Watanzania wana bidii ya maombi sana, bila dhana ya Mungu watakosa maana ya maisha kabisa

Watanzania wana bidii ya maombi sana, bila dhana ya Mungu watakosa maana ya maisha kabisa

Maombi huwa nahisi ni hamu ya miujiza itokee baada ya kukutana na kitu ambacho kimetuvuka uwezo kifikra na kukitatua.
Maombi yapo kwa ajili ya kujazana tumaini tu wala hayanaga vitendo vya live kwenye kusaidia mkwamo wa mtu ama situation.
MUNGU gani mpaka tumuambie(tumuombe) ndo afanye? Kwani hajui kama watoto wake watakuja kuangukiwa na ghorofa na je hajui kama wanafamilia wanatakiwa warudi kwao ila bado karuhusu wakwame kwenye kifusi wakati anajua kabisa rescue team yetu ilivyo?
Inasikitisha
 
Watu wanaomba na kufunga na kukesha hata Kama hakuna janga lolote. Ukitaka kuwazuia lete hoja nzito kuliko hizi zilizotufunga kwenye imani. Ukishindwa kwendraaaa, maana wewe Ni shetani tu Kama mashetani wengine.
 
Unaniita shetani kwani mimi ndiye nimefukia watu kwenya kifusi cha ghorofa Kariakoo?
Nimeleta hoja gani zaidi ya kuelezea kile ambacho ninakiona kinatendeka katika jamii??
 
Unaniita shetani kwani mimi ndiye nimefukia watu kwenya kifusi cha ghorofa Kariakoo?
Nimeleta hoja gani zaidi ya kuelezea kile ambacho ninakiona kinatendeka katika jamii??
Sasa kwani wewe umeona watu wamehimiza kusali baada ya ghorofa kuanguka? Ibada zipo tu siku zote. Akina mwamposa wanafanya ibada kila siku,

Wewe Ni shetani ndio, unashawishi watu waache kumuomba Mungu wao huna maana, sio mfano mzuri wa kuigwa.
 
Tino Hapa umedanganya Mungu ndo anausika na Uovu wote na Ubaya wote..

Isaya 45:7

"Mimi naiumba nuru, na kulihuluku giza; mimi nafanya suluhu, na kuhuluku ubaya; Mimi ni Bwana, niyatendaye hayo yote."

"I form the light, and create darkness: I make peace, and create evil: I the LORD do all these things."
DR MJ sio kila kilichoandikwa kwenye biblia ni neno la Mungu.

Biblia ni chanzo msingi katika kutafuta na kujua ukweli. Lakini hatuwezi kutegemea biblia peke yake katika kuthibitisha huo ukweli.
 
DR MJ sio kila kilichoandikwa kwenye biblia ni neno la Mungu.

Biblia ni chanzo msingi katika kutafuta na kujua ukweli. Lakini hatuwezi kutegemea biblia peke yake katika kuthibitisha huo ukweli.
😳😳😳
Hii Mpya min -me nisaidie Mimi nimeishiwa Nguvu huku..
Sasa Ukweli nina upataje kama Biblia sio Neno la Mungu
 
Mkuu ni bora uamini hata kama hayupo haitakupunguzia chochote kuliko ukute yupo na haujaamini utaona cha mtema kuni, utapigwa kibiriti halafu haufi unateseka tu milele mkuu🤔
Ubongo mdogo alionipa ndo umegundua yeye hayupo sasa atanichomaje moto yaani unaleta habari za umetengeneza baiskeli bila break alafu ikikuvunja miguu hapo utamlaumu nani?
Ni sawa yeye alivyotushushia li shetan hapa duniani alafu limetuzoa wote zambini alafu atatuchomaje moto na wakati katuletea matatizo ye mwenyewe
 
Hii Mpya @min -me nisaidie Mimi nimeishiwa Nguvu huku..
Sasa Ukweli nina upataje kama Biblia sio Neno la Mungu
Ukweli unatafutwa kwa kufikiri na kufanya uchunguzi. Kusoma biblia au kuhudhuria masomo darasani bila kufikiri na kufanya uchunguzi hakufanyi mtu kupata maarifa.
 
Katika mkasa wa jengo la Kariakoo kuanguka nimewasikia watu wengi wanaotegemea watu kutolewa au ambao waliangukiwa na jengo wakiomba na kushukuru Mungu, Allah au Yesu katika mkasa huo mkasa. Kila posti niliyosoma mtandaoni, kila clip au maongezi ya kila mtu aliyefukuliwa huwezi kuyakosa haya maneno(Maombi, Mungu, Allah, Ya Rabbi, Alhamdulillah na Yesu)

Hakika Watanzania dini imewakaa, ni viumbe wa kidini, bila dini na mungu sidhani kama wana tumaini lolote au muelekeo wowote wa maisha.
Wasikutishe,watanzania ni washirikina sana wanajifanya wako karibu na Mungu adharani ila kwa waganga ndio wenyewe
 
Ubongo mdogo alionipa ndo umegundua yeye hayupo sasa atanichomaje moto yaani unaleta habari za umetengeneza baiskeli bila break alafu ikikuvunja miguu hapo utamlaumu nani?
Ni sawa yeye alivyotushushia li shetan hapa duniani alafu limetuzoa wote zambini alafu atatuchomaje moto na wakati katuletea matatizo ye mwenyewe
Umepewa machaguzi mkuu🤔🤔 wewe binafsi ,bila yeye kukuingilia ukichagua motoni ni wewe mwenyewe tu yeye hausiki😂😂😂
 
Ukweli unatafutwa kwa kufikiri na kufanya uchunguzi. Kusoma biblia au kuhudhuria masomo darasani bila kufikiri na kufanya uchunguzi hakufanyi mtu kupata maarifa.
Kwa bahati mbaya Sana mambo ya Imani Ukishaweka Fikra tu na Uchunguzi yote unayapoteza..
Kwa Sababu huwezi Kujenga Hypothesis Based on Something which has Not even evidently..

Ukiingiza Uchunguzi wa Kiakili basi Dini na imani yote unaipoteza hakuna Dini wala Imani kwenye Uchunguzi wa Kiakili wapa Tafakuri ya Kina..

Na ndo maana Magumu yote kwenye Imani Huitw fumbo la Imani
 
Back
Top Bottom