Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Wewe unaamini hivi vyombo vyetu vya uchunguzi na kutoa haki vinaweza kutenda haki kwa wakati kwa mtu mkubwa mwandamizi bila kushinikiwa au kusukumwa?Una uhakika gani kama ni kweli?. Wacha tusubiri vyombo vya kutoa haki vifanye kazi yake ndipo tuweze kupanua midomo yetu. Unajua wakati mwingine uongo huwa unapanda lift na ukweli huwa unapanda ngazi. Lakini taratibu utafika roof top. Tumeambiwa hawa wamama wana bifu tangu zamani. Na inasemekana wako na bifu za kiitikadi pia. So lolote linaweza kuwa kweli kwa maana ya kumzushia gekul au gekul kufanya unyama. Njia pekee ni kusubiri court watu wapeleke ushahidi na haki itatolewa.
Kama wewe unaamini Gekul huenda anaonewa au kusingiziwa basi bakia na mtizamo huo. Yaani mpaka leo, hujaona ufedhuli wa Gekul?
Lakini kwa sisi wananchi kupitia mahakama zetu za kijamii tayari tumeshamtia hatiani Gekul kwa tuhuma zote zinazomkabili, na sasa tunakwenda kutoa hukumu ya kijamii, na kama anahisi ameonewa basi aje kukata rufaa kwenye jamii ili tumsikilize upya.