Watanzania wanaosoma Urusi huwa wanachezewa akili na Warusi?

Watanzania wanaosoma Urusi huwa wanachezewa akili na Warusi?

we humuoni Lukuvi mana nae alienda huko miaka ya 1970s kwa course ya wiki moja kuchukua certificate ya political science...............VODKA inahusika hapa
mkuu itakua na wewe ni wale wale wanaotajwa hapa maana hakuna certificate ya wiki moja..
 
Nazungumzia watanzania waliosoma Urusi kwakuwa ni hao ambao ninawafahamu vizuri pengine na wa nchi nyingine wapo hivyo pia lakini sifahamu.

Kikubwa ni kwamba wasomi wengi waliosoma nchini Urusi wakirudi na wakarudi nchini wengi wao huwa wanakuwa hawana akili nzuri, nimefatilia hilo kwa kipindi kirefu sana.

Nina baba yangu mdogo alisoma Urusi kwa kipindi cha kipindi cha miaka saba aliporudi nchini amekuwa mlevi wa kupindukia haeleweki kabisa mambo anayoyafanya wakati alipokuwa akiondoka alishakuwa daktari mzuri tu.

Mwingine ni mjomba wa rafiki yangu wa karibu, yeye siku ambayo mjomba wake anafika airport walimshangaa kwakuwa jinsi walivyomkuta hawakutegemea kabisa alikuwa kama chizi chizi tu na muda huu ninapoandika thread hii mjomba wa rafiki yangu huyu ni kichaa kabisa.

Ni wengi sana ninaowafahamu walienda kusoma Urusi wakiwa na akili nzuri tu na waliporudi wamerudi wakiwa hawana akili timamu kabisa yaani wanakuwa hawaeleweki eleweki kabisa.

Nikawa nafikiria pengine wakifika nchi za watu wanaiga sana tabia ya kunywa pombe kwakuwa wenzetu wa Urusi wanakunywa sana pombe hivyo pombe hizo zinawaathiri nikagundua kuwa sikweli kwakuwa hata Ujerumani ni wanywaji wazuri sana wa pombe lakini watanzania wanaosoma huko hawapo kama ndugu zetu (wengi) walisoma Urusi.

Je? Warusi huwa wanachezea akili za Watanzania? hili tatizo lipo kwa watanzania tu?

Duuh basi inategemea mana mm nina bro wangu kasoma mpk master Russia yupo vizuri na anakula shavu now vilevile kuna classmate wangu kamaliza degree now yupo USA army anakula bata
 
mkuu itakua na wewe ni wale wale wanaotajwa hapa maana hakuna certificate ya wiki moja..

mkuu certificates zipo hata za siku moja.... mfano workshop mbalimbali hufanyika siku 1 au mbili au wiki..


participants wanapewa =>certificates of attendance
 
Nina kaka yangu kasomea urussi na sasa ni assistant lecture wa university flani hapa bongo.....huyu jamaa ni matatizo ile mbaya yaan namshangaaga sana judgemements zake

aliporudi alikuwa na pombe za kufa mtu kwenye mabegi mawili
 
aisee..ukweli kuna jambo kt nchi hyo.ata mm wpo ninao wajua walio wahi kusoma urusi na kurudi kuambulia O".
Ninyi...acheni kuwa zushia...! Warusi, Mbona mwalimu (alisomewa Urusi) wangu bado yuko fiti na anaendesha shirika la Serikali bila matatizo tena huyo alikuja na mke wa kirussia kabisa...!!
 
.....
Ushauri: Serikali isiwe inawatelekeza hawa watoto na vijana wetu walio kule. Iwe inajaribu kufanya follow ups na kujua maendeleo yao academically. Elimu ya Russia ni nzuri sana, lakini kuna udanganyifu wa hali ya juu kwenye kupata marks na hatimaye cheti.

Ahsante sana kwa maelezo yako . naomba ufafanuzi juu ya udanganyifu wa kupata marks na hatimaye cheti.
 
Ila hiu inawezekana, nilikua na headmaster wangu pale kahama wigehe anaitwa makonda nae alisoma huko,dah alkua na wenge balaaaa
 
Mimi Nafikiria ni Tatizo la Mtu mwenyewe na Sio warusi. Mimi nawaelewa wengi waliosoma na Hivi sasa wanamafanikio ya kutosha nakutajiaa.
1. Kuna Daktari wa Wanawake yuko Mnazi mmoja Zanzibar anaitwa Dr. Juma ambaye hata Muhimbili wanamtumia yeye wiki mara mo anakwenda Muhimbili.
2. Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar vile vile Kasoma Urusi Jina Dr. Garu
3. Dr. Talib Ali yeye kamaliza Urusi, kafanya kazi Muhimbili miaka miwili, baadaye kaenda Amerika kasoma na hivi sasa kaanzisha Detal clinik ya kwake mwenyewe karibu na washington nenda inaitwa AVATAR Dental clinic
Na wengi ninawaelewa
4. Mimi mwenyewe nimesoma Urusi, Baadaye nimefanya kazi Tanzania miaka 5, na Hivi sas niko Ujarumani na nafanya kazi kwenye Consulting Company kwa miaka 10 hivi sasa kama Structural Engineer

Tatizo liko kwo wenyewe

Hongera sana
 
Mimi ninayo mifano miwili tu. Nahisi lipo tatizo kubwa ambalo limefungiwa macho. Hao wawili waliondoka hapa wakiwa vizuri tu. Wamerudi wote wakiwa punguani.
 
Aisee kuna ukweli juu ya hili. Mimi namfahamu mzee mmoja kaka yao na akina Joyce Mhavile (yule wa ITV) nae alisoma huko Russia ni chapombe balaa na ni kama kadata hivi. Tumepotezana miaka mingi sana sijui kama yupo hai ila ni mzee maarufu sana alizoea kutembelea Kinondoni na Mtoni kwa Azizi anajulikana kama Mzee Mhavile.
Inabidi nimcheki classmate wangu naye yupo huko Urusi mwaka wa9 sasa kazamia. Ntaongea na nduguze juu ya hili make nae nasikia siku hizi ni mzee wa mvinyo sana wakati wazazi wake wanamtegemea.
 
Jamani mmesahau na jambo moja,sio kuwa machizi tu Bali hukana dini zote na kusema hakuna MUNGU,nawajua watano akiwemo kingunge,wakirejea tu wanajitoa mwenye dini na kusema hakuna dini wala MUNGU.
 
Wote wanarudi na watoto wa kirusi. Mfano prof mwampamba, dr balampama nk. Ukitaka kwenda class mtoto anakubembeleza mpate mavitu.
 
hii ni kweli kuna mshua wa best yangu apa alirud miaka ya 1990 akaja na mavideo redio na vitu km imbavyo bongo kumilik ilikuwa ndoto..sasa alipoenda mara ya pili sa iv karud haelewek anawashaur wtt wake akiwepo rafk yangu aache chuo waende nae russia na mzee kashakanyaga 67 years now
 
Back
Top Bottom