Watanzania tususie biashara za Pauline Gekul mpaka aombe msamaha

Wewe unaamini hivi vyombo vyetu vya uchunguzi na kutoa haki vinaweza kutenda haki kwa wakati kwa mtu mkubwa mwandamizi bila kushinikiwa au kusukumwa?

Kama wewe unaamini Gekul huenda anaonewa au kusingiziwa basi bakia na mtizamo huo. Yaani mpaka leo, hujaona ufedhuli wa Gekul?

Lakini kwa sisi wananchi kupitia mahakama zetu za kijamii tayari tumeshamtia hatiani Gekul kwa tuhuma zote zinazomkabili, na sasa tunakwenda kutoa hukumu ya kijamii, na kama anahisi ameonewa basi aje kukata rufaa kwenye jamii ili tumsikilize upya.
 
Bisshara ni bisshara na maisha binafsi ni tofauti na biashara
 
Msimamizi wa sheria anafanya unyama kwa mpiga kura? Haijawahi tokea. Sasa anasimamia nini? Lazima tususe. Hatutaki kumwongezea nguvu mtu mwenye roho ya uuaji?
Kama unadhani huyu ndo Mbunge wa Kwanza kufanya unyama utakuwa uko nyuma Sana Kwa Taarifa. Ninewahi kushuhudia Mpiga Kura amechomwa vidole na mgombea Ubunge wa CCM na hakufanywa chochote zaidi ya Mhanga kuwa mtuhumiwa kaiba bendera za Chama. Kama huwajui hawa waliojimilikisha nchi unaweza kudhani wema.
 
Umechunguza kwa kina na ukabaini sababu ya mh huyo kuwapa adhabu watumishi wake hao au unashauri tu kwa Sababu uns uwezo wa kuandika?
 
Umechunguza kwa kina na ukabaini sababu ya mh huyo kuwapa adhabu watumishi wake hao au unashauri tu kwa Sababu uns uwezo wa kuandika?
Hakuna mtu mwenye mamlaka ya kutoa adhabu ya kupiga au kumwingizia mfanyakazi wake chupa hata kama ameiba. Mahakama tu ndio inatoa adhabu. Na hili ndio maana kuna wizara ya sheria na katiba ambayo Gekul anaisimamia.
 
Kwa hiyo unashauri tuwe tunaacha haya mambo yaendelee tu?
 
Ni mshirikina haswa hizi mambo zitaisha tu
 
Mwacheni dada wa watu, ni nani ambae hajawahi kufanya makosa hapa duniani? Hakuna binadamu aliekamilika
Ungewekewa chupa hiyo wewe au kijana wako, mtu wako wa karibu nina uhakika maoni yako yangebadilika.

Ila sababu ni mtoto wa maskini, hujali unatetea maslahi ya chama zaidi kuliko ubinadamu.

Jamii iliyostarabika inapimwa jinsi inavyotenda haki hata, hasa kwa maskini, watoto, wajane, watu wa chini.
 
Sasa atakuomba Msamaha akiwa kizuizini ,Mahabusu
 
Wananchi ndio walio sababisha Jambo hilo kufikia hapo... Kina Martin Maria na wengine kule twitter (x) walipambana sana... Jana ni hao hao wananchi waligundua kuwa alikuwa na mpango wa kutorokea kenya kupitia holili... akakamatwa na polisi kwa msaada wa raia.

Watu wakivichoka vitendo vibaya automatically cha moto utakipata.
 
Tuhuma hazijathibitishwa mbona mnamhukumu kwa maneno? Kama tukio limekuwa staged unajuaje?
 
🤣 chezea waswahili wewe. Huwa wanaapa viapo vyote kumbe wanasingizia. Huko mahakamani kila kitu kitaeleweka. Siasa zina mambo mengi sana. Ukitaka kujua basi mfuatilie mzee Trump wa USA anavyofanyiwa vitimbi lkn yupo imara na jamii yake inamwamini. Tofauti kabisa na jamii zetu unazozisema ambazo huwa haitumii muda kujiridhisha na tuhuma au uzushi kabla ya kuhukumu. We've a long way to get to the real civilization. Hali kadhalika kama ilivyo ktk safari ya elimu ya uraia. Kama jamii lazima tutambue na kuachia nafasi mamlaka zinazohusika na upelelezi , uandaaji wa mashitaka na hatimaye usikilizwaji wa mashauri na hukumu.
Tusiwe kama nyumbu
 
Msimamizi wa sheria anafanya unyama kwa mpiga kura? Haijawahi tokea. Sasa anasimamia nini? Lazima tususe. Hatutaki kumwongezea nguvu mtu mwenye roho ya uuaji?
Wewe utakuwa na matatizo ya kiakili,tunavyombo vinavyotakiwa kudhibitisha kosa la mtuhumiwa,sio kukurupuka tu na mibangi yako kichwani na kutoa hukumu.kama tutaanza kila mtu amhukumu mwingine kwa hisia,hii itakuwa nchi ya wapumbavu. Pauline gekul yupo hapo kwa sababu ya kuruhusu mawazo ya kipumbavu kama uliyo nayo wewe.
 
Watanzania wapi hao wa kususia biashara ya mtu??? Unachekesha wewe
 
Video akifanyiwa ukatili ipo wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…