Watanzania tujiulize: Ikiwa sisi ndiyo wenye mali, nini kinatukimbiza nje kutafuta wa kuja kuzila (eti kuwekeza)?

Watanzania tujiulize: Ikiwa sisi ndiyo wenye mali, nini kinatukimbiza nje kutafuta wa kuja kuzila (eti kuwekeza)?

Mkuu usimfananishe Samia na JPM, kila rais anayo haki ya kupita njia anazoona zinaifaa Tanzania. Kipaji alichokuwa nacho JPM Samia hana.

Kipaji alichonacho Samia JPM hana, hivyo msitake kulazimisha hisia zenu za kumpenda JPM ndizo hizo hizo zimeongoze Samia, mnatwanga maji kwenye kinu, mnapoteza muda.
Hakuna anayekulazimisha kumpenda JPM ila JPM atakumbukwa na mambo na uwezo wake wa kazi na wala sina chuki na mama nipende nisipende ndo Rais wangu. Nitafurahi zaidi kwa Rais wangu akiwa creative wa mambo sio kutegemea wawekezaji sanaa hawana tija cha msinge akupe tupate mitaji,akusanye kodi bila kuangalia sura ya m2 na kusimamia rasilimali zetu kama chanzo cha mapato.Hakuna mwekezaji atakayeleta viwanda Africa sahau Wataleta low scale industry.sisi ni wazalishaji wa mali ghafi kwa ajili ya viwanda vyao huko kwako na ndo yupigwa pin hapo hatutoki.Maana wakileta viwanda Africa maana watauwa viwanda vyao kwa kukosa mali ghafi Je nani? Anakubali kuuwa viwanda vyao na kuwanyima ajira watu wao kwa ajili ya africa?.let us think broadly
 
Kwanza Tanzania hatuna rasilimali za thamani kama tunavyoaminishana utasikia eti tuna mito, mabwawa, ardhi, madini, wanyama pori, maziwa ni rasilimali sawa ila hazina thamani kama tunavyoaminishana.
Afadhali utindio wa ubongo, utindio wa mawazo ni hatari kwa Taifa lelote
 
Tunakimbizana na maisha bwashee. Inawezekana we umesukumwa na ubinafsi tu kuandika haya lakini kumbuka watanzania Ni wengi maskini wanatafuta ajira. Laiti ajira au serikali ingekuwa na uwezo wa ku accommodate watanzani wote hakuna haja ya uwekezaji kutoka nje lakini ujue hata marekani ndani kwao Kuna wawekezaji wengi kutoka china, urusi n.k. Hivyo siku nyingine ficha ujinga wako
Hizo Nchi zote ulizozitaja hawakujenga nguvu zao za uchumi kwa wawekezaji, bali kwa nguvu Mtu. Ujinga ni akili pia. wacha hizo
 
Watanzania wenzangu, kuna kitu hakiko sawa!

Tutachanganyiwa lugha zote kuwa tunafungua nchi kumbe kuna hila ndani yake.

Sikubaliani kabisa viongozi kuzunguka dunia nzima kuomba pesa na uwekezaji.
Tunajidhalilisha!

Tuna bunge, Mawaziri, Wasomi, Wanasiasa, Wafanyabiashara maarufu nk,tumeshindwa kutulia na kukipanga hata iwe miaka 100 ijayo tukaijenga nchi yetu wenyewe? Hiyo haraka ni ya nini?

Wazee wetu kina Warioba, Msekwa, Malecela, Msuya nk niwaulize, mmekubali wajukuu zenu na elimu zao kuwa manamba wa Wazungu? Ndivyo hivyo Mwl. Nyerere aliwausia? Vijana,wajukuu zenu serikali iliwasomesha hadi vyuo vikuu ili wawe ombaomba duniani? Au waendesha bodaboda tuu na siyo kusimamia rasilimali zetu?

Ni kwa nini kila Rais aingiapo tunaruhusu alete mambo yake mapya na siyo kuendeleza ya mtangulizi au yaliyoasisiwa na nyie wazee wetu?

Mwl. Nyerere alituachia rasilimali tuzitumie kujiletea maendeleo au kuzinadia duniani?

Tujitizame.
Acha ushamba.
Kama hata uwekezaji hujui kalime ungojee mvua.
 
Tumezuia "Vipaji" tunaenda kuvitafuta nje, hivyo siyo vyetu!!!! Tusijidanganye. Viongozi wanaokotezana kindugu wanadanganyana kutafuta" mjomba feki" kuwa atawasaidia, huyo mjomba ni mjinga? Hatusomi Historia? China,Vietnam,Indonesia,Malaysia,Brazil kwa uchache waliwezaje? Vijana wenye uelewa wapo, tujenge maono ya mbele tuwawezeshe kwanza Hawa. " The time is coming when all stupid minds will be uprooted,and the facts open " Haiwezekani Wazazi wetu watuachie mali tutapanye kwa kukosa maarifa! Hilo nalikataa.
Ninyi watu ujinga umewatawala.
Tembea vijiweni uone hao vijana wanavyosubiri manna itelemke toka mbinguni.
 
Kujisahihisha ni muhimu la sivyo ni kusubili aibu. CCM inafanya makosa makubwa sana kwa kuendeshwa na serikali na kufanya kazi ya chama kuonekana rahisi sana. Serikalini watumishi hawaaminiki maana na wenyewe wamekandamizwa na mfuma mbovu pamoja na masilahi kiduchu.

Tanzania ina kila kitu ikiwemo mitaji ya kutosha tatizo viongozi wakuu hawajaamua au hawajui la kufanya. Muda ni sasa visingizio hatutaki amkeni tuanze kijenga nchi aibu ya umaskini jamani inatosha.
Kuna ukweli na unachokisema.
Magenge ya CCM, yameharibu sana.
 
"uomba pesa na uwekezaji" Unapotosha pesa za uwekezaji haziombwi kwasababu sio za serikali. Serikali inahimiza uwekezaji na hii inatokea kila mahali. Huku nje mfano hapa USA hata miji na majimbo yanafanya hivyo hapa Texas Governor wetu anaenda California kujaribu kuwashawishi wawekezaji waje hapa.
Huo ni uwekezaji wa ndani hata sisi tunatakiwa tuwe ivo.lakini nakumbuka kipindi cha gesi wawekezaji wa ndani walinyimwa vitalu na wengine kukejeliwa kuwa hawana hela yakuwekeza kwenye gesi na muhongo kipindi kile.Hakuna kampuni kubwa huku italetwa kwa ajili ya uwekezaji Afrika sahau tutaletewa low scale industrie kama viwanda vya maji,biskuti,pipi na kadhalika ambavyo hata sisi bakhresa anavyo.ubaguzi upo china wafrika wote wametengewa soko lao kwazuuu ambapo bidhaa nyingi zinazalishwa na viwanda vidogo huna uwezo wa kwenda kufunga mzigo hongkong utaaza wapi? Na utamuuzia nani?.its special for uropean only
 
Hebu na wewe jiulize jambo moja tu:-

Assume leo hii dunia YOTE inasusia Dhahabu na Tanzanite kutoka Tanzania na bidhaa zake. Pamoja na hayo, wewe ndo unakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Je, kama taifa, dhahabu na tanzanite yetu tutaitumia kwa matumizi yapi?
Umeshawahi kufikiria barter trade? Panua mawazo ya kufikiri.
 
Ardhi ya Tanzania peke yake ni rasimali ya thamani sana ambayo ingeweza kutotoa kwenye umaskini kabisa kama tungekuwa tunajitambua vizuri. Tanzania ni eneo ambalo unaweza kuzalisha mazao ya aina yote ya dunia hii na kwa kiwango cha kutolesheleza ndani ya nchi na kubaki kuuza nje ya nchi.
Kwanza Tanzania hatuna rasilimali za thamani kama tunavyoaminishana utasikia eti tuna mito, mabwawa, ardhi, madini, wanyama pori, maziwa ni rasilimali sawa ila hazina thamani kama tunavyoaminishana.
 
Hata Urusi na Marekani wanahitaji wawekezaji wa nje. Mataifa yanategemeana na kushirikiana kama wewe unavyotegemea ndizi za wakulima wa Mgeta, Kinole na Kauzeni.
Acha uongo, Marekani haihitaji wawekezaji wa nje.
 
Umejaa fedheha na udhahiki. Jidu la mbambaai
Ina nifanya niamimi wewe sio Mwafrika wala Mtanzania. Ujinga ni akili pia.
Changia basi badala ya kuhemeka tu. You can gugu translate this.
 
Hizi ndio akili za waafrika, anaamini hawezi kuwekaza na wala hawa hawezi pata mtaji, hivi akili wao walitoa wapi hao wazungu mnaoenda kuomba,? Kama ni technology hawakuiokota, walisoma, maanake elimu Bora ndio umewasaidia kupata technology, nyie elimu yenu ikoje? Yani huwa hatuwezi kuona mambo zaidi ya urefu wa pua.

Basi someni historia ya nchi zingine waliwezaje? Singapore waliwezaje na ni kisiwa? Ndio nchi yenye watu wenye IQ kubwa duniani,
Ungeelekeza swali lako kwa CCM, na sio kujumuisha Waafrika wote. Unachodai ni udhalilishaji.
 
Kwanza akili iliyotengeneza mkwamo ni nadra sana ikajikita kutatua mkwamo husika.
Piga picha hata kijijini kwenu pale, wasipokuja wageni na wengine wenye maono ya tofauti mtabaki vile vile miaka nenda rudi.

Sasa kama taifa inaonekana mmewekeza kuijenga ccm na kuimarisha taasisi ya urais na rais. Kiasi kwamba mnakosa fedha za kuwekeza kwenye mitaji, elimu, afya na teknolojia.

Uchumi wa kibebari unahitaji uwekezaji wa kibepari!

Ukitaka faida kwa kuwakamua watu wako wekeza peke yako.
Ukitaka maendeleo endelevu na manufaa kwa wengi ruhusu wawekezaji binafsi kutoka pande zote za dunia.
 
akili zetu ni ndogo kuanzia wanaojiita viongozi mpaka wanaoongozwa.
 
Hakuna anayekulazimisha kumpenda JPM ila JPM atakumbukwa na mambo na uwezo wake wa kazi na wala sina chuki na mama nipende nisipende ndo Rais wangu. Nitafurahi zaidi kwa Rais wangu akiwa creative wa mambo sio kutegemea wawekezaji sanaa hawana tija cha msinge akupe tupate mitaji,akusanye kodi bila kuangalia sura ya m2 na kusimamia rasilimali zetu kama chanzo cha mapato.Hakuna mwekezaji atakayeleta viwanda Africa sahau Wataleta low scale industry.sisi ni wazalishaji wa mali ghafi kwa ajili ya viwanda vyao huko kwako na ndo yupigwa pin hapo hatutoki.Maana wakileta viwanda Africa maana watauwa viwanda vyao kwa kukosa mali ghafi Je nani? Anakubali kuuwa viwanda vyao na kuwanyima ajira watu wao kwa ajili ya africa?.let us think broadly
Hizo hizo low scale industries zinatoa ajira na kupunguza tatizo la ukosefu wa kazi. Punguza uoga wa wageni mkuu, dunia tunayoishi ni lazima ujichanganye, huwezi kukwepa kujumuika pamoja na watu mbali mbali.
 
Hapo ndio kosa la sisi kuwa hapa tulipo...., No one is clever / bright than all of us...., Kumpa mamlaka mtu mmoja ndio achague nini cha kufanya au njia gani za kupita ni matumizi mabaya ya Human Resources..., Wadau na Wataalamu inabidi wachague njia Rais ni kusimamia tu....
Haiwezekani rais akamsikiliza kila mtu, litakuwa ni soko kama la Kariakoo. Kila mjuaji akiwa anasikilizwa hiyo sio nchi tena.
 
Back
Top Bottom