Watanzania tususie biashara za Pauline Gekul mpaka aombe msamaha

Watanzania tususie biashara za Pauline Gekul mpaka aombe msamaha

Business entity, the owner of the business and the business are independent, owner anaweza akawa mchawi ila biashara ikawa ni takatifu, au mwenye biashara anaweza kuwa mtu safi toka moyoni ila biashara ni ya kuzimu
 
WanaJF,



Nashauri kuanzia leo tususie biashara zote anazofanya huyu mbunge wa Babati kwa kitendo chake cha unyanyasaji. Naomba anayezifahamu aweke majina yake hapa.



Tuanze na hiyo hoteli inaitwa Palii sijui nini.



Hakuna kufanya biashara na muuaji au wanaomsapoti mpaka akili iwakae sawa.



Nimemaliza


Ungeleta similar post kwa lake oil na home shopping centre ingependeza
 
Lakini kumbuka hajatumwa kufanya uovu alioufanya. Ni vyema awajibishwe.

Kwenye biashara,kumbuka,iwe familia yake au wanaofanya kazi kwake,wanazitegemea hizo hizo. Na kwa vyovyote wateja wasipopatikana, kuna watu kutunza familia zao itakuwa shida. Bora ungeshauli njia sahihi ya yeye kuwajibishwa
 
WanaJF,

Nashauri kuanzia leo tususie biashara zote anazofanya huyu mbunge wa Babati kwa kitendo chake cha unyanyasaji. Naomba anayezifahamu aweke majina yake hapa.

Tuanze na hiyo hoteli inaitwa Palii sijui nini.

Hakuna kufanya biashara na muuaji au wanaomsapoti mpaka akili iwakae sawa.

Nimemaliza
Mkuu kamuua nani? Kamnyanyasa nani kwa ushahidi upi? Tulia, tafakari halafu ndio uandike.

Kila mtu anatuhumiwa, hata wewe unaweza kutuhumiwa wakati wowote! Tuhuma sio hatia.

Mkuu watanzania wengi hufurahia maumivu ya watu wengine haswa wenye hadhi, nafasi au ukwasi ndani ya jamii.
 
Wewe unaamini hivi vyombo vyetu vya uchunguzi na kutoa haki vinaweza kutenda haki kwa wakati kwa mtu mkubwa mwandamizi bila kushinikiwa au kusukumwa?

Kama wewe unaamini Gekul huenda anaonewa au kusingiziwa basi bakia na mtizamo huo. Yaani mpaka leo, hujaona ufedhuli wa Gekul?

Lakini kwa sisi wananchi kupitia mahakama zetu za kijamii tayari tumeshamtia hatiani Gekul kwa tuhuma zote zinazomkabili, na sasa tunakwenda kutoa hukumu ya kijamii, na kama anahisi ameonewa basi aje kukata rufaa kwenye jamii ili tumsikilize upya.
Mkuu huko ni kujifurahisha kama kichaa anatembea njiani akicheka cheka.
 
Uko sawa. Ila, tangu utoto nimefunzwa kuwa kila kosa lina wajibu wake, kuanzia kuangaliwa jicho, kuonyeshwa kidole, kufinywa shavu, kwenda kujikatia kiboko n.k. Na yeye, kama kweli ametenda kosa basi anastahili awajibishwe kulingana na sheria zilizopo.
Watanzania tumejaa ujamaa mpaka kwenye mambo ya msingi yenye kuhitaji maamuzi ni ujamaa tu.

Sent from my 23021RAAEG using JamiiForums mobile app
 
Ccm imemtuma? Huyu si alikuwa chadema pia, sasa hapa nani ni Mwl wake?
Kwa sauti ya mdogo wake inayosambaa mtandaoni inasema chadema walikuwa wanaendesha kwa mapanga na marungu. Sasa hapo tuchukue kipi?
Kuna wana cdm na ccm waaminifu na kuna wana cdm na ccm walikokiwa wananunuliwa. Hapa ni roho ya mtu mwenyewe

Sidhani kama kususia ni wivu... Ususiaji pia huwa tunausisitiza kwenye mambo mengine mfano kampuni inanyanyasa watoto etc. kwa mazingira hayo sisi walaji tuna boycott huduma zinazotolewa ili kuonyesha solidarity na waathirika. Wewe ni mmoja wa beneficiaries wa biashara za Gekul kwa hiyo ndio maana umechanganyikiwa. Sasa unafikiri tunawezaje kuonyesha hasira zetu bila kususia biashara za muhusika tena ambazo zimemsababishia mwananchi matatizo?
Mkuu imethibitika wapi kuwa kafanya mbona unakamia kama Ulikuwepo! Tusubiri vyombo vya uchunguzi vifanye kazi na makahama itoe uamuzi wake ndio tuzungumze.
 
Aisee kuna kukosea na kuna kumtia mtu chupa Takoni, hiyo ni Gross Misconduct atalaaniwa mpaka Motoni huyu mama.
Mkuu inakuwa gross misconduct ikithibitika mahakamani. Until then bado ni tuhuma tu like any other.
 
Business entity, the owner of the business and the business are independent, owner anaweza akawa mchawi ila biashara ikawa ni takatifu, au mwenye biashara anaweza kuwa mtu safi toka moyoni ila biashara ni ya kuzimu
Hakuna kitu kama hiki
 
Hivi Mpka raisi wa Nchi, inamfikia na kuamua kumtumbua unafikiri bado Ni Tuhuma??? Unaijua Intelligensia Ya office ya Raisi ?? Raisi hakulupuki kashapewa data kuwa ni kweli....

Then kusingiziana huku ni kwetu kajamba Nani, ww unaweza msingizia Naibu waziri wa Sheria??
Mkuu hiyo ni assumptions yako of which uko entitled nayo. Kwa taarifa yako Rais kamtumbua kupisha uchunguzi.
 
Ndio amuingize mtu chupa mkundun(I)
Hebu akuingoze wewe au mtoto wako then ndio umsameheme.
Yaani vaa viatu vya dogo ya kwamba "Kuna mwanao Leo umemuacha mzima ila kurudi umemkuta kaingizwa chupa au wewe umeingizwa chupa"

THEN SAMEHE...

#YNWA
Mkuu hivi kwa mfano ikibainika kuwa ni uongo utakuja kumsafisha mtuhumiwa huku jukwaani?

The allegations could be true or not, so tusubiri uchunguzi ukamilike na uamuzi wa mahakama utoke then uzungumze ukiwa na ukweli.
 
Ungewekewa chupa hiyo wewe au kijana wako, mtu wako wa karibu nina uhakika maoni yako yangebadilika.

Ila sababu ni mtoto wa maskini, hujali unatetea maslahi ya chama zaidi kuliko ubinadamu.

Jamii iliyostaabika inapimwa jinsi inavyotenda haki hata, hasa kwa maskini, watoto, wajane, watu wa chini.
Haki anatakiwa atendewe yoyote pasipo kipaumbele kwa mtu yeyote.
 
Back
Top Bottom