Watanzania wanaishi Nchi ya Uchumi wa Kati?

Umepata likes kadhaa[emoji3]
 

Mh Zitto, wewe unajinasibu ni mchumi, umefanya uchambuzi wa kina kuhusu namna Pato la Taifa linavyototolewa, lakini unahitimisha kinadharia nyuma yake ukiwa na malengo binafsi na ya kisiasa.

Kama unakiri kumekuwa na ongezeko la $3 kila mwaka katika awamu hii ya utawala; kama unakubali utawala umetumia fedha nyingi katika km kununua ndege na kuwekeza katika miradi mikubwa, kwa nini huoanisha uwekezaji huo kama kichocheo cha kukua kwa uchumi?

Kwamba kwako wewe hiyo fedha ungewekeza kwenye kilimo wakati unajua bayana kilimo pasipo kuwa na soko, miundo mbinu imara ya usafirishaji na mazingira rafiki kwa mkulima kuongeza tija katika kilimo, ni sawa na ndoto za mchana.

Labda unajisahaulisha au kukwepa, kwa makusudi, kwamba pamoja na kuwa Mbunge kwa kipindi kirefu hukuweza kuinua kilimo cha Michikichi jimboni kwako kama zao kuu la biashara hadi Serikali iliyoko madarakani kufanya hivyo. Na hata vile badala ya kushirikiana nayo umekuwa ukiilaumu kuhusu zao la korosho ambalo si zao la jimbo lako (charity begins at home)

Unajua, kama mchumi, na ndicho kinachofanywa na Serikali iliyoko madarakani, kujenga mifumo imara (huduma za jamii) na kuimarisha miundo mbinu, kunachochea kukua kwa uchumi na hatimaye kupanua wigo wa kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika uchumi wake mwenyewe na wa Taifa.

Kwa hoja hiyo natoa mfano wa mkulima (umependa kuzungumzia kilimo):-
√ Kuwepo kwa usafiri wa uhakika wa majini, ardhini na angani, kunamhakikisha kufikisha mazao yake ya kilimo (japo kidogo anachozalisha) kwenye masoko yaliyo mbali. Kama si yeye wataenda wafanyabiaashara wa mazao kununua;
√ Kuwepo kwa viwanda kunamwongezea mkulima huyo soko la mazao yake ya kilimo; na
√ Kwamba Serikali inaboresha na kupanua huduma za jamii, kunaimarisha na kuongeza uwezo wake mkulima kiafya na kiakili kumudu changamoto za maendeleo yake mwenyewe.

IWEJE UPOTOSHE MAANA YA KUONGEZEKA KWA PATO LA TAIFA.

Natumaini, wakati tukielekea kwenye Uchaguzi Mkuu, chama chako kitaweka hadharani Sera na Mikakati mbadala ya maendeleo ambayo itaendeleza yaliyofanywa na Serikali iliyoko madarakani, kama ulivyokiri, nanukuu Ni muhimu sana kutambua kuwa kufikia hatua hii ni mchango wa awamu zote zilizotangulia na wananchi wa Tanzania na si matokeo ya awamu moja au miaka 5 tu

Unahitimisha andiko lako, lililojaa kebehi tupu, kwa kuaminisha WaTz kuwa mkiingia madarakani ni #KaziNaBata, pasipo kueleza ni kazi zipi za kumpata huyo Bata? HapaKazi Tu# angalau imewezesha kipato kuongezeka kwa $3 ikiwa ni pamoja na uwekezaji mkubwa kwenye vichocheo vya maendeleo.
 

Maelezo mazuri, ila yapo kinadharia zaidi. Kama wakulima wana hali hiyo, mbona huko vijijini wenye ardhi ndio wanatutegemea sisi wa mjini tuwatumie hela ya kuendesha maisha? Mfano ukiwa barmaid hapa mjini, na kuishi nyumba ya kupanga, utajikuta unaishi vizuri kuliko mtu anayemiliki nyumba kijijini na shamba la heka 5. I stand to be corrected.
 

Swali chokonozi hasa kwa upande wa kilimo. Hivi akikujia mkulima mwenye heka 5 kijijini, na kuishi kwenye nyumba yake, na barmaid anayeishi hapa mjini kwenye double room ya kupanga, wakakukopa 1m@. Ni yupi utafunga roho kumpa ukitarajia hiyo hela kurudi baada ya mwaka?
 
Kama nimekuelewa kwako wewe fedha au pesa ndiyo msingi wa maendeleo, dhana inayobebwa na wanaopinga kuwa Tanzania siyo nchi ya Kipato cha Kati?
 
Sijauelewa mlinganisho wako wa Barmaid na Mkulima, watu wawili wenye vipato na maisha tofauti kabisa, katika muktadha wa mjadala unaoendelea.
 
Sijauelewa mlinganisho wako wa Barmaid na Mkulima, watu wawili wenye vipato na maisha tofauti kabisa, katika muktadha wa mjadala unaoendelea.

Unaelewa maana ya swali chokonozi?
 
Kama nimekuelewa kwako wewe fedha au pesa ndiyo msingi wa maendeleo, dhana inayobebwa na wanaopinga kuwa Tanzania siyo nchi ya Kipato cha Kati?

Msingi wa maendeleo ni nini? Maana naona wote wenye maendeleo ni wenye hela.
 
MATAGA hawapendi hizo nondo maana zinawakata stimu ya MAYOWE yao ya Uchumi wa kati.
 
Msingi wa maendeleo ni nini? Maana naona wote wenye maendeleo ni wenye hela.
Inategemea ni maendeleo gani kwa hiyo hela? Kwa tafsiri finyu ya maendeleo ndiyo hiyo uliyoitaja
 
Contrary to the fact ndio maana kuna nchi zimedai economic rebase to reflect activities of their sorrounding.

Asilimia kubwa ya watu wa mjini including yourself wakienda kutembea vijijini wakirudi mjini wengi wanarudi kwa kupewa zawadi za nafaka kama sio gunia basi debe au mfugo au ata wakinunua masokoni ni way cheaper kushinda wanapoishi.

Tatizo la ugumu wa vijijini ni kuweza kupata masoko ya uzalishaji kitu ambacho Magufuli anawapigania.

Sijui wewe mimi binafsi nikienda huko kijijini kwetu Nyabula hizo zawadi ni kushinda unachowapa wao.

Magu anapigana kuwapatia hawa access ya masoko mkuu tumuunge mkono. It’s about social utility (we have to look at the bigger picture) pamoja na weakness zake.

Watu kama Zitto wapo kwa ajili ya kuvunja jitihada kwa sababu awaelewi malengo ya Magufuli.

Kuna wakati wa kusikiliza upuuzi wa Zitto hila sio kipindi hiki for now kila mtu anatakiwa kuelewa Magufuli anataka kutupeleka wapi.
 
Zitto pamoja na kuwa umejitahidi kuchambua, ila uchambuzi wako unaelezea upande mmoja tu. Kwa nini msilinganishe pia na namna serikali ilivyo fanya "Government Expenditure" ukilinganisha na serikali zilizopita? Ukiangalia kwa kutumia hizo statistics za expenditure utaona serikali ya awamu ya 5 imejenga uchumi ambao inakua rahisi zaidi kufikia malengo tunayoyaona sasa na yale ya 2025. Kuhusu kukopa, nadhani wewe mwenyewe unafahamu kwa jinsi serikali yetu inavyojitegemea kwa kila jambo, hilo sidhani kama ni tatizo. Tunachoamini watangulizi wa Dkt Magufuli walifanya kazi kubwa ila awamu ya 4 ilijaaa rushwa na wizi wa kupindukia kiasi kwamba hicho kilichokuwa growth lilikuwa bomu kama ilivyo Kenya. Nadhani tutakubaliana uchumi imara na endelevu ni ule unaojengwa ktk mazingira ya uadilifu, na ndiyo maana nchi kama Norway pamoja na udogo wake lakini hawana malalamiko eti sijui ya kukopa.

Hivyo acheni kupotosha, tuangalie pia uwekezaji wa serikali awamu ya 5 vs awamu zilizopita.
 
Zitto sometimes ukitulia akili yako inafanya kazi vizuri Sana Kama ulivyo fanya hapa uchambuzi murua kabisa

Ila Sasa muda mwingine sijui huwa unawekaga wapi kichwa chako
 
Zitto ni mchumi kinadharia na mpotoshaji kutimiza lengo lake kisiasa.

Nafahamu ana uelewa mkubwa wa Nizania za kifedha (km mapato na matumizi). Upotoshaji wake ni pale anapojikita kwenye mapato kuliko matumizi. Kwamba kipato cha Mtanzania wa kawaida akiashirii nchi iko kwenye Kipato cha Kati na wanaomuunga mkono tindo, mmawia, Savimbi Jr, Mafinanga, nk.

Mwananchi wa kawaida, na hata mwenye kipato kizuri, huathirika kimaendeleo kama gharama za maisha zitaongezeka. Hizi ni gharama za elimu, afya, maji, nishati na usafiri. Serikali ikipanua na kuboresha sekta hizo, hajuna shaka hata kipato kidogo kitamwezesha mtu kumudu gharama za maisha na kubakisha kiasi kwa ajili ya maendeleo yake.

Iko mifano kadhaa inayothibitisha Serikali iliyoko madarakani imezingatia HOJA hiyo na ndiyo maana inawekeza fedha nyingi kwenye miradi ya "maendeleo vitu" badala ya kuwaongezea mishahara watumishi wake. Idadi yao halingani kabisa na WaTz wengi ambao zaidi ya 70% wanaishi vijijini kuliko na huduma hafifu za elimu, afya, maji, usafiri na nishati.

Mwanakijiji gani mgonjwa wa figo angeweza kumudu gharama za tiba yake? Mwanakijiji gani angeweza kumpeleka chekechea wake kwenye shule za awali kwa gharama zaidi ya TZS milioni? Huyu mwanakijiji apotezae muda wa kuzalisha mali apate kipato cha kumudu gharama za maisha, anahangaika kutafuta kuni au maji!

Ukweli unabaki ukweli kuwa wanasiasa waje na hoja zenye kulenga kumpunguzia Mtanzania gharama za maisha.
 
Zito kaleta hoja objective sana mlivyo na akili finyu mnaleta ngonjera.
 
Hivyo ukiwa kama kiongozi na mwana uchumi unashauri serikali ichukue hatua zipi ili kufikia lengo hiyo 2025..??
Hatua kaongea tumewekeza kwenye ndege zaidi inayotumiwa na 5%
Kashindwa kwenye kilimo 67%
Unataka ashauri nini chengine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…