Tetesi: Watanzania tukatae Uwanja wa KIA kupewa Oman

Wacha uzushi wewe uwanja wa ndege hauwezi kuuzwa ni uhaini kufanya hivyo
 
Watauzaje kipande cha ardhi ndani ya Tz.
Jeshi letu limepewa kazi ya kufanya usafi badala ya kulinda mali za nchi
 
Watanzania wenzangu tukatae sasa kila rasilimali za nchi hii kupewa Waarabu. KIA ilijengwa na Mwalimu Nyerere kwa maono makubwa iweje leo apewe Oman? Kuna watu wanamtumia Rais vibaya kujinufaisha na mikataba hii kama ile ya DP.
Jana kulikuwa na uzi unasema kuna viongozi wanunua majumba Dubai kwa Bil 25 na wengine Masaki kwa Bil 6
 
Kama wenyewe tumeshindwa kuuendesha kwa faida kwanini wasipewe wanaoweza tukapata faida?

Mnaleta ya DP World, sasa hivi tunaona bandari inaingiza faida kubwa serikalini, mizigo na meli zimeongezeka kuwapa tugati 4 DP World. Tena nashauri wapewe bandari yote kuiendesha.


Hiyo KIA wapewe haraka sana waOman waiendeshe kama bado hawajapewa.

Kwanza hao utakuta wanaokuja kufanya kazi wote wana nasaba kubwa za Kitanzania.
 
Ujilaumu wewe kwa kuichagua ccm
 
watanzania mnachojuwa sahvi ni kukatika uno misomisondo na maapiqno na maumbea tu

Ova
 
Kwa maoni yako ni kwamba nchi haina uwezo wa kuendesha viwanja hivyo! Yaani,hata akili ya kuajili watu wa kusaidizana na wa ndani kuviendesha,haipo!! Mwisho wa siku kuna watu wenu mtatoa kwa sababu kuwashughulikia mmeshindwa. Mnaogopaga nini kujifunza kwa waliopatia? Sisi ndo sisi, sisi tunajua,sisi tunaweza,sisi tutapatamo nini, ndo inayowaponza
 
Mbona KIA ina MOU muda tu na hao jamaa kama sikosei mwaka jana au hii ni mpya? [emoji28] same as shirika la posta.
 
Dah!! Hivi nyie wenzetu katika Imani mna akili Gani? Dah
Mjibu kwanza ndio umulizie akili zake, mbona kauliza swali la msingi tu?

Tatizo lenu mnakimbia ukweli
Kisa udini, halafu nyie nyie ndio mnaita wenzenu wadini

Jibu swali lake, je ingekuwa wazungu ni sawa tu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…