali ghafi kwa ajili ya viwanda vyao huko kwako na ndo yupigwa pin hapo hatutoki.Maana wakileta viwanda Africa maana watauwa viwanda vyao kwa kukosa mali ghafi Je nani? Anakubali kuuwa viwanda vyao na kuwanyima ajira watu wao kwa ajili ya africa?.let us think broadly
 
Kwanza Tanzania hatuna rasilimali za thamani kama tunavyoaminishana utasikia eti tuna mito, mabwawa, ardhi, madini, wanyama pori, maziwa ni rasilimali sawa ila hazina thamani kama tunavyoaminishana.
Afadhali utindio wa ubongo, utindio wa mawazo ni hatari kwa Taifa lelote
 
Hizo Nchi zote ulizozitaja hawakujenga nguvu zao za uchumi kwa wawekezaji, bali kwa nguvu Mtu. Ujinga ni akili pia. wacha hizo
 
Acha ushamba.
Kama hata uwekezaji hujui kalime ungojee mvua.
 
Ninyi watu ujinga umewatawala.
Tembea vijiweni uone hao vijana wanavyosubiri manna itelemke toka mbinguni.
 
Kuna ukweli na unachokisema.
Magenge ya CCM, yameharibu sana.
 
Huo ni uwekezaji wa ndani hata sisi tunatakiwa tuwe ivo.lakini nakumbuka kipindi cha gesi wawekezaji wa ndani walinyimwa vitalu na wengine kukejeliwa kuwa hawana hela yakuwekeza kwenye gesi na muhongo kipindi kile.Hakuna kampuni kubwa huku italetwa kwa ajili ya uwekezaji Afrika sahau tutaletewa low scale industrie kama viwanda vya maji,biskuti,pipi na kadhalika ambavyo hata sisi bakhresa anavyo.ubaguzi upo china wafrika wote wametengewa soko lao kwazuuu ambapo bidhaa nyingi zinazalishwa na viwanda vidogo huna uwezo wa kwenda kufunga mzigo hongkong utaaza wapi? Na utamuuzia nani?.its special for uropean only
 
Umeshawahi kufikiria barter trade? Panua mawazo ya kufikiri.
 
Ardhi ya Tanzania peke yake ni rasimali ya thamani sana ambayo ingeweza kutotoa kwenye umaskini kabisa kama tungekuwa tunajitambua vizuri. Tanzania ni eneo ambalo unaweza kuzalisha mazao ya aina yote ya dunia hii na kwa kiwango cha kutolesheleza ndani ya nchi na kubaki kuuza nje ya nchi.
Kwanza Tanzania hatuna rasilimali za thamani kama tunavyoaminishana utasikia eti tuna mito, mabwawa, ardhi, madini, wanyama pori, maziwa ni rasilimali sawa ila hazina thamani kama tunavyoaminishana.
 
Hata Urusi na Marekani wanahitaji wawekezaji wa nje. Mataifa yanategemeana na kushirikiana kama wewe unavyotegemea ndizi za wakulima wa Mgeta, Kinole na Kauzeni.
Acha uongo, Marekani haihitaji wawekezaji wa nje.
 
Umejaa fedheha na udhahiki. Jidu la mbambaai
Ina nifanya niamimi wewe sio Mwafrika wala Mtanzania. Ujinga ni akili pia.
Changia basi badala ya kuhemeka tu. You can gugu translate this.
 
Ungeelekeza swali lako kwa CCM, na sio kujumuisha Waafrika wote. Unachodai ni udhalilishaji.
 
Kwanza akili iliyotengeneza mkwamo ni nadra sana ikajikita kutatua mkwamo husika.
Piga picha hata kijijini kwenu pale, wasipokuja wageni na wengine wenye maono ya tofauti mtabaki vile vile miaka nenda rudi.

Sasa kama taifa inaonekana mmewekeza kuijenga ccm na kuimarisha taasisi ya urais na rais. Kiasi kwamba mnakosa fedha za kuwekeza kwenye mitaji, elimu, afya na teknolojia.

Uchumi wa kibebari unahitaji uwekezaji wa kibepari!

Ukitaka faida kwa kuwakamua watu wako wekeza peke yako.
Ukitaka maendeleo endelevu na manufaa kwa wengi ruhusu wawekezaji binafsi kutoka pande zote za dunia.
 
akili zetu ni ndogo kuanzia wanaojiita viongozi mpaka wanaoongozwa.
 
Hizo hizo low scale industries zinatoa ajira na kupunguza tatizo la ukosefu wa kazi. Punguza uoga wa wageni mkuu, dunia tunayoishi ni lazima ujichanganye, huwezi kukwepa kujumuika pamoja na watu mbali mbali.
 
Haiwezekani rais akamsikiliza kila mtu, litakuwa ni soko kama la Kariakoo. Kila mjuaji akiwa anasikilizwa hiyo sio nchi tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…