Kuna code ngumu sana kuelewa pale kwenye andiko.
Hakuna cha code bhana. Watu ni lazima wamshukuru Allah kwa kila kitu. Hivi ndivyo tunavyofundishwa Waislam. Na hatuachi kumuomba Allah katika hali zote. Dua kwetu ni 'Ibada.
Sisi waafrika tumepewa mambo mengi na mwenyeezi Mungu ila kwa sababu ya giza lililopo kichwani tumeshindwa kuona mwanga.
Na ndio maana tunamshukuru Allah kwa neema zake kwetu na kwa kila kitu tukijua kuwa kuna hikma katika kila aliloliqadiria. Na hatuachi kuomba kheri kutoka kwake. Watu wanamshukuru Allah na kumtukuza, wewe unaumizwa na nini?
Bado kumtajataja sana Mola kila eneo/sehemu siyo ishara ya wema au kwenda peponi, wala haisaidii chochote kwake.
Kumkumbuka Allah na kumtaja ni katika sifa njema za waumini. Ni katika sifa nzuri kwetu Waislam. Kumtaja sana Allah na kumkumbuka ni sifa nzuri kwetu Waislam.
"Na kwa yakini kumdhukuru Mwenyezi Mungu ndilo jambo kubwa kabisa"
(Qur'an 29:45)
"na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa."
( Qur'an 62:10)
"na wanao mdhukuru Mwenyezi Mungu kwa wingi wanaume na wanawake, Mwenyezi Mungu amewaandalia msamaha na ujira mkubwa."
(Qur'an 33:35)
41. Enyi mlio amini! Mdhukuruni Mwenyezi Mungu kwa wingi wa kumdhukuru.
42. Na mtakaseni asubuhi na jioni.
(Qur'an 33:41-42)
Kuna dhikr na kumkumbuka Allah kulikothibiti katika kila mnasaba. Ikiwemo kwenye msiba.
Na Dua ni ibada kwetu Waislam.
And yes, kumdhukuru Allah kwa wingi ni katika sababu ya kufanikiwa na kuingia Peponi. Allah atuingize katika Pepo yake.
Na unaposema haisaidii chochote kwa Allah tunapomkumbuka na kumtaja sio kweli.
152 from Surah Al-Baqarah
﴿فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ﴾
[ البقرة: 152]
Basi nikumbukeni nitakukumbukeni, na nishukuruni wala msinikufuru
Hivyo usimzungumzie Allah bila elimu.
Waafrika dini zimetulevya sana kuliko vile tunavyotakiwa kuiendea hiyo dini.
Hatuachi kumdhukuru Mola wetu. Allah atuweke katika kundi la WachaMungu na atufishe katika Tawheed na Sunnah.
Mfano mdogo; Kama Japan wangekuwa kama wewe, ile nchi isingekuwepo, kila wkt majanga ya matetemeko ila kwa sababu ya kutumia akili wanapata taarifa kabla tetemeko halijatokea.
Mimi siwaangalii Wajapan, naangalia Mola wangu kaniamrisha nini. Kama wajapan hawamshukuru Allah kwa neema alizowapa na hawamdhukuru na wala kumuabudu Yeye peke yake bila ya kumshirikisha na chochote, ni tatizo kwao na ninasikitika kwa hilo. Namshukuru Allah kwa neema ya Uislam na Sunnah na ninamuomba Allah anifishe katika Uislam. Aameen. Namuomba pia azidi kuueneza Uislam katika ardhi ya wajapan. Aameen.