Watanzania tunapaswa kuambiwa na kujua ukweli kwamba Gesi inayochimbwa Mtwara si yetu

Mkuu Kilatha , unaposema hakuna sheria inayosema Tanzania itapata 16%, uwe umejiridhisha kuwa wewe mwenyewe umeisoma hiyo sheria, na ukakuta hakuna sheria hiyo, ikitokea sheria hiyo ipo, wewe tukuiteje?. Sasa kabla sijaendelea na hili, naomba nikuulize swali dogo tuu na naomba unijibu kwa ukweli tuu, jee wewe Mkuu Kilatha , umeisoma sheria mpya ya madini, ukakuta hakuna sheria inayosema Tanzania itapata 16 % ?.
Hapa naomba nikupe ushauri wa bure, kwenye kujadili maslahi ya taifa, usilete personalities, leta hoja tuu, hakuna ubishi huyo uliyemtaja ni mbobezi mwenye Ph.D, ila amini nakuambia, mtu kuwa na Ph.D ya kwenye makaratasi ni tofauti kabisa na wenye experience, kwenye baadhi ya issues, darasa la saba anaweza kuwa mzuri kuliko Ph.D holder. Tembelea uzi huu, Je, Wanaoshangilia na Kupongeza Bajeti Wanajua Wanashangilia Nini? , Au Tunashangilia Ujinga?! . usome hoja zangu, kuhusu huyu Ph.D holder wako, kisha ujiulize hoja hizo zimewahi kujibiwa kipindi chake chote akiwa eneo hilo?.
P.
 
Kwani JPM alivyosema kwenye gesi hatuna chetu hukumuelewa? Unazani kwanini aliamua kuingia kwenye umeme wa Hydro? RIP Jembe
Ndugu haya mambo sio ya kumsifia fulani na kumponda mwingine huo ni unafiki. Kaa chini fanya upembuzi kwanza ujue gharama zinatumika kuzalisha umeme we gesi kama ni himilivu sio mziko kwa tafa usisikie ya kuambiwa mengine yanaweza kuwa chuki tu. Pia ukumbuke umeme wa maji pia una changamoto zake hivyo tunaitaji kuwa na vyanzo vingi vya kuzalisha umeme. Wengi wengependa kuona uelewa wako pingine una mawazo mazuri yanayoweza kulikomboa hili taifa una haki kama mwananchi. Sifa za mtu mmoja hazasaidii chochote
 
Siku GST wakianza kufanya physical exploration ndio nchii itaamka lakini kwa sasa tusikilizie kwanza.
 
Ni serikali ya CHAMA GANI ILIPITISHA MAUZO HAYA YA GESI YETU?
Mkuu mkulima gwakikolo , kuna maswali mengine, kuwauliza baadhi ya watu sio kuwatendea haki!.
Naomba usinionee bure!.
Swali hili ni kama uko na rafiki yako, anamjua baba yako, halafu mko mbele ya watu, kuna mlevi mmoja watu wanancheka kwa kuzidiwa na kilaji, halafu rafiki yako anaona kabisa huyo ni mzee wako, halafu anakuuliza wewe mbele ya ule umati wa watu, ati yule mlevi ni baba yake nani vile?.
Wewe utajibu?. Mswali mengine sio ya kujibiwa, swali hili ungeniuliza mimi enzi zangu zile za maswali kama haya
ndio ningekujibu.
P
 
Kwani JPM alivyosema kwenye gesi hatuna chetu hukumuelewa? Unazani kwanini aliamua kuingia kwenye umeme wa Hydro? RIP Jembe

Ndo hapo watu bado hawaelewi kwa nn mzee baba aliingia kwa namna ingine maana ayaie aliichungulia gas akashindwa masharti magumu ikiwa angevunja mkataba
 
Hapa tuwekane sawa nadhani elimu inahitajika. Kuna kitu kinaitwa PSA huu ndio mkataba unaoweka wazi na PSA hasa inaipa nchi power zaidi katika maisha ya mradi. Mwekezaji anawekeza kila kitu tuseme kaweka Billion 1 uzalishaji ukianza mwekezaji anaanza kuchukuwa asilimia 75% mfano na serikali inachukuwa 25% faida baada ya operating cost. Kila mwaka budget ya kampuni ambayo ndio operating cost inapitishwa na shareholders wote pamoja na serikali kwa kuwa inalipa hiyo 25% kupitia mauzo sasa kila miaka inavyokwenda kwa maana muwekezaji anakuwa ana recover cost ile % yake inashuka kwa mfano 70% to 30% na itaenda hivyo katika maisha ya PSA kama ni 20 au 25 years, dhumuni kubwa la PSA kwa mwekezaji kurudisha ile billion yake aliyowekeza na kupata faida sasa ikifika kipindi cost recovered ile PSA inakuwa katika miaka ya mwisho ya PSA serikali kupata 80% na muwekezaji 20% lakini kumbuka kabla ya kugawana faida serikali inachukuwa Tax inaweza kwa mujibu wa kisheria. PSA iki expire ule mradi unakuwa own by serikali 100%. Sasa nii juu ya serikali kusema labda sisi hatuna uwezo wa kuendesha mradi tunakupa kama operators tu ukampa 10% tu na wewe uka cover budget 100%. Kwa mfano mwepesi PSA ni kama wewe una kiwanha Kariakoo lakini huna uwezo wa kujenga. Kaja mtu kasema tuingie ubia hiyo ni PSA, mimi nitajenga gorofa kumi nitakupa gorofa 1 mimi 9 mkataba wa miaka 20 kila mwaka navyo rudisha gharama zangu utakuwa na 2 mimi 8 itakwenda ikifika 20 years muwekezaji ana moja wewe 9 hiyo ndio biashara ya mafuta na Gas. Tofauti kubwa na Oil na Gas ni Oil unauza miezi mitatu mbele na bei inabadilika kila siku ukija kwenye Gas unaingia mkataba wa kuuza kwa muda mrefu kwa client bei ya Gas haibadiliki haraka sana unaweza kuuza kwa mwaka bei ya chini kuliko soko sababu mikataba ya supply inakuwa ya muda mrefu. Nadhani hoja kuwa tumeibiwa mradi hauna faida sio kweli hapa ni PSA ikoje. Budget ya muwekezaji lazima serikali kama main shareholder kuipitisha sababu ni cost recovery au CAPEX yoyote lazima serikali wa approve sababu ni cost recovery. kikubwa uaminifi walioaminiwa na serikali vingenevyo wanaweza kuongeza budget na CAPEX mkakuta mnapigwa tu latika cost recovery, kumbuka cost recovery kabla ya Tax na kugawana profit.
 
mayalla tusipindishe pindishe ukwel, mm ni mwanachama na kipnz wa ccm kindakindaki ,lkn kwenye ukweli lazma niseme ukwel na nisimame kwenye ukweli pengine itasaidia kubust ubongo wa hawa watu tuliowapa dhamana ya kusmamia raslimali zetu ,gesi Niya watu wa nje , hatuna gesi pale,ingekuwa yetu umeme ungeshuka Bei kwa wananchi lkn wapi,gesi ipo kwetu hapo karbu mtwara ,mtungi kadogo 23000/= hizo Sheria mpya vp!? Tulijua kwa Sheria hizo Basi angalau ingesaidi Bei ya gas hapa nchini ingekuwa nafuu kwa watz lkn wapi !!,
 
Wapi nimesema wanachukua kila kitu wanachokikuta huko chini? Hata hivyo wachangiaji wengi wameeleza tena wengine wameeleza kiundani zaidi kuhusu hizo biashara katika maeneo mbalimbali huko duniani.
 
Kwa nini wapate exclusive rights ? Ukigundua una dhahabu kwenye shamba lako na huna uwezo wa kuichimba, utampa exclusive rights mtu anayeweza kuichimba?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23], oi naomba niku support kucheka mkuu, eti mbona kama wananchi wanachukulia fresh tu[emoji1787].
Mis education inafanya kazi, tatizo kubwa ni elimu, wananchi wengi hawajui hata serikali ni nn, ww umesoma ndo maana unaliona hilo, kumbuka hata ww ulivokua mdogo ulikua unaamini serikali ni kampuni binafsi inayosaidia watu.[emoji23]
Imagine ungekua hujaelimishwa
 

Halafu bado Kuna watu humu wanakuja na Mada eti Ni bora tutumie Umeme wa Gas,Eti Sijui tufufue palnts za Gas za Tanesco sijui Kinyerezi gani na gani wakati tunaongeza gharama sababu Gas tunaninunua na Tanesco anauziwa kama alivyosema Mtoa Mada!
[emoji3516][emoji41][emoji851][emoji30]
 
Kwa nini wapate exclusive rights ? Ukigundua una dhahabu kwenye shamba lako na huna uwezo wa kuichimba, utampa exclusive rights mtu anayeweza kuichimba?
Gharama za kufanya seismic studies hadi kugundua mafuta/gas sio cheap kabisa especially offshore, costs zinavuka $1 billion plus easily na unaweza fanya shughuli yote ukakuta reserve yenyewe not worth of commercial exploitation, wapo watu waliopoteza hizo hela ata Tanzania. Sio vitalu vyote vilivyofanyiwa exploration vimekutwa na reserve (ndio maana Prof Muhongo akasema watanzania wanamitaji ya hela za viwanda vya juice tu).

Exploration ni high risk ndio maana kampuni nyingi zinazofanya hizo shughuli either ni kutoka large oil companies zenye mitaji ya kuchezea au government sponsored huko kwao, sio sehemu ya kuingia kichwa kichwa kabisa nchi nyingi maskini aziwezi kuchukua hizo risk wanatafuta wengine wafanye hiyo shughuli.

Kwa minajili hiyo kampuni zinazochukua hizo risk wakikuta kuna reserve za kutosha wanakuwa rights pia za kurudisha mtaji na kufaidika pia kwa kazi yao ndio sababu ya kuwa na exclusive rights.
 
Nchi zote ipo ivyo kasoro chache mainly in the Middle East wakiongozwa na Saudi Arabia ndio oil is highly subsidised (but then they earn a lot in exports annually to meet their budgetary obligations) na ata wao walifikiria kupunguza subsidisation kipindi ambacho uchumi wa dunia uliporomoka.

Ukijaribu kuwa too low madhara yake yanakuwa kama Venezuela if you are not exporting, sisi atujaanza ku export gas bado na ata tukianza atuwezi kuwa Qatar au Russia, so lazima wauze bei iwe kiasi gani hiyo ni debate nyingine.
 
Madini yanayochimbwa kwingine kokote ni yenu?
 
Sina tatizo la wao kuwa na rights za kurudisha mitaji yao. Nina tatizo la wao kuwa na exclusive rights. Ina maana wenyewe wata dictate terms & conditions kwa nchi husika ni jinsi gani wanaweza kufaidika na matunda ya mali zao za asili. Na kwa nini iwe hivyo ? Gharama isiwe kigezo kwani ni hiari yao kuchimba au kuacha.
 
Aindolewe dalali TPDC Ili serikali kupitia Tanesco wanunue moja kwa moja kutoka kwa makampuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…