Watanzania wana bidii ya maombi sana, bila dhana ya Mungu watakosa maana ya maisha kabisa

Watanzania wana bidii ya maombi sana, bila dhana ya Mungu watakosa maana ya maisha kabisa

Akiwa na upumbavu katika mambo mengine lakini sio katika Hilo.
Hiyo ni kulingana na wewe.

Una amini kuna Mungu unayemtegemea, Halafu kwenye majanga, Huyo Mungu unaye mtegemea na kumtumainia haonekani akitoa msaada wowote.

Kama wewe sio Mpumbavu ni nini?

Ni uwendawazimu wa hali juu, Unakaa una amini kuna Mungu wa kukuokoa, Halafu yakitokea majanga, unaomba binadamu wenzako waje kukuokoa.

Kwa nini usi subiri huko chini ya kifusi, Huyo Mungu wako unayemtegemea aje aku okoe?
 
Mimi ili niamini tena kuna Mungu lazima nimuone. Haiwezekani kukawa na Miungu zaidi ya 3,000 lakini wa kwako ndiyo wa kweli na wengine ni wa uongo.

Baada ya kuhoji maswali yasiyokuwa na majibu ya moja kwa moja na kubaki njia panda imani yangu ilitoka 50% mpaka 0%. Sijawahi kuamini dhana ya kuwa kuna Mungu kwa 100%
Kama Mungu yupo basi hizi habari zetu za sadaka,kusali na ma hovyo hovyo mengine hayajui nafikili alijenga ulimwengu akazeeka akafa
 
Kwa Sababu Akili ya binadamu Iko limited,
Ingekuwa Akili ya binadamu ni infinity tusingekuwa na haja ya Kuamini.

Akili ya binadamu inategemea milango ya fahamu àmbayo Iko limited ili kuthibitisha uwèpo wa Jambo.

Mfano, MTU àmbaye ni kiziwi au kipofu Huwezi kuniambia kwamba anatakiwa kujua kûna kitu kinaitwa sauti ambacho tangu kuzaliwa hajawahi kukisikia.

Au Mtu àmbaye NI kipofu Huwezi kumtaka ajue uwèpo wa Nuru àmbayo tangu kuzaliwa hakuwahi kuiona.

Hivi Siku kipofu tangu kuzaliwa àmbaye hajawahi kuona Mwezi Hapo angani akikuambia hakuna Mwezi utamthibitishiaje?
Mungu anaedaiwa kwamba ni yeye kaunda akili ya binadamu iliyopo limited wala hapaswi kukasirika wengine wakisema hayupo , hapo sioni sababu ya wewe kusema asiye amini ni mpumbavu kwa sababu hata wewe unae amini hauwezi kuthibitisha unachokiamini 🤔🤔🤔🤔
 
Moto wa nyokoo ha ha ha kutishana tu mi pepo yangu ni hapa hapa duniani nikiwa furaha hapa inatosha na nikila msoto ndo moto wangu ila nafanya jitihada kimatendo ili nirudi peponi kwangu
Mkuu ni bora uamini hata kama hayupo haitakupunguzia chochote kuliko ukute yupo na haujaamini utaona cha mtema kuni, utapigwa kibiriti halafu haufi unateseka tu milele mkuu🤔
 
Mungu hausiki na mabaya au uovu wowote, wala haruhusu uovu au mabaya yatokee.
Kama Mungu hausiki na mabaya au uovu, Pia Mungu huyohuyo Hausiki na mema na mazuri yoyote.

Na Mungu huyo hayupo.
Wewe usipotambuwa kwa akili ukweli, usipojua jambo lipi ni jema utasababisha hasara, uharibifu, uchungu, maumivu na vifo; utaingilia mpangilio wa shughuli za vitu vingine.
Binadamu haihitaji Mungu yeyote yule kujua na kufanya wema au ubaya.

If a person cannot determine right from wrong, then he lacks common sense not God.
 
Mkuu ni bora uamini hata kama hayupo haitakupunguzia chochote kuliko ukute yupo na haujaamini utaona cha mtema kuni, utapigwa kibiriti halafu haufi unateseka tu milele mkuu🤔
Sasa Umkute Hayupo wapi??
Au Umkute Yupo wapi?

Mimi Mtu akinijibu Mbinguni ni wapi nitakubaliana naye vizuri..

Na Tunaenda kwa mwili Upi?
Huu wa nyama au Wa Mwili na Kama wa Nyama Vipi kuhusu Tunapokufa?
Na kama wa Roho unawezaje Kuichoma Roho ambayo ni Upepo na unawezaje kula maziwa na asali kwa mwili wa Upepo
 
Kwanza Mungu gani anatetewa na binadamu
Mungu anaye tetewa na Binadamu, Ni Mungu mdhaifu na mchovu sana.

Watu wanahangaika sana kumuongelea na kumuelezea Mungu ambaye hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe, kujitetea mwenyewe na kujidhihirisha mwenyewe yeye kama yeye, kwamba yupo.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze hadharani mwenyewe ajidhihirishe mwenyewe, ajitetee mwenyewe na ajiongelee mwenyewe kama ana huo uwezo.
 
Maisha Bila Mungu hayafai kitu Yoda

Ukiwa Mpumbavu Huwezi elewa haya Mambo.
Na Moja ya Sifa ya Mpumbavu ni upumbavu usiojificha na kujifanya, kuwaza, kusema Hakuna Mungu au kutomtegemea Mungu.
Ajabu kila mtu ana Mungu wake na kila mtu anajiona yuko perfect 100%.
Wachina ambao unawaona makafiri 100 kwa scenario ya ajali kama ile wangeweza kuokoa watu wengi zaidi kwa muda mfupi kuliko nyie mnaotajataja Mungu hovyo huku huyo Mungu hamumjui mnaishi kwa illusion tu.
 
Sasa Umkute Hayupo wapi??
Au Umkute Yupo wapi?

Mimi Mtu akinijibu Mbinguni ni wapi nitakubaliana naye vizuri..

Na Tunaenda kwa mwili Upi?
Huu wa nyama au Wa Mwili na Kama wa Nyama Vipi kuhusu Tunapokufa?
Na kama wa Roho unawezaje Kuichoma Roho ambayo ni Upepo na unawezaje kula maziwa na asali kwa mwili wa Upepo
Mkuu yesu alitwaliwa mawinguni kwenda kwa baba mbele za wanafunzi wake mbinguni itakua ni juu 🤔 na parapanda na baragumu zikilia tutamwona akishuka mawinguni kama njiwa , kila jicho litamwona , kwa kanisa lililopo Buza andika ✍️
 
Mungu hausiki na mabaya au uovu wowote, wala haruhusu uovu au mabaya yatokee.

Wewe usipotambuwa kwa akili ukweli, usipojua jambo lipi ni jema utasababisha hasara, uharibifu, uchungu, maumivu na vifo; utaingilia mpangilio wa shughuli za vitu vingine.
Tino Hapa umedanganya Mungu ndo anausika na Uovu wote na Ubaya wote..

Isaya 45:7

"Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni Bwana, niyatendaye hayo yote."

"I form the light, and create darkness: I make peace, and create evil: I the LORD do all these things."


Aisome min -me kwenye Jalada
 
Back
Top Bottom