Watanzania wameyakataa kabisa majiko ya umeme, hivi ni ujinga au ushamba?

Tatizo umeme sio wa uhakika mfano unapika ugali mara umekatika si utaishia kunywa uji ndio maana watu wengi wanaishia kutumia gesi inakuwa na uhakika chakula kuiva bila shida
 
Weka basi ufafanuzi wa huo utafiti hapa
 
Nimekuwa nikitumia jiko moja la umeme watt 1500. Umeme matumizi madogo wa sh 5000 unabaki na kubaki kwa siku 30. Hapo jiko linapika wali, mboga na ugali. Jiko za kawaida hazili umeme labda uwe unazilisha
Jiko gani hilo mkuu. Weka picha na details, ndio haya wanayosema induction cooker?
 
Dhana ya majiko ya umeme iliingizwa vibaya miaka mingi iliyopita, yalionekana yanakula umeme sana.
Shida ni,Umeme kuwa ghali,Umeme kutokupatikana wakati wote na Mkaa.
 
Shida ni,Umeme kuwa ghali,Umeme kutokupatikana wakati wote na Mkaa.
Ukipiga hesabu vizuri unaweza kukuta gharama ni zilezile au zaidi ya hapo, kumbuka jiko la umeme linatumia muda mchache tofauti na la mkaa.
 
majiko ya umeme yanayofaa ni aidha infrared au induction
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…