Watanzania wana bidii ya maombi sana, bila dhana ya Mungu watakosa maana ya maisha kabisa

Haka kafilosofia ka JF hakawezi kukuelewa,...kanajikutaga kana nondo kweli,...😁😁😂😂😂😂
 
Hapa kuna mambo matatu...., Maombi ni kama confidence booster na stress removal ; Na hapa siongelei tu Mungu huyu aliyeletwa na hawa wakuja, bali hata mizimu ya mababu na Imani za asili.....;

Mbili kwahio mtu aliyepo Dodoma au huko Kijijini hana la kufanya zaidi ya kushirikia kwa kujiridhisha yeye kwamba anasaidia (be it msaada wake kwa hao hauna nguvu ila kwake huenda unamsaidia kuondoa Stress)

Mwisho kabisa kwa wahusika wanaotakiwa kuweka mambo sawa, au wale waliopo ground itakuwa ni kukosa maarifa na kutokuwa na ufanisi badala ya kuokoa watu na kupanga mikakati kupoteza hata dakika kumi kufanya maombi...., Kwa wanaotaka maombi au kufanya maombi wakafanye Kanisani hapo ground zifanyike shughuli practical na kwa watumishi wetu (Idara husika) zijaribu kuwa proactive ili kama ni uzembe usitokee tena...
 
unapiga sana kwenye mishono,...kwani sehemu zingine huoni mkuuu?😂😂🙌🙌
 
Nimekuambia kipofu unamthibitishiaje kûna Mwezi juu ya anga?
Kama utashindwa kuthibitisha itaamaanisha Mwezi haupo?
Kuna mtu alikuuliza hapo juu unazungumzia Mungu yupi?

Dhana nzima ya kupinga uwepo wa Mungu ni mkanganyiko wa sifa alizopewa katika vitabu vya dini na uhalisia wa mambo.

Kipofu akikuambia ninaweza kuendesha BMW X5 kwa spidi ya 180km/ph utaamini au utaomba uthibitisho?
 
Kwa nini unaona tunapaswa kuamini na sio kujua mkuu?
Uko sahihi Kabisa ..

Mungu anasema Tusiamini Ila Tumjue...
Neno kuamini limekaa Kitumwa Tumwa sana ni bora neno Kumjua Mungu..

Ayubu 22:21

"Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;

Ndivyo mema yatakavyokujia."

NA Hata Yesu aluwahi Kufundisha..

Yohana 8:32
"Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru."
And ye shall know the truth, and the truth shall make you free.
 
Dah Hii hoja Imebidi Nikaiprint kabisa 🤣🤣🤣
Naomba Niiweke na Kwenye Lamination🤣🤣
 
Watanzania tunampenda Mungu wa Wazungu na Waarabu lakini hatupendi.
 
Kumbe neno lenyewe linataka mtu upate kujua kwa hakika na sio kuamini tu🤔
 
Mungu yupo ndugu Hilo halina ubishi, haushangai hata taifa la wajanja zaidi marekani wanamuamini Mungu wewe ni Nani upinge,in God we trust
Mungu yupo, wapi?

Ulijuaje na unathibitishaje kwamba Mungu yupo?

Marekani kuamini Mungu yupo, sio uthibitisho wa kwamba ndio kuna Mungu kweli.

Kuamini unaweza kuamini hata uongo. Hata wamarekani wana amini kuna Dragons 🐉 watemao moto 🔥 midomoni mwao. Kwa sababu ni jambo la "kuamini" tu bila kuhitaji uthibitisho wowote ule.

Lakini tukitaka kuverify hiyo imani lazima tutake uthibitisho wa uwepo wa hao Dragons wenyewe walivyo, tuhakikishe na tuthibitishe.

Vivyo hivyo hata imani kwamba kuna Mungu, watu pamoja na wamarekani wana amini tu kuna Mungu, ila hawana na hakuna uthibitisho wowote ule wa uwepo wa huyo Mungu.

Sasa Tutahakikisha vipi na unathibitishaje kwamba kuna Mungu?

Kwa nini uhitaji kuamini Mungu yupo, Badala ya kujua kwa uhakika, ushahidi na uthibitisho kwamba Mungu yupo?
 
Nadhani Africa tuna shida, tunataja taja Mungu hovyo bila.kuwa na vitendo. Siku moja nilienda Helsinki Finland, kuna fire detector ikapiga alarm, yaani zima moto na kikosi cha uokozi kilifika ndani ya dakika 5. Watu wakaamriwa watoke na eneo likazungushiwa zile tap za tahadhari. Na hakuna mtu kusogea eneo hilo kama sio wa kikosi maalum.
Tuna kazi kubwa sana Africa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…