Watanzania wana bidii ya maombi sana, bila dhana ya Mungu watakosa maana ya maisha kabisa

Watanzania wana bidii ya maombi sana, bila dhana ya Mungu watakosa maana ya maisha kabisa

Katika mkasa wa jengo la Kariakoo kuanguka nimewasikia watu wengi wanaotegemea watu kutolewa au ambao waliangukiwa na jengo wakiomba na kushukuru Mungu, Allah au Yesu katika mkasa huo mkasa. Kila posti niliyosoma mtandaoni, kila clip au maongezi ya kila mtu aliyefukuliwa huwezi kuyakosa haya maneno(Maombi, Mungu, Allah, Ya Rabbi, Alhamdulillah na Yesu)

Hakika Watanzania dini imewakaa, ni viumbe wa kidini, bila dini na mungu sidhani kama wana tumaini lolote au muelekeo wowote wa maisha.
Hujaeweka mkuu kwahiyo watu wasimwabudu Mungu??au wasiwe na tumain na Mungu wamtumain Nani?
 
Nini Dolphin na Sokwe katika historia ya kuwepo kwao wamefanya mathalani uvumbuzi na ugunduzi?
Sijawahi Kuwa Dolphin au Sokwe Huenda Wamevumbua Vingi na wanavyo vingi vya Kujisifu na Kuambizana..

Kuna Kitu ambacho tunajisahau wanadamu Kujiona Sisi Ni bora kuliko wanyama wengine bila Kujua Maisha yao hao wengine wanaishije..

Unafikiri Binadamu alihitaji Huo Ugunduzi ili kuwa Bora kuliko wengine??

Mhubiri 3:18-20

"18 Nikasema moyoni mwangu, Ni kwa sababu ya wanadamu, ili Mungu awajaribu, nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama.

19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.

20 Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena."
 
Sijawahi Kuwa Dolphin au Sokwe Huenda Wamevumbua Vingi na wanavyo vingi vya Kujisifu na Kuambizana..

Kuna Kitu ambacho tunajisahau wanadamu Kujiona Sisi Ni bora kuliko wanyama wengine bila Kujua Maisha yao hao wengine wanaishije..

Unafikiri Binadamu alihitaji Huo Ugunduzi ili kuwa Bora kuliko wengine??

Mhubiri 3:18-20

"18 Nikasema moyoni mwangu, Ni kwa sababu ya wanadamu, ili Mungu awajaribu, nao waone ya kuwa wao wenyewe wafanana na wanyama.

19 Kwa maana linalowatukia wanadamu linawatukia wanyama; jambo moja lawatukia; anavyokufa huyu ndivyo anavyokufa huyu; naam, wote wanayo pumzi moja; wala mwanadamu hana kitu cha kumpita mnyama; kwa maana yote ni ubatili.


20 Wote huendea mahali pamoja; wote hutoka katika mavumbi; na hata mavumbini hurudi tena."
Mtu mwenye akili anatambuwa kwa akili uongo na ukweli, anajua jambo jema na baya.

Mhubiri anatufundisha tutafute kujua ukweli badala ya mivuto au vitu, maslahi au mang'amuzi binafsi.
 
Watu wamejaribu kutafuta elimu ya uumbaji kwa namna mbalimbali lakini wapi bado wanafeli. Wamedai kuhusu evolution lkn imepwaya haikidhi kujibu maswali ya kibinadamu.
Wamehamia kwenye maanunaki lakini kukonect baadhi ya dot imeshindikana, ukiwauliza elimu hiyo imetoka wapi wanajichanganya Mara oooh! Tunakusanya taarifa mbalimbali ambazo hazina uhakika.

Walikuja na bigbang lkn bado inamapancha kibao.
Biblia pekee ndiyo yenye ujumbe ambao unakidhi vigezo na kubeba ujumbe timilifu, maana hata Kama Kuna makosa ya uandishi bado hayaondoi dhima ya ujumbe uliokusudiwa. Sasa watu wanajaribu kumvuruga mtu wa imani kwakuleta vikwazo kibao. Mara ooh mazayuni, oooh Mungu inatakiwa aonekane , oooh roman empire iliiba kurasa za kweli basi tu ilimradi aipinge biblia. Lkn Bible inaishi, neno la Mungu halistopishwi na mawazo ya watu uchwara na litaendelea kuchagua wateule wake Kama lilivyokusudiwa.
 
Kwa sababu maisha Nayo hayako Static yako dynamic na matatizo huongezeka na Utatuzi ubadilika
Katika kuishi, na katika kutatua au kukabiliana na matatizo, yanahitajika maarifa zaidi ya kitu chochote.

Maarifa yanakua. Maarifa tulionayo leo hayatakuwa sawa na maarifa ya miaka 2000 ijayo.

Hii ina maana gani? Mambo ambayo hatuyajui leo au ambayo hayajulikani vizuri sasa yanaweza kujulikana wazi baadaye.

Kwa hiyo utafiti au uchunguzi ni shughuli endelevu kwa sababu maarifa yanakuwa na kuendelea.
 
Ila wakoloni walikuwa mafundi sio tu kututawala na kutunyonya hata dini kiukweli wamejua kutupandikiza
I wish waafrica tungebaki na dini zetu
 
Ila wakoloni walikuwa mafundi sio tu kututawala na kutunyonya hata dini kiukweli wamejua kutupandikiza
I wish waafrica tungebaki na dini zetu
Hakuna Cha dini zetu, zilikuwa na kasoro, masharti kibao, Kuna kuchinja, wajawazito wasile mayai, matambiko ambayo Ni ibada za kishetani tu, kuchanja chale. Someni biblia mtagundua hata chanzo Cha imani hizo za dini za asili
 
Ifike hatua tukubali tu akili kubwa itawale ndogo. Hata Kama tutaamua kugeuza biblia kuwa imeandikwa na wazungu kwania ya kututawala, bado utakubaliana na Mimi kuwa wametuzidi mbali kiakili.

Kiswahili tu bado kinagombea uhuru katika nchi yake na hakijapata hadi leo.
Ccm tu imewabana koromeo hata pakupumulia hamna , mmebaki Kama mazwazwa, bendera fuata upepo. Na uchawa.

Nmeshindwa kujitoa ktk Mambo madogomadogo Kama hayo mtawezaje kujikwamua kwa Yale mengi makubwa?

Shida za wajinga haziishi. Trump aliwaambia ukweli mkadai anawatukana.
Na Wala hamna sababu yoyote ya kuona imani kwa mtazamo wa njia yakutawaliwa Bali Ni uzamwamwa wenu tu unawasumbua.
Mbona wazungu kibao tu wanachapa injili Kama hawana akili nzuri.
Mnatumia upagani kuhalalisha umafia wenu. Mungu yupo na ataendelea kuwepo.
 
Hapa kuna mambo matatu...., Maombi ni kama confidence booster na stress removal ; Na hapa siongelei tu Mungu huyu aliyeletwa na hawa wakuja, bali hata mizimu ya mababu na Imani za asili.....;

Mbili kwahio mtu aliyepo Dodoma au huko Kijijini hana la kufanya zaidi ya kushirikia kwa kujiridhisha yeye kwamba anasaidia (be it msaada wake kwa hao hauna nguvu ila kwake huenda unamsaidia kuondoa Stress)

Mwisho kabisa kwa wahusika wanaotakiwa kuweka mambo sawa, au wale waliopo ground itakuwa ni kukosa maarifa na kutokuwa na ufanisi badala ya kuokoa watu na kupanga mikakati kupoteza hata dakika kumi kufanya maombi...., Kwa wanaotaka maombi au kufanya maombi wakafanye Kanisani hapo ground zifanyike shughuli practical na kwa watumishi wetu (Idara husika) zijaribu kuwa proactive ili kama ni uzembe usitokee tena...


Hebu nipe ufafanuzi wa "bali hata mizimu ya mababu na Imani za asili.....;" Maana Tanzania ya leo ni nadra sana kuona hao waumini wa mababu na mizimu ya asili....1
 
The God gene hypothesis proposes that human spirituality is influenced by heredity and that a specific gene, called vesicular monoamine transporter 2 (VMAT2), predisposes humans towards spiritual or mystic experiences.
 
Na ninyi mnaotumia kingereza kwenye post zenu humu mkome, wajinga.
Bado mnaonesha Ni jinsi gani mlivyo mazwazwa. Mnatumia lugha za kigeni ili tujue mmesoma au! Hiyo Ni lugha tu. Bahati mbaya sana ukishakuwa msomi mzuri Tanzania alafu na ukajua hako kakiingereza chako inakuwa ndio ngao yakutambia wajinga mkasahau kwamba kwa wenye lugha yao unaonekana fala mzuri tu kutokana na rafudhi 😃 huna tofauti na mzenji kwa rafudhi ya kiswahili hapa tz, watu watakuenjoy tu, mwenyewe unajiona umemaliza kila kitu.
Wasomi wetu Ni kwaajili ya nchi yetu.
 
Hebu nipe ufafanuzi wa "bali hata mizimu ya mababu na Imani za asili.....;" Maana Tanzania ya leo ni nadra sana kuona hao waumini wa mababu na mizimu ya asili....1
Who cares kama ni nadra au hata yupo mmoja au wawili..., Sababu Imani ni Imani kwahio anayeamini hizi zilizokuja na Merikebu na anayeamini hizo za mababu zetu wote ni Imani tu... Na kama nilivyosema sababu hizi ni confidence booster hata ukiamini Chale au Hirizi uliyovaa vyote vitakusaidi kwa kukupa Confidence kuamini kwamba kuna Super Power inakusaidia (Sasa tukitaka tuangalie authenticity ya hizo imani..., that's a different ball game)
 
Back
Top Bottom