Watanzania tunazidi kustarabika. Siku hizi ni ngumu sana kukuta watu wakipigana kama zamani, Tujipe hongera

Ishara nyingine ya ustaarabu kwa Watanzania ni kuendelea kuwepo taa za barabarani zile zinazotumia sola. Zile taa kuna maeneo mwaka wa pili sasa zimefungwa na hazijaibiwa.

Kuna sehemu mlingoti wa hizo taa ulianguka kutokana na maji kuchimba karibu na mlingoti lakini ile taa na mlingoti ilibaki imeinama kwa siku kadhaa mpaka wakaja wahusika.

Miaka ya nyuma watu wangeziiba sana zile taa.

Pia, hata wizi wa vibao vya alama za barabarani umepungua sana. Zamani vilikuwa vinaibiwa na unakuta watu wanafanya mwichi wa kutwangia kwenye kinu.

Kipengele kimojawapo ambacho bado Watanzania hatujastaarabika ni kipengele cha kutunza na usafi wa mazingira. Unakuta mtu anaishi nyumba imezungukwa na manyasi. Wananchi hutapalilii njia za kuelekea majumbani kwetu, nyasi kibao.
 
Kweli wewe ni mfuasi wa Andrew Tate

Ila kiuhalisia, nikikutana na mtu ambaye kila kitu anakimbilia ngumi, huwa namuona yupo weak kihisia na kiakili kwa sababu mtu anaeona misuli kama solution zaidi bhasi akili yake imekosa matumizi

Kingine siku hizi maisha ni magumu sana na hii imeifanya nguvu kuwa ni pesa. Kwa hiyo haijalishi una misuli au unaweza kupigana kiasi gani ila kama hauna pesa, vyote vinakuwa useless maana hakuna atakaekuheshimu wala kukuogopa maana yoyote mwenye pesa anaweza kukuadabisha anavyotaka na usifanye lolote
 

True, na zamani kutumia nguvu ilikuwa sifa sana. Kuwa mtoto wa kiume lazma ufyatue tofali, ubebe zege, ulime na ufuge "nchi ya wakulima" etc ili utoboe

Lakini maisha yanavyoenda race, hizo kazi ni za hand to mouth tena kwa sasa mtu akizifanya anadharaulika maana ni za kimaskini. Leo hii mtu haangalii unajitesaje ila unafanikiwaje, ndio maana ushenzini kwetu dereva boda au fundi AC anaheshimika maana at least ana pesa za kuishi vizuri ila mbeba tofali au kuli anaonekana hopeless maana pesa hana

Kiufupi, hizo muscles utishie watu ukiwa na pesa ndio utasifiwa uanaume maana
tushaanza kutoka kwenye maisha ya ujamaa ya kuangaliana kiubinadamu kwenda kwenye kuangaliana kimaslahi. Sasa mtu una muscles ila hela huna na badi unatishia watu ili uogopwe. Hapo Si unaonekana umechanganywa na ugumu wa maisha mkuu😁
 
Ni maendeleo ya jamii kustaarabika

🔹 Kuna kipindi Cha zamani ( according to philosophers walivyokuwa wanaelezea theories of social contract) binaadamu wa walikuwa kama wanyama. Wakikutana tuu wansaanza kushambuliana for no reasons

🔹Kwa bongo ujinga huu na tuzishukiru shule za kata unaanza kuondoka, ila umebaki ule wa vijana kutembea na fimbo kuchapa watu ambao wanakula hadhatani kwenye mwezi . Hii insturudisha nyuma katika kuwa jamii ya kistaarabu
 
Lakini kumbuka hata kwenye huo wimbo. Tommy alipoona dharau zimezidi hadi kwake kwa mke wake. ALIWAPASUA wale vijana hawakuamka, na hawatakaa waamini!! Na akaconclude 'sometimes you got to fight when you are a man'

Lakini hiyo ni last resort, pale akili za wahusika wote zimeshindwa kufanya kazi kikamilifu. Akili kwanza mtu wangu, akili tu.
 
Ngoja nichangie kidogo.

Nina bahati sana kuzaliwa uswahilini Mabibo na kuishi zama za miaka ya 1970-1990.

Kwanza Mabibo nzima kulikuwa hakuna kituo hata kimoja cha polisi. Vituo vya polisi vilikuwa Buguruni, Urafiki na Magomeni.

Na ikumbukwe kuwa mwaka 1972 serikali ilifuta serikali za mitaa na nafasi yake ikachukuliwa na TANU baadae CCM. Na hapo ndipo ule msemo wa "chama kushika hatamu" ulipoibukia.

Kwa Ivo nakumbuka "utemi" ndiyo ulikuwa ama ulinzi wako au Silaha dhidi ya wengine.

Maana kama huna ubavu basi nani atakutetea. Na Kuna wakati wababe wala hawakuwa watu wahalifu bali watuliza dhoruba za mtaa.

Kwa ivo mapigano mengi yalihusu kujitetea dhidi ya uonevu, ulevi, bidhaa za magendo, kugombania wanawake na kuonesha umiliki wa eneo.

Maisha Yale yalikuwa na misisimko yake pia. Mjumbe wa nyumba kumi kumi alikuwa ni mtu mkubwa kweli kweli.
 
Mkipigana hadharani wote wawilinakwenda kulala gerezani, siku inayofuata mahakamani.
 
Zamani ilikuwa lazima ujipambanie mwenyewe ndo upate haki yako. Ndio maana mambo ya watu kujichukulia hatua yalikuwepo sana. Mifumo ya utoaji haki haikuwa imara kama ya leo.

Bila ubabe ilikuwa hautoboi popote hata shuleni ilikuwa ukiripoti tu lazima upelekwe puta sana na wanafunzi wenzako unaowakuta hapo.

Mke sijui mchepuko ukizingua anakula mbata za kufa mtu na hakuna kitu atafanya. Sasa jaribu kufanya hayo leo hii kama haujaishia kunyea ndoo.

Ukirudi toka jela unakuta nchi imepiga hatua kwa mbali, wale wa rika lako wameshakuacha mbali kimaisha.
 
Kwahio mmezipanga mtu mbike au sio😂? Vipi ulimchapa au kakugaragaza. Kiufupi dharau ndio chanzo cha nakoz konz
Ndio mwanangu paling mtu mbili puta mchanga tema mate vuka msitari
Ile sijakaa sawa Jamaa kwanza alinipa mbili za faster zenye ujazo kama kilo 50 hivi
Nikaona nyota 2 tatu me mfupi kidogo jamaa mrefu nikawa narudisha ngumi zngu zikawa hazina madhara kwake HAZIFIKI usoni
Na bado jamaa anarusha ngumi mfululizo sema kwakuwa kishawaka nikawa nakwepa na kuzipanchi
Nikasema sasa leo nitaahibika nikiangalia pembeni watu hawagombelezei wanatuangalia tu nikawaza nikimbie nikasema nitakuwa VERY COWARD mbele ya mama chanja mwanaume akimbii vitani na mama watoto NYOTA atanivua nyingi sana

Ikabidi sasa nifanye km nataka kumvaa ile ajaribu kunipush kumbe mm lengo langu kumkata mtama
Nikafanikiwa kwakuwa hakujiandaa
Nikamkalia juu na kumpelkea ngumi mfulilizo yaan mpk sasa mkono unauma kishezi nikaja kuvutwa kwa nguvu kutolewa juu wakati huo jamaa sijui hali yake ikoje sikutaka tena kuendelea kuwepo hapo tukasepa na WIFE
ila mpk sasa nina NUNDU kichwani yaan hata kutafuna vizuri siwezi upande wa kushoto
NGUMI zake kari sana zinaujazo haswa nusura anitengue taya

Lakini pamoja na yote nimefurahi nimechangansha mwili na kuweka mipaka ya HESHIMA mtaani
Wakati tupo hone ananikqnda NUNDU na barafu
Akawa anasema kumbe wewe ukikasilika ni mkorofi hvyo jamani pole MUME WANGU
Basi bana usiku wa jana nikapewa vitu hadimu sana ambavyo nilivimiss tangu enzi ya HONEYMOON
Hvyo pamoja na NUNDU lkini nimeonesha uanaume hvyo nimeongeza NYOTA nyingi kwa mama chanja
 
Kumbe ulikuwa na 1st Lady halafu ukataka kuchoraa😂!!! All in All ngumi nzuri kuzitazama tu ila sio wewe uwe unakandwa.
 
Naona mnakwepa kwepa tu kwa sasa vijana wana low testosterone ujasir wa kupigana hamna
 
Kupigana mjini pesa then unajiona mjinga.
Ukitaka kupigana andaa pesa ya kumlipa unaempiga pili pesa ya police ili kumaliza kesi.
Angalau uwe na laki tatu kwenda juu
 
Sure
 
Dunia imestaarabika saivi kila mtu anapigana na maisha yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…